Nimepata mbinu mpya ya kupunguza gharama ya tozo za miamala

chrisbleez

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
735
1,208
Bila shaka Mungu ni mwema na ninawasalimu kwa jina la jamuhuri.

Nimeona nishee nanyi wenzangu katika kuwahabarisha kuhusu huduma tajwa hapo juu

Katika kusheherekea na kufurahia ushindi wa simba hapo jana niliona nipombeke kidogondipo nikajikuta mzigo kama unakata hivi mfukoni, ikasogea kwa wakala aliyekaribu yangu akanifundisha kaujanja flani hivi ambapo aliniambia nilipe kwa TigoPesa *150*01#(kwa wakati huo nilikuwa na pesa tigopesa) then unaenda namba 5 lipa kwa Tigopesa basi bwana nikajaribu kulipa kama laki moja hivi.

Unajua nini nilikiona, yaani makato ni shilingi mia nane(800). Sikuamini macho yangu hali iliyonifanya nirudi tena kutoa kiasi kama kile kile nilichokitoa pale mwanzo baadae wakati nilipotaka kuondoka na hali ikawa vile vile

Hivyo nikajikuta nimetoa sh.laki mbili(200,000)kwa makato ya Tsh.1600 wakati makato ya kawaida yangekuwa ni Tsh.16,480

Hii tunasema ahsante yule wakala kwa kunisanua nitakuwa ninakwenda kutoa pesa zangu kwake kamseleleko.
 
Du umeharibu sana wewe. Yaani kesho mambo yatakuwa tofauti kabisa maana Tigo watarekebisa
. Una haraka hujafafanua vizuri labda kama mimi ndio sikuelewa.
Una hela kwenye tigo. Ukatuma ama ukatoa kutoka Tigo ndio ukakatwa hiyo shs 800?
Fafanua taratibu Comrade maana wengine Mabichwa yetu haya ni mazito kuelewa jambo mara moja!
 
Fafanueni basi , japo naunga mkono tozo ila sitaki kukatwa 😄😄🏃🏃
Ni hivi, kutoa 100,000/- kwenye Tigopesa gharama yake ni 6,180tzs; wakati huo huo kulipia kitu cha 100,000/- gharama yake ni 1,000 tu.

Sasa ukitumiwa pesa, kama una kitu cha kununua, usitoe hela, nenda tumia kwenye lipa kwa simu. Tatizo tu, sio sehemu nyingi zinapokea, ila kama ni vituo vya mafuta, restaurants na supermarkets wanapokea.

Tozo ni kuwenye kutuma na kutoa tu, huku kwingine bado.

Dawa nyingine ni kutumia benki tu. Una 1mil ya kumpa mtu, weka CRDB/NMB yako, kumtumia bure, akienda kutoa mara 3 gharama jumla 2400.
 
Mkuu fafanua zaidi hiyo aya ya mwisho.
 
Waweke vibanda vya kuweka na kutoa hadi vijijini
 
Anasema ukiwa na salio MPESA au tigo Pesa na unataka kununua kitu fulani tafuta Duka lenye option ya kulipa Kwa MPESA au Tigo Pesa . Makato Kwa kulipa Kwa MPESA au Tigo Pesa ni madogo.
Au pia kama una mtu mnayejuana naye anayefanya biashara na ambaye anatumia huduma hiyo ya lipa kwa simu basi unaweza ukamlipa kwenye lipa namba yake na yeye akakupa hela cash,atapunguza tu kidogo ile ya transaction fee
 
Anasema ukiwa na salio MPESA au tigo Pesa na unataka kununua kitu fulani tafuta Duka lenye option ya kulipa Kwa MPESA au Tigo Pesa . Makato Kwa kulipa Kwa MPESA au Tigo Pesa ni madogo.
Ni kweli na kwenye laki moja tigo wanakata sh.mia nane tu raha iliyojeeeeeee
 
Kwahio wewe unafanya kama umelipia kitu halafu yeye anakupa cash?
Wazungu wangekuwa wanakwepa hivi kulipa Kodi ( kukatwa Kodi ) sidhani kama nchi zao leo hii zingekuwa na Maendeleo makubwa mpaka Sisi hawa hawa Watanzania ( Waafrika ) wakwepa Kodi na Tozo tunahangaika kutafuta Viza za kwenda huko Kwao na hata Misaada yao ya Kifedha ( Kipesa ) huwa wanatupa kila Uchao.

Tuacheni janja janja hebu tulipeni Kodi.
 
Back
Top Bottom