Nimepata mshutko baada ya kuambiwa ni nywele za maiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimepata mshutko baada ya kuambiwa ni nywele za maiti

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by VISIONEER, May 28, 2011.

 1. VISIONEER

  VISIONEER Senior Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna nywele siku hizi wanawake weusi wanazivaa kichwani wanaziita human hair, mwanamke mweusi akizivaa hizo nywele anakua kama mhindi si mhindi, mzungu si mzungu.

  Mwanzo mimi nilifikiri ni utaalam wa wenzetu wazungu labda wanatenngeneza makatani halafu yanakuwa hivyo, lakini baada ya kuambiwa ni nywele za maiti kwakweli nilishindwa kuelewa inakuwaje wanawake weusi wanayaweka manywele hayo kichwani.
  Na zinauzwa bei mbaya kweli mpaka laki nne lakini watu wanazinunua

  je hatuoni ni kama kujikataa, kumkosoa muumba kwamba hakukuumba vizuri?
   

  Attached Files:

 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Ishu sio kuwa nyele za maiti ishu ni kutokuvaa na kupoteza uafrika wao,inaniboa!Ulisoma ile thread ya mawigi?
   
 3. 4

  4 PRINCE Senior Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani hawajatambua kuwa huwa wanapendeza hata bila mawigi.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  mmeshaanza somo la sayansi kimu eeh? safi sana! waambie aisee,watakufa!

  </p>
  <p>&nbsp;</p>
   
 5. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We dogo vp tena?
   
 6. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  View attachment 31014

  ni kweli kabisa mengi ya hayo majitu yameibwa makaburini
  nyie lingeni tu mitaa lakini mnatembea na wafu vichwani
   
 7. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  tena kwa kadiri inavyokuwa nzuri bora na yenye mfuto na mabei kubwa ndio kutokana na maiti kunaongezeka
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama ni maiti sababu nimeshawahi ona documentari CNN huko Russia na Aljaazera huko India.
  Ile ya CNN inaonesha jinsi hii biashara inavyofanywa huko East europe hasa Russia, kuna salon za kike rasmi kabisa wananunua hizo nywele. Msichana anakuwa anafanya hiyo biashara anafuga nywele zikiwa kubwa anaenda kwenye salon wanamnyoa anakula pesa yake anaondoka, so mwenye salon anapata wasichana kwa akina mama wanaenda pale yeye anawanyoa anakusanya marobota na marobota ya nywele destination ni Italy ndo kwenye viwanda wanakochambua na kuziweka dawa na kubind style tofauti tofauti. India nako the same, kuna waitaliano wako huko wanakusanya mpaka za watoto wa shule kwa kuwa Indians wengi ni maskini km huko wanauza kwa bei ndogo sana ili kuweza kulipia ada ya shule na mahitaji muhimu. Niliona msichana mdogo huko india mama yake anamlazimisha akanyoe ili wapate pesa ya ada ya shule maskini yule mtoto alizitunza vizuri sana nywele zake lkn umaskini ukamfanya awe na kipara. So mkuu hii ni biashara ya watu wanaifanya na si nywele za maiti km unavyofikiria
   
 9. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwani huyo maiti ni nani?, mtu ukitokwa na uhai ndio hufai tena? ni viungo vingapi vya maiti vinatumika kwa binadamu walio hai? nini kinamfanya maiti kuwa kitu cha ajabu? je wewe ukifa ukimbiwe kwa sababu umekuwa maiti?
  Acheni hizo bana, wanawake watasuka human hair na kuweka weaves na wigs za kutosha, maisha yenyewe haya mafupi kwa nini mtu usipendeze na kufurahi rohoni mwako kisa eti mtu hapendi kuona nywele za maiti, inahusu
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  duh! Ulivyotetea! Nasikia hadi ubongo wa maiti huwa unatumika kutengenezea dawa za binadamu. Wadau watasema hapa.
   
 11. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  cha kushangaza dawa hazisemwi, zimeonwa nywele ambazo zimekuwa treated na zinasukwa nje ya mwili, hizo dawa zinazoingia ndani ya mwili aah ni sawa, hebu watu wawaache watu wengine na uhuru wao bana
   
 12. w

  wahu New Member

  #12
  May 28, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haa! teh teh teh;
   
 13. VISIONEER

  VISIONEER Senior Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesema kweli mkuu, eti mtu anajiona mrembo kwa kuvaa nywele za mtu mwingine? Kwani za kwako za asili zina tatizo gani? Kwanini uvae nywele za mhindi kichwani?   
 14. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Mmeamua kurudisha thread kiaina, mmekutana na mabomu, mnalo. Ile ya kwanza mlifanikiwa kuwashambulia wadada leo naona mmegonga mwamba japo mmekuja na hoja za nguvu kuliko mwanzo.
   
 15. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unavaa nguo za wadhungu usiivae magome ya miti au ngozi za wanyama?

   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  May 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Yaani dawa zinatengenezwa kutokana na ubongo wa binadamu....!

  Ndo aina gani hiyo ya dawa, iliyotokana na Brain I mean ubongo wa Binadamu, au hata wa panya?


  Aspro!?
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Wanawake wavaao mawigi, na wale wanaojikoroga huwa hawajiamini uzuri wao wa asili.
   
 18. L

  Leornado JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  hii documentary pia na mie niliiona. Kuhusu maitinkunyolewa na nywele kuuzwa sijawahi kusikia. Ila inawezekana maana dunia utapeli kila kona.:biggrin1:
   
 19. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  mkuu hiyo hapa sio kwamba ni siri, hicho kipindi ulichoona wewe alikuwa wanaelezea kwa upande huo na hawakugusia za binadamu,
  dada zetu weusi wanakana kwamba hawazai nywele za wafu, lakini wazungu wanakiri na wanapokwenda kununu wanauliza kabisa kipi ni kipi,
  sema maduka ya bongo sio wa kweli, ila huu ni uchafa.
  Ubongo kutumika kama dawa ni issue tofauti, dawa ni uhai lakini pia ni dawa gani hizo zinazotumia ubongo, dawa nyingi sinatumia mimea hachani kutanganya watu, sanyasi ya tiba hiko mbali sana kwa sasa, kila kitu wanatengeneza maabara kwa maana nyingine hata mimea wanayotumi wanaiotesha kichemicaly kwenye mahabara,
  kama kuna mtu anatumia hayo manywele basi ujua unatembea na maiti kichwa wala hakuna kuzoga hapa.  Product rating
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
  These stick tip extensions are some of the finest available! They are a perfect choice for anyone who loves to add volume and length by applying extensions through micro and shrink rings.

  And our stick tip extensions are only 100% human remy hair! Which means you can wash, curl, straighten and even dye them to suit your own look!

  This single pack contains 50 strands. For a full head look we do recommend purchasing a minimum of 3 to 4 packs (that's 150 to 200 strands)

  Item Specifications:
  Number of pieces: 50
  Length of hair extensions: 20" (50cm)
  Weight of hair: 0.8 grams per strand: 40 grams total
  Type of hair: 100% Remy Human Hair
   
 20. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  angalia hiyo video huyo dada ni mkweli atasema

  [video]http://youtu.be/ZGzwVfVyJF8[/video]
   
Loading...