Nimepata kazi naombeni kanuni za kuishi na boss mwanamke,madhaifu yao pia,wanapenda nini pia

kikale

JF-Expert Member
Oct 14, 2012
410
500
Looh kumbe hujui.....Huyo ni kumkaza maramoja usicheleweshe...
 

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,727
2,000
Kazi haina boss mwanamke au mwanaume na hilo ndiyo tatizo la sisi watanzania.

Umepewa JD yako unatakiwa kuifanyia kazi tu hiyo silaha yako.

Sasa ukiingiza ujinga wako eti boss mwanamke sijui boss kabla gani,sijui boss mzungu,sijui boss tajiri,sijui boss mlevi sana,sijui boss mlokole unaomba ushauri ufanyaje naye kazi hiyo itakula kwako na utafukuzwa dakika moja hapo!!

Fanya kazi kwa kufuata Job Description yako na sheria za kazi na kanuni zenu hapo plus taratibu na kuhakikisha unatimiza malengo ya kazi yako ndiyo vitu vya msingi.
 

msausoghonoi

Member
Mar 13, 2017
17
45
Nafikiri swali lake linaweza kuwa na Mantiki. You cant out-shine your boss thats the principle. Mheshimu, fanya kazi yako kama JD inavyosema na zaidi ya JD acha mambo za kutumia internet za kazini kushinda facebook. Na ni kweli kila boss anatofautiana na boss mwingine hilo ulijue. Sio wote wako sawa. Kuna wengine huwa hawapendi kupewa challenge (siwapendi hawa) itabidi tu uishi kama kondoo mwema timiza majukumu yako chukua salary tulia. Kuna wengine wakikuona huna jipya unawaboa- changamka toa mawazo mapya na ujitahidi kumshirikisha kabla hujafanya- Kuna wengine "Uanamke" unawasumbua hata kama ni maboss ukiwabishia kitu wanajua huyu ananiona mie "Mwanamke ndo mana" reaction zao ni very bitter. Kumbuka tu kwamba Mwanamke hata kama ni boss saikolojia yao ya asili iko pale pale "mwapreciate (kiofisi) anapofanya kitu kizuri hapo utaishi vizuri haha. Kwa hiyo kama wewe sio mwepesi kumsoma mtu yukoje ishi kwa kufuata JD yako na mengine kama nilivyoeleza.
 

Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
2,173
2,000
Achana na mifumo DUME KWA BOSS, UTAISHI. ILA IKITOKEA AMEKUTONGOZA UKAMPA DAA! AAA! SEMINA ZOTE ZAKO, NAFASI NZURINZURI TUUU.KUPANDISHWA CHEO HRK.

NA WANAJUA KUPENDA HATARE!
 

kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Nina boss wa kike jambo dogo kwake linaumuka kama limewekwa hamila. Ni mkali sana akikasirika usimjibu,usioneshe mtazamo unaokinzana na wake. Nh mara chache sana kuchukua ushauri/maoni kutoka chini. Neno lake akiwa na hasira "MNANIONA MWANAMKE? SASA NITAWAONYESHA UANAUKE WANGU". Kifupi ishi na boss wako wa kike kwa akili ili kulinda kitumbua chako,kuwa mwepesi kuomba msamaha usidharau kosa kwake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom