Nimepata matatizo lakini hakuna Ndugu yangu aliyekuja wala kupiga Simu ya pole

Mondela

JF-Expert Member
Aug 20, 2021
2,570
3,763
Habari zenu? Kunakipindi nilileta uzi huu, Ndugu zangu nashindwa kuwaelewa

Baada ya kuvuta jiko niliishi na mke wangu, mwezi wa 11/2021 tulibahatika kupata mtoto na mke wangu, sikuwa na hiyana niliona japo ndugu zangu walinikosea kiasi fulani acha niwataarifu japo mke wangu alipata PPH (Postpartum Haemorrhage) nusura afe niliwataarifu pia kuhusu hayo matatizo lakini hawakujali na wala mke wangu hakupigiwa simu wala kuulizwa chochote.

Baadae nilisema isiwe kesi acha niendelee kutulia kimya nikaamua kutokuwatafuta tena, pia japo nilifiwa na baba niliandika kwenye uzi hiyo link juu, baada ya kutoka msibani hakukuwa na mtu aliyekuja kunipa pole hasa mama yangu mdogo wala wajomba zangu hakuna na wala eti waulizie kuhusu mtoto wangu anaendeleaje hakuna.

Baada ya kuona hivyo nilitulia tulii, juzi kati mamdogo wangu ananipigia na kunilazimisha nimpeleke mke wangu na mtoto wangu kwake, pia naambiwa mtoto wa mjomba anafunga ndoa mwaka huu hivyo nijiandae kirohoni nikajisemea hivi hawa wananichukuliaje?

Nimepata msiba hawajaja na baadhi yao hajanipigia simu kunipa pole, haya mke wangu alijifungua na akapata matatizo na niliwataarifu hakuna aliye toa pole na wala kujali.

Nawasilisha wakuu, hiyo ni sahihi?

Pia kuna mambo mengi tu sema siwezi andika Wakuu
 
Japo si vizuri kufanya hukumu ila nimejiuliza kweli familia nzima kama sio ukoo wakutenge kwa kiwango hicho?

Mkuu yawezekana kuna namna wewe ni tatizo aidha kujiona umewin sana maisha au ukawa na dharau kwa huo ukoo.

Jitafakari kuna tatizo mahali kwako wewe japo unajitetea.
 
Japo si vizuri kufanya hukumu ila nimejiuliza kweli familia nzima kama sio ukoo wakutenge kwa kiwango hicho? Mkuu yawezekana kuna namna wewe ni tatizo aidha kujiona umewin sana maisha au ukawa na dharau kwa huo ukoo. Jitafakari kuna tatizo mahali kwako wewe japo unajitetea.
Mkuu sio kwamba ni ukoo mzima wamenitenga ni baadhi ya ndugu zangu tu, kuna dada yangu mtoto wa shangazi naheshimiana nae na wadogo zangu ambao walifiwa na baba yao nawasaidia sana.

Pia naweza kukuambia kuwa hao baba zangu wameanza kunichukia tangu nipo mdogo yaani nilikuwa hata nikiugua hai kabisa hawajali kwa lolote kwani kwa kipindi hicho niliishi na babu na bibi kwani mama aliniacha nikiwa na miaka 3 na baba alipata magonjwa ya akili mkuu.

Sikatai kuwa kila mtu anamatatizo na hakuna mkamilifu ila mtoto akikosea muonye maana wao ni wazazi na si kumchukia, sina baba wala mama kwasasa na wao niliwachukulia kama baba na mama zangu, mkuu we hujui tu ila kama nikujiona nime win sisingeweza kuwa naenda kuwasalimia kila likizo na kama baba yangu mdogo alikuwa akiomba support ya kumtumia babu pesa natuma.

Inshort walikiwa hawajali kwa lolote tangu niko darasa la kwanza mkuu.
 
Maisha yamebadilika sana mkuu, ndugu sikuhizi siyo wale wa damu tu, ndugu ni yule aliye tayari kuwa na wewe wakati wa shida na raha bila kujali.

Ukipata watu wa aina hiyo hatakama siyo ndugu yako wa damu ishi nao vizuri.


Mindset uliyonayo ya kutaka ndugu wa damu waonyeshe ushirikiano na kukujali kwa kila jambo kwasababu tu ni ndugu /wana ukoo, hiyo mindset ondoa kabisa na kuwa flexible kuishi nao jinsi walivyo.

Siyo ndugu tu, hata marafiki pia, kuwa flexible kuishi nao jinsi walivyo, yaani usilazimishe kuwa na umuhimu katika maisha ya wengine.

Shida zipo na huwezi kosa mtu hata mmoja wa kukupa support.

Hao wachache walio tayari kuwa na wewe komaa nao, ambao wako bize na maisha yao waache waendelee na maisha yao.

Usipokuwa na umuhimu katika maisha ya mtu usitegemee ataonyesha kujali na kukupa muda wake, hivyo achana na habari ya kuamini ndugu wa damu LAZIMA wawe upande wako kila wakati.


Ulimwengu umebadilika sana, mind your own business na ishi kutafuta amani ya moyo wako na siyo kutafuta ndugu.


Huwezi pendwa na wote, hata Yesu mwana wa Mungu hakupendwa na wote, wewe ni nani kila mtu akupende na kujali matatizo yako??


ISHI MAISHA YAKO, ALIYE UPANDE WAKO NENDA NAYE, ASIYE UPANDE WAKO ACHANA NAYE.

Kikubwa USIWACHUKIE. Kubali tu uhalisia wao na uendelee na maisha yako.

Hiyo mialiko kama imetoka kwa watu ambao hawakuonyesha kukujali wakati wa matatizo na wewe USIENDE, endelea na maisha yako.

Kama ipo pesa ya ZIADA wachangie kidogo waambie ratiba zimebana ila kama pesa uliyonayo una bajeti nayo muhimu USITOE.

Ukiishi kutaka kumfurahisha kila mtu huwezi ishi kwa amani kamwe.
 
Mkuu sio kwamba ni ukoo mzima wamenitenga ni baadhi ya ndugu zangu tu, kuna dada yangu mtoto wa shangazi naheshimiana nae na wadogo zangu ambao walifiwa na baba yao nawasaidia sana. Pia naweza kukuambia kuwa hao baba zangu wameanza kunichukia tangu nipo mdogo yaani nilikuwa hata nikiugua hai kabisa hawajali kwa lolote kwani kwa kipindi hicho niliishi na babu na bibi kwani mama aliniacha nikiwa na miaka 3 na baba alipata magonjwa ya akili mkuu.

Sikatai kuwa kila mtu anamatatizo na hakuna mkamilifu ila mtoto akikosea muonye maana wao ni wazazi na si kumchukia, sina baba wala mama kwasasa na wao niliwachukulia kama baba na mama zangu, mkuu we hujui tu ila kama nikujiona nime win sisingeweza kuwa naenda kuwasalimia kila likizo na kama baba yangu mdogo alikuwa akiomba support ya kumtumia babu pesa natuma. Inshort walikiwa hawajali kwa lolote tangu niko darasa la kwanza mkuu.
Ninge kuwa wewe nisinge hangaika nao kwa lolote
 
Mpende na shirikiana na anae kupenda, wengine waweke kando.

Hao wanaokutatafuta wakati wao wanakuhitaji, na wakati una shida hawakutatufuti , achana nao.

Watakupa stress tuu, maana wao hawajali
 
Kweli mkuu, sasa sijui wanafanya hivyo kwakuwa wanapesa? Maana hao ninao waongelea wanapesa hivyo wanajiona matawi japo mimi nilikuwa napenda kuwajulia hali. Chakushangaza sasa ninao elewana nao mimi ni wale wenye maisha ya kawaida kama mimi.
Kama wana pesa basi wapotezee tu Mkuu.. Ukiwaendekeza hawakawii kusema unajipendekeza kwao..

Kwani maisha yako bila wao unaona hayawezekani?
 
Back
Top Bottom