Nimepata kazi lakini mshahara ni mdogo mno

Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
Soma post namba 5 hapo juu. Ukielewa mantiki ya alichofafanua Dr hapo,huwez kulalamika tena
 
We ulijuaje km unalipwa kdg? Mbn mwajiri wako ameamua kukuvumilia wkt huu unajifunza kazi na bdo anakulipa? Hv umejiuliza maswali km hayo kwnz kabla ya kuleta upuuzi wako humu unazani kuna mwajiri anapenda kumwajiri mtu akajifunzie kwake? Je ungekuwa ww ndo mwajiri af mwajiri wako ndo ww ungekubali kumwajiri aje kufanya trio and error kwny kampuni yko?
 
Mitoto mingine sijui vp!

Ukiangalia apatacho mwenzio ukataka na ww utachemka,mm naanza kazi 2010 nikiwa fresh graduate class of 2009 nachukua net 400K nafundisha kichuo wakati sio mwalimu huku wenzangu wengi wao wapo >800K na wanafanya kazi zilizo kwenye taaluma zao ila sikupagawa.

2011 nikapata kazi iliyo kwenye taaluma yangu net ikawa ~250K nikaifuata huku nikiacha ile ya awali yenye hela nzuri zaidi lakn nikiamini hii itanijenga zaidi kitaalamu(maono ya mbali),after a year salary ilianza kupaa kwa kasi na promotion za ajabu mpaka nikashangaa.

Ningeangalia wenzangu wanapata nini ningebaki chini mpaka leo kwa kung'ang'ania ile laki 4.

Focus young fella!
 
Mdogo wewe una sh ngapi? Kama huna huo huo udogo unauonaje? Hata hivyo hulazimishwi acha usubiri mshahara mkubwa
 
Kazi yoyote wakuu isiyohitaji mawasiliano sana naomba,mshahara ni wa bosi mradi nile na kushiba....
 
Nilijua 60,000 kumbe 600,000!! Hauko sriaz mkuu, kuna watu wanalipwa 120,000 kwa mwezi
 
Hili wenge lilitaka kunipitia kipind nmemaliza chuo bhana..
Nlipata kazi kampuni ya x..mshahara nikaambiwa laki 2..aseee nikiwaza wezangu wameanza na laki 6 na kitu kwa 8500 na mwingine mgodini akaanzia 1.2 trainee kidogo niache kazi aseee..kbla hta cjaanza
Ebhana nikajikaza kisabuni tu..ilmradi tu nisiwe nakaa geto kutwa nzima..
Nikaanza mtingo mdo mdo..Ila kuja kukaa vizur asee nlikuwa natengeneza mpka 3 to 5m kila mwezi kwenye marupurupu..na gepu za kupiga zilikuwa nyingi..mpka jamaa zangu wakawa wanantamani Tena na ka laki mbili kangu..
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom