nimepata kazi mkoani ...najishauri!!

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
habarini JF

nipo dms nafanya kazi kampuni fulani ya simu.nimepata kibarua kingine kwenye kampuni nyingine ya simu kwa tofauti ya mshahara ya laki 2...i mean ya mkoani imezidi kwa laki 2 mshahara wa apa dar..........wananipa na gari ya kazi!!hardbody...lakini bado naona ugumu kuenda huko meatu...nishaurini niende au nibaki?
 
Unamaanisha Dsm ni JIMBO? Kufanya kazi Dsm ulishauriwa na nani? Kwanini asikushauri tena kwenda Meatu?
 
Angalia maslahi zaidi,unaweza ukaenda huko na hilo gari lao halafu hakuna hata barabara,social services zipo mbali,but angalia kwanza mazingira ya huko mkoani kwanza halafu ukiona mazuri au mabaya ndo ufanye uamuzi
 
Nenda tuu hakuna mbaya
kwani una familia inayokusumbua na inayokufanya wewe kwenda huko
Nenda ni sehemu nzuri sana na nishafika sana kule
 
wewe huko Meatu hakufai bana ..kaa mujini fanya kazi kwa bidii tafuta namna ya kuingiza kipato nje ya mshahara wako ...sitaki hata kusikia yaani tofauti ya laki mbili 2 ,na hiyo gari sio yako binafsi ni ya ofisi..lol we panda daladala .bana ..
 
Angalia maslahi zaidi,unaweza ukaenda huko na hilo gari lao halafu hakuna hata barabara,social services zipo mbali,but angalia kwanza mazingira ya huko mkoani kwanza halafu ukiona mazuri au mabaya ndo ufanye uamuzi

Mkuu kuhusu barabara asahau lami kwa muda maana wilaya nzima haina hata meta moja ya lami ila mipango (as u know michakato ya serikali yetu) iko mbioni kujenga barabara mle
Ila huduma nyingine ziko poa hospital ipo polisi, shule na maji yapo
Ila kwa ukame ni noma maana hali ya mkoa wa shinyanga maeneo mengi kipindi cha jua ni kukame mbaya
Na ni karibu kwenda mwanza akitaka good time atakuwa anaenda mwanza
 
tatizo nashindwa kuelewa kwa nn moyo wangu umekua mzito..........sijafanya maamuz nna siku 3 sasa..sina sababu za msingi saana zaidi ya mchumba ambaye yy analia tu mda wte akiskia naondoka,halinipi shida sana......sasa nitaufahamu vp huo mji?nitakua pia hadi maswa...nahitaji kufahamishwa na wenyej plz
 
habarini JF

nipo dms nafanya kazi kampuni fulani ya simu.nimepata kibarua kingine kwenye kampuni nyingine ya simu kwa tofauti ya mshahara ya laki 2...i mean ya mkoani imezidi kwa laki 2 mshahara wa apa dar..........wananipa na gari ya kazi!!hardbody...lakini bado naona ugumu kuenda huko meatu...nishaurini niende au nibaki?

This is not the right forum!! Unatuyeyusha!!
 
Unachoogopa ni nini haswa?if udnt hv any other source of income and yet nt invested anythng u beta leave bongo.dnt wory 2make changes.
 
Maamuzi ya kufanya kazi DAR au kuondoka yapo mikononi mwako maana kwa uhalisia kila mtu anajua siri ya kazi yake
 
habarini JF

nipo dms nafanya kazi kampuni fulani ya simu.nimepata kibarua kingine kwenye kampuni nyingine ya simu kwa tofauti ya mshahara ya laki 2...i mean ya mkoani imezidi kwa laki 2 mshahara wa apa dar..........wananipa na gari ya kazi!!hardbody...lakini bado naona ugumu kuenda huko meatu...nishaurini niende au nibaki?

mmmmh!..mimi napata kigugumizi kidogo kuhusu haya mambo_hv ikiwa kila mtu anataka kufanya kazi dar,arusha,mwanza,mby i.e sehemu nzuri tu,..tunafikiri hizo sehemu zingine nani ataziendeleza kwa kupeleka huduma nzuri pamoja na changamoto mbali mbali,..nafikiri muda umefika wa kwenda popote kwenda kufanya kazi kwa maendeleo ya watanzania...ni mtazamo tu msije nipiga mawe maake mnaokaa na kufanya kazi huko ni kama mmerogwa...njooni huku tabora tuijenge nchi___kuna ndugu zetu huku
 
wewe huko Meatu hakufai bana ..kaa mujini fanya kazi kwa bidii tafuta namna ya kuingiza kipato nje ya mshahara wako ...sitaki hata kusikia yaani tofauti ya laki mbili 2 ,na hiyo gari sio yako binafsi ni ya ofisi..lol we panda daladala .bana ..

sasa kama hakufai unataka nani akafanye kazi huko,kama sio mm na ww,...kwani huko dar mbona kuna kero kibao,..foleni,joto,maji ya chunvi na bado shida etc,...kama ni mawe nipigeni bana mmezidi usharobaro usio na maana
 
habarini JF

nipo dms nafanya kazi kampuni fulani ya simu.nimepata kibarua kingine kwenye kampuni nyingine ya simu kwa tofauti ya mshahara ya laki 2...i mean ya mkoani imezidi kwa laki 2 mshahara wa apa dar..........wananipa na gari ya kazi!!hardbody...lakini bado naona ugumu kuenda huko meatu...nishaurini niende au nibaki?
Kwani wewe ni mzaramo hadi ung'ang'anie Dar? Kwani Dsm ni nini jamani? Kuna kitu gani cha ziada unachopata ukiwa Dar es Salaam?
 
habarini JF

nipo dms nafanya kazi kampuni fulani ya simu.nimepata kibarua kingine kwenye kampuni nyingine ya simu kwa tofauti ya mshahara ya laki 2...i mean ya mkoani imezidi kwa laki 2 mshahara wa apa dar..........wananipa na gari ya kazi!!hardbody...lakini bado naona ugumu kuenda huko meatu...nishaurini niende au nibaki?
*angalia maslahi ya kimaisha,na msimamao wa kampuni hiyo na unaweza kwenda huko mkoani alafu kampuni yenyewe ikawa haina future baadae.Alafu maisha ni popote*
 
wewe huko Meatu hakufai bana ..kaa mujini fanya kazi kwa bidii tafuta namna ya kuingiza kipato nje ya mshahara wako ...sitaki hata kusikia yaani tofauti ya laki mbili 2 ,na hiyo gari sio yako binafsi ni ya ofisi..lol we panda daladala .bana ..

acha mtazamo hasi wewe laki mbili hiyo ni mshahara wa mtu! kwani Dar ni mbinguni? kwanza kwa mtu anayejua hakuna mji mbaya saizi kama Dar hata uwe na gari lako ni sawa tu na aliye huko meatu kwani mifolen kero za kila namna
 
Nenda Meatu.Acha imani kuwa kuwa Dar ndo kila kitu.Mimi nimefanya kazi dar baadae nikaenda mkoa nilifanikiwa zaidi kuliko nilipokuwa dar.Kwa hiyo wewe nenda ipo siku utanikumbuka.
 
Watu wana saka hela mkoani baada ya hapo wanakuja dar.
Nakushauri uende meatu ufanye kazi vyema na wanaweza wao wenyewe wakakurudisha mjini kwa cheo bora zaidi.
Mkoani kuna opportunities nyingi sana kuliko dar.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom