TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Tukiacha maumivu ya mwili na usumbufu walioupata mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzake baada ya kutekwa na watu wasiyojulikana lazima tukubali kuwa Kisaikolojia pia watakuwa hawako vizuri. Maumivu ya mwili na usumbufu ni mambo ya muda tu lakini kuathirika kisaikolojia kama lisipochukuliwa kwa uzito kwake hapana shana wahanga wanaweza kupata matatizo ya kudumu.
Binafsi nimefurahishwa na jinsi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe anavyolishughulikia suala hilo. Hapana shaka kwamba matukio kama haya yanapotokea, watu wengi Marafiki na hata Maadui wa Wahanga wanakuwa na mihemuko michache yenye nia nzuri na mingi yenye nia mbaya kwa Wahanga.
Pongezi za pekee ziwaendee Roma Mkatoliki na wenzake kwa kutanguliza mbele afya ya akili zao, familia zao na hata kazi zao kuliko kufuata upepo wa watu.
Tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki lilitaka kufanywa kama lile la Kuvamiwa kwa Studio za Clouds Media Group na kusahau kuwa haya ni matukio mawili tofauti kabisa. Tukio la Roma na wenzake mpaka sasa haliwezi kuhusishwa na siasa moja kwa moja au na mtu fulani moja kwa moja tofauti na lile la Clouds ambalo lilikuwa na mazingira kuhusisha mtu fulani moja kwa moja.
Pamoja na hayo, mazingira ya namna tukio la Clouds Media Group lilivyoshughulikiwa yalikuwa na kila aina mihemuko, chuko binafsi na kutaka kulipiza visasi. Matokeo ya namna tukio hilo lilivyoshughulikiwa nadhani kila mtu anayajua. Wengi wanadhani madhara yamekuwa kwa Waziri mwenye dhamana ya Habari wakati huo, Nape Nnauye, lakini kumbe madhara yamewakumba hata Clouds Media Group wenyewe kwani kulikuwa na uwezekano wa Clouds media Group kupata matokeo ambayo ni chanya zaidi kama mazingira ya kulishughulikia tatizo yangekuwa siyo ya mihemuko, chuki binafsi na visasi. Ikumbukwe kuwa mbali na Clouds Media Group kama taasisi, wapo watu walioathirika wao kama wao ambao kama busara zingetumika zaidi pengine wangejisikia kuthaminiwa kulikoni ambavyo mazingira ya kushughulikia suala lao hayakuwa rafiki.
Nimtakie kila heri Waziri Mkwakyembe katika kusimamia vyema Wizara hii kwani ameonesha mwanzo mzuri wa kuwaunganisha wanahabari, Wasanii na wadau wengine ikiwemo Serikali.