Nimepata kazi serikalini, je niondoke vipi huku private?

Kwani huwa hamsaini mkataba wa kazi huko private.... umeosoma mkataba wako ?
Au mnapewa kazi kishikaji....
Kama upo mkataba usome utakueeleza jinsi kuacha kazi kwa ridhaa yako,
Sijui huko, lakini kutakuwa kuna kifungu kinahusina na kutoa notisi ya kuacha kazi
Inaweza kuwa notisi ya mwezi au miezi unaendelea nao, ukimaliza ndio unaenda kuanza kazi nyingine
Na utamwambia mwajiri wako mpya nina notisi ya mwezi kwenye kazi yangu kabla ya kuaanza kazi mpya
Au labda naota njozi za mchana... huko mambo yanaenda kimzobe mzobe....
 
Je,nisipoandika nikaaga kawaida au nikapiga sim tu nimeacha kazi vp
Inawezekana tatizo si namna ya kuacha kazi bali ni maneno gani utatumia. Huo si ustaarabu, ustaarabu ni kuandika barua ukieleza umefanya kazi kwa muda mrefu na unashukuru kwa ushirikiano na uzoefu mkubwa ulioupata hapo. Kwa heshima na taadhima unaomba kutoka katika kazi hiyo au katika kampuni hiyo na kuhamia kwingine ili kwenda kupata uzoefu zaidi utaokuwezesha kujifunza zaidi
 
Madam tajwa hapo juu yahusika sana.

Nimekua sekta binafsi kwa miaka kadhaa sasa, hadi kufikia kupewa madaraka makubwa tu kazini. Natakiwa kwenda kuripoti na hapa niko najiuliza namna gani nzuri ya kuaga uongozi na wafanyakazi wenzangu.

Naombeni ushauri wenu wakuu.
Huijui serekali ww!!?
utahamishwa kushoto na kulia mpaka ukome....
 
Back
Top Bottom