Nimepata msichana mwenye mwanaume mwingine

Sasa ndo wewe unamegewa demu wako mlioanza nae kutambo unahisi ungejisikia je ? Angekuwa anakupenda wewe tayari kasha muacha utakuwa wewe unamsaidia majukumu ndo maana kajishikisha acha kula vya watu tafuta wako
 
Unaonjeshwa asali unaamua kuchonga mzinga kabisa; jomba vp?!

Anyway, kama vp; piga fitina tu, hamna jinsi!!

Nikufundishe?!
 
Hahahaha hebu nielekezee kidogo ilikuwaje
Yangu iko hivi;
Yani Nilikua na Manzi zamani kidgo ka 6 Months zimepita tukazinguana then, tukaachana. Sasa nikaondoka mjini nikaja huku nikamkuta huyu manzi yupo kwenye ugomvi mkubwa sana na mshkaji ake so nika take chance ila akanipa tahadhari kuwa anamshikaji although hawapo kwenye goodterms. Hii ndio iliyonipa ujasiri zaidi wa kuwa nae, Lakini kadri siku zinavosonga naona jamaa bado yuko nae in tourch. Hapa Manzi wangu wa zamani nae bado huwa ananipigia simu mara chache thow naona niko in love na huyu mpya wa jamaaa.
 
Kuna uwezekano ni mke wa mtu!anaogopa kukueleza ukweli kua kaolewa,hebu mwambie unahitaji kumtolea posa na kumvisha pete hatimae awe mke,tena mwambie ni jambo la haraka hilo,usikie atakuambiaje.
 
ujue wewe ndio kidumu na pia ndio fimbo ya karibu....Chukua hatua!
 
Wakuu wanajamvi habari zenu?

Bila kupoteza muda na ukizingatia mmetoka katika msimu wa Pasaka basi nisiwachoshe, naomba niende moja kwa moja katika mada,

Mimi ni kijana(Me) amabae sijao bado. Sasa kutokana na kuwa kwe mahusiano kadhaa yasio kuwa na mafanikio sana kipindi cha nyuma nikiwa katika jiji la Dar es Salaam baadae nilihamishwa kikazi kwenda mkoani ambako ninaishi kwa sasa.

Nimekuja mkoani huku takribani miezi 5 kwa sasa, basi nilivyofika hapa kazini nikapata msichana ambae kwakweli nikaanza kumpenda (sijui kwa ajili ya ukaribu wetu?) Sasa wakati tunaanza nae mahusiano akaniambia anamsela wake ambae kamuacha mkoa mwingine.

Mimi nikamwambia isiwe kesi wacha tufanye yetu na kwa bahati mbaya au nzuri nikaendelea kumega tunda huku bado msichana akiwa anaongea na jamaa kwenye simu sometimes na mimi nikiwepo (sababu nafahamu).

Sasa issue hapa inakuja wapi? Sasa hivi nahisi nanza kumpenda na sioni dalili ya huyu msichana kumuacha mpenzi wake wa zamani kwa sababu hata akipata likizo kidgo huenda kumpelekea mshkaji. Ila ukimuuliza anadai eti ananipenda mimi. Wazee naombeni ushauri wenu maana hapa naona sasa nazidiwa nguvu mtoto wa kiumeni.

Nb: Tunaishi nyumba moja kwa miezi 2 sasa
Wewe ni chokooo na unaudhaifuu mkubwa Sana,na udhaifu wako huo utakutafuna mpka unafukiwa kaburin pumbafu wewe
 
Yangu iko hivi;
Yani Nilikua na Manzi zamani kidgo ka 6 Months zimepita tukazinguana then, tukaachana. Sasa nikaondoka mjini nikaja huku nikamkuta huyu manzi yupo kwenye ugomvi mkubwa sana na mshkaji ake so nika take chance ila akanipa tahadhari kuwa anamshikaji although hawapo kwenye goodterms. Hii ndio iliyonipa ujasiri zaidi wa kuwa nae, Lakini kadri siku zinavosonga naona jamaa bado yuko nae in tourch. Hapa Manzi wangu wa zamani nae bado huwa ananipigia simu mara chache thow naona niko in love na huyu mpya wa jamaaa.
Duh Dillema hio, fanya maamuzi magumu
 
Mkuu kifupi tu huwezi kupata mwanamke ambaye hana boyfriend. Ni vizuri huyo kawa mkweli kabisa. Na ninafikiri kama kweli umempenda basi tangaza nia huyo jamaa atapigwa chini mpaka utamhurumia. Wanawake ambao wako kwenye umri wa kuolewa hapa naongelea 22+ huwa lazima awe kwenye mahusiano ya watu zaidi ya mmoja ila mnakuwa mnapangwa kiprofessional hamfahamiani. Kila mtu anaambiwa nina mtu wangu ambaye tunapendana. Kama ujuavyo tena mwanaume akishatamani akili zote huhamia kwenye pumbu. Lazima useme wewe mm nitaheshimu mahusiano yako. So cha kufanya mwambie nataka kukuoa and sitaki nisikie habari za una mwanaume mwingine zaidi yangu. Sasa uwe mchumba wangu
 
wewe kula kisela mwenzako anajitambua anacho fanya wewe ndo unaleta mapenzi yako ya zamani ashakuambia tokea mwanzo kuwa anamtu wake sasa wewe unataka nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom