Nimependa nisipopendwa, Navumilia tu..ila maisha lazima yaendelee

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Heshima kwenu wakuu,

Hivi kwanini watu hawana roho ya huruma kwa wale wawapendao? ni Jeuri ya kupendwa na watu wengi au?

Unakuta umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama Watsapp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status.

Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu?
Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote.

Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae.

Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande!

Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee. Mia
 
nyie wengi matapeli tu wa mapenzi hata mtu awe malaika mtamliza tu
so tulie wote
Tatizo haufanyi uchunguzi kabla ya kuingia kwenye uhusiano na mtu,yani umetongozwa mchama halafu usiku unatoa jibu bila kujiridhisha tabia za uyo mtu kama ni nzuri au ni mbaya.Ukiachwa ndio unanza kusema sikujua kama uyu ni player wakati ulikua na mda wa kumchunguza na kujiridhisha kama anakufaa au hafai.
 
Pole sana, aliponasa pakigeuka pachungu ataanza kujibu text zako.
 
Hata mioyo inaDelete Button tuzitumie kwa Ufasaha......
 
Heshima kwenu wakuu,

Hivi kwanini watu hawana roho ya huruma kwa wale wawapendao? ni Jeuri ya kupendwa na watu wengi au?

Unakuta umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama Watsapp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status.

Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu?
Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote.

Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae.

Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande!

Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee. Mia
Katafute fweza mkuu, pesa ndio kila kitu.
 
Suluhisho la mwanaume kuzuia kuumia kwa ajili ya mapenzi, unatakiwa uwe na mademu wengi ili upendo uugawe kwa hao wote..
Ili muda huu akikuumiza huyu badae uko kwa yule anakuliwaza.

Its my principle
 
Kuna dada alinifanyia hivyo nikichomfanyia haya sahau milele
Ana bahati tu angestukia naenda mposa afu naoa mwingine
 
Mwenzako hakuwa na habari na wewe, ungemposa ukaoa 10, angekucheka tu unavyojitesa
 
Kwanini ujitese aisee?

Sometimes inabidi uwe 50/50 tu mapenzi yenyewe zengwe tu
 
Love has seasons like times of the year, sio muda wote katika mahusiano yenu mtakua mnachat kwa wingi there are tyms inatokea hivo,ukiona anakupuuza sana muweke karibu muulize watsap, otherwise na wewe punguza kumtafuta ili akumiss,Don be too available law of demand and supply inaapply hata kwenye mapenzi
 
Sijawai fanyiwa ivyo.Ila mimi nawafanyiaga wengi tu ako ka mchezo.Sana sana wanao jifanya wame fall in love kwangu
 
Back
Top Bottom