Nimepata ujauzito licha ya kunywa vidonge vya kuzuia mimba

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
"Haikuwahi kutokea kwangu kuwa nilitumia dawa za kuzuia mimba 'morning-after pill' na zikashindwa kufanya kazi.''
'Rachel' ambalo si jina lake halisi, alipata ujauzito baada kubakwa akiwa nchini Canada.

Pamoja na kwamba alikunywa dawa ya kuzuia mimba usiku huohuo alikwenda kupata huduma ya afya baada ya kufanyiwa unyama.

"Baada ya miezi miwili nilishangaa kuwa nina ujauzito - nilichanganyikiwa zaidi kutokana na kile kilichonipata , nilishtuka sana -ujauzito huo ulikuja kama kitu cha kushangaza sana, " anakumbuka kuwa hakutarajia hata kidogo kuwa kitu kama hicho kingeweza kutokea kwake.

Rachel ambaye sasa ana umri wa miaka 34, anasema kuwa hakuambiwa na madaktari kuwa anaweza kupata ujauzito baada ya kumeza vidonge hivyo vya kuzuia mimba:

"Katika maongezi yangu na daktari sikumbuki kama daktari aligusia kuwa kuna uwezekano wa mimi kupata ujauzito, kwamba dawa inaweza isifanye kazi vizuri."

Inakadiriwa kuwa asilimia 0.6 mpaka asilimia 2.6 ya wanawake wanaokunywa vidonge vya kuzuia mimba mara baada ya kufanya mapenzi ambayo salama wanaweza kupata ujauzito.

Mambo gani watu wanayajua - na mambo gani ambayo hawayajui - kuhusu vidonge vya kuzuia mimba.

Ni namna gani vidonge vya kuzuia mimba vinafanya kazi?

• Kuchelewa kupevuka kwa yai kutokana homoni za mtu
• Kama yai limepevuka kabla mtu hajanywa dawa na likiwa bado linapevuka wakati unapofanya ngono ambayo si salama basi dawa haiwezi kuzuia mtu kupata kupata mimba
• Hii ina maanisha kwamba vidonge vya kuzuia mimba zinaweza zisifanye kazi vizuri kutokana na mzunguko wa hedhi wa mtu.
• Kupevuka kwa yai huwa inatokea wiki mbili kabla ya siku za hedhi.
• Kuna aina mbili za vidonge vya kuzuia ujauzito ,kuna vidonge ambavyo mtu anakunywa ndani ya saa 72(siku tatu) tangu afanye ngono ambayo si salama na nyingine ni anapaswa kunywa ndani ya saa 120(siku tano)
Baadhi ya dawa zinaweza kuvuruga ufanisi wa dawa hizo pia, amesema Dkt. Caroline Cooper ambaye ni mtaalamu wa afya ya uzazi.
"Dawa hizi zinaweza kuharibu utaratibu wa jinsi figo linavyofanya kazi," alisema.
Dawa ambazo zinaharibu ufanisi wa vidonge vya kuzuia mimba ni pamoja na dawa za kupunguza maumivu ya virusi vya ukimwi.
Sababu nyingine ya vidonge vya ujauzito kushindwa kufanya kazi ni uzito wa mwanamke, Dkt. Cooper anaeleza.
Wanawake wenye uzito mkubwa wako kwenye hatari ya kupata ujauzito baada ya kunywa dawa hizo ingawa si lazima kuwa uzito ndio kigezo.

' Ni kitu ambacho akitabiriki'

Lakini wanawake wangapi wanajua kuhusu suala hili? Kwamba dawa ya kuzuia mimba inaweza kushindwa kufanya kazi kutokana na kuchelewa kupevuka kwa yai.

Hata maelezo ambayo yapo kwenye kasha la dawa za kuzuia mimba hayasemi chochote kuhusu ukweli wa ufanisi wa dawa hizo kutegemea mzunguko wa hedhi.

Lakini kwa nini wanawake wote hawapati taarifa muhimu kama hizi wanapopewa dawa hizo za kuzuia mimba?
"Nilikuwa sitarajii kabisa kuwa dawa hizo kushindwa kufanya kazi,"

Harriet mwenye miaka 26, anaeleza namna ambavyo alikunywa dawa za kuzuia ujauzito wakati ambapo kondomu yake ilipopasuka.

Anasema kwamba alikuwa anafuata utaratibu ulio sahihi.

Harriet aliongeza kusema kuwa aliambiwa kuwa vidonge mara nyingine huwa havifanyi kazi lakini hatari ambayo walimwambia ni kuhusu kuchelewa kunywa dawa hizo.

Yaani ni lazima dawa hizo zinywewe ndani ya saa 24, lakini cha kushangaza wiki moja baadae alijikuta kuwa mjauzito.
Kwa upande wake Rachel, kutojua kuwa vidonge vya kuzuia mimba vinaweza kushindwa kufanya kazi kulimpa wakati mgumu sana.

"Lakini nisingeweza kubadili kile kilichotokea - mtoto wangu sasa ana miaka 15 na ningekuwa na maumivu sana kama nisingempata," alisema. "Lakini wakati huo niliumia sana…nilihisi kuwa ujauzito uliharibu maisha yangu bila kutarajia."
Nilimuuliza Dkt.Cooper kama wanawake huwa wanaambiwa na wauza dawa kuhusu mzunguko wa hedhi unaweza kusababisha utofauti katika ufanyaji kazi wa dawa.

"Nadhani wanawake wanapaswa kufahamu," alisema. Aliongeza kusema kuwa wauza dawa huwa wana uelewa kuhusu hizo lakini mara nyingine hawatoi maelezo hayo.

Wanawake wawili kati ya 100 ambao wanatumia dawa hizo huwa wanapata ujauzito kwa makadirio ya asilimia 0.6-2.6%.

Mimba
 
Back
Top Bottom