Nimepata kazi lakini mshahara ni mdogo mno

Kuna watu hamna shukrani, wenzako wanafanya kwa laki 2 wewe unalalamika laki 6? Doh
 
Shenz kabisa ww !!!mm mshahara wangu take home 380k bado nina familia nauli kila siku buku 2 chai na msosi mchana buku 4!! Bado nasurvuve kibishi kweli!!
Usilete undezi hapa
 
Mimi nakushauri upotezee usirudi pale ili wengine wanaohitaji huo mshahara wafanye hiyo kazi.
 
Dogo amekosea kuuliza swali humu, ungetafuta watu wako wa karibu uliosoma nao au waliokuzidi elimu kidogo. People in the same career as you are. Humu wamejaa walimu na watu wa biashara. Wengi wao hata ajira hawajapata that's why their anger is misdirected at you. Don't take it personally.

Kafanye kazi lakini usifanye hapo zaidi ya mwaka. Zikitoka post za serikali omba.
 
Baki nyumbani tuu, sikiliza music maisha yanaendelea mbele
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
 
Laki 6 ni mshahara mzuri Kwa kuanzia kazi na kutafuta experience. Sisi wenzio tuliajiriwaga serikalini na mshahara wa 567,000/= na take home ilikuwa 450,000. Ukiiacha hiyo kazi utaikumbuka siku za mbeleni. Graduate serikalini hulipwa TGSD ambapo Kwa sasa ni kama 710,000 ukitoa na makato inabakia 569000/= ukitoa na 15% ya loanboard inabakia 460,000/ =
Habarini humu ndani

Kama nimekosea jukwaa mtanisamehe. Mimi ni fresh graduate. Nimemaliza chuo mwaka jana. Katika mishe za kutafuta kazi nimehangaika sana. Nime apply sehemu kama 10+ hakuna hata moja nilioitwa interview.

Basi hivi karibuni kuna dada alinielekeza mahali akaniambia hiyo sehemu kazi zipo ila wanalipa hela kidogo sana nenda pale muulizie flani huyo ndo anaajiri hapo.. Nikaenda kupeleka documents zangu hata hakufungua yule jamaa. Baada ya kuuliza chuo nlichosoma basi akaniuliza unataka mshahara wa shillingi ngapi. I asked how much do you offer akasema Tsh 600,000 kiwango ambacho ni kidogo zaidi ya salary scale ya serikali (tsh 980,000) Kwa kua sijui ni uoga au ni desperation basi nikakubali. Akaniambia baada ya kuweka mambo yangu sawa nirudi.

Baada ya kutoka pale nilikua nimefurahi sana finally nimepata kazi lakini kila nikifikiria sina amani. I feel stupid. Nimeongea na rafiki yangu ameniambia yeye kapata kazi analipwa 1.5M hapo ndo nimechangamyikiwa kabisa. Nafikiria sijui nipotezee nisirudi pale. Sielewi cha kufanya. Kazi nataka lakini pesa ndogo. Sijui nifanye nini.
 
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
Kama bado hujaacha hiyo kazi basi we ni lofa sana tena ungekuwa mwanangu ningekupa adhabu ya kulisha mifugo na kujaza pipa la maji kwa miezi 3! Yaani ulipwe 600K na madigrii yako huku mwenzako akilipwa 1,500,000.00! Ona masifuri sifuri hayo yalivyojaa! Laki 6, OH MY GOD; si bora ukae home kucheki movie!
 
Shenz kabisa ww !!!mm mshahara wangu take home 380k bado nina familia nauli kila siku buku 2 chai na msosi mchana buku 4!! Bado nasurvuve kibishi kweli!!
Usilete undezi hapa
Shida zako ni zako .Don't inflict your own miserable life style into others lives . Usidhani kila mtu ana ndoto za kuishi kimaskini kama wewe . Kama hukuwa na cha kumshauri ni bora usingeandika upupu kama huu ulioandika . Pumbavu
 
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
Acha hio kazi,endelea kutafuta unayoitaka. Usifanye kabisa utaharibu kazi ya watu, maana wewe unatafuta mshahara sio kazi.
 
Basic. Maana yake wakikata naweza kuondoka na 400k.
Fanya kile moyo wako unapenda kama haujapenda huo mshahara fanya kazi huku ukijiongeza kucheki other companies wengi wanao comment hapa naona kama ni either huo mshahara hawajawahi kuupata au wanafuata mkumbo tu
 
Ukiikataa hiyo kazi utajuta sana baadae. Ulishawahi kusikia watu wamekaa five years bila ajira wanakula msoto? Wewe muda mchache hivyo na umepata kianzio kizuri na bado unakataa kweli?

Wenzio tulianza na mishahara hiyo hiyo tukakomaa. Wakati mwingine kama huna majukumu usiangalie sana mshahara bali tengeneza CV yako. Watu wanatafuta sehemu wafanye kazi bure kabisa ili tu kusafisha CV wewe na hela hiyo unaikataa.

Nakushauri chukua hiyo kazi wakati unatafuta pazuri zaidi lakini ukiona haikidhi vigezo vyako vya mshahara achana nayo ila nikwambie tu maisha mtaani magumu sana usidharau hiyo 600k mkuu.
 
Back
Top Bottom