Nimepata kazi lakini mshahara ni mdogo mno

Magnumpi

Member
Oct 4, 2019
68
172
Habarini humu ndani

Kama nimekosea jukwaa mtanisamehe. Mimi ni fresh graduate. Nimemaliza chuo mwaka jana. Katika mishe za kutafuta kazi nimehangaika sana. Nime apply sehemu kama 10+ hakuna hata moja nilioitwa interview.

Basi hivi karibuni kuna dada alinielekeza mahali akaniambia hiyo sehemu kazi zipo ila wanalipa hela kidogo sana nenda pale muulizie flani huyo ndo anaajiri hapo.. Nikaenda kupeleka documents zangu hata hakufungua yule jamaa. Baada ya kuuliza chuo nlichosoma basi akaniuliza unataka mshahara wa shillingi ngapi. I asked how much do you offer akasema Tsh 600,000 kiwango ambacho ni kidogo zaidi ya salary scale ya serikali (tsh 980,000) Kwa kua sijui ni uoga au ni desperation basi nikakubali. Akaniambia baada ya kuweka mambo yangu sawa nirudi.

Baada ya kutoka pale nilikua nimefurahi sana finally nimepata kazi lakini kila nikifikiria sina amani. I feel stupid. Nimeongea na rafiki yangu ameniambia yeye kapata kazi analipwa 1.5M hapo ndo nimechangamyikiwa kabisa. Nafikiria sijui nipotezee nisirudi pale. Sielewi cha kufanya. Kazi nataka lakini pesa ndogo. Sijui nifanye nini.
 
Acha upumbavu wewe....
Vijana wa siku hizi mna shida gani?

Kwanza, comperatively hiyo hela ni nyingi sana ukilinganisha na starting salary za watu wengi.... Kuna watu wako makazini 10+ years hawajafikia huo mshahara!
By the way, mshahara haujawahi kutosha hata siku moja.

Wewe unatakiwa ku focus katika kile unachotaka ku achieve.... And look at the bigger picture. Think hiyo kazi uliyoipata itakusaidiaje kufikia malengo yako say in the next 2,5,7,10 yrs? Kwani unataka ufie hapo? Au ni kampuni yako hiyo au ya baba yako?

Chukua hiyo kazi, do ur best fanya kazi, learn and learn and learn...... Inaweza kukufanya after 6 months or one year ukapata kazi ambayo mshahara ni mara 6 ya huo... Au hiyo kazi ikaku connect na mtu/kampuni ambayo inaweza kukupa kazi ya mamilioni.... au hiyo kazi ikakupa skills ambazo zitakufanya uwe lulu in the corporate world... Au ikakupa ujanja wa kuweza kuanzisha biashara au consultancy yako ambayo itakulipa zaidi...
Think.
 
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
akasema kiwango ambacho ni kidogo zaidi ya salary scale ya serikali (tsh 980,000)
Ulichoandika hapa ni sawa na mtu amekula milo mitatu alafu kisa haja pata juice anasema leo sijala, tena anasema mbele za watu ambao hawajala kabisa siku nzima.

Mkuu jifunze kutumia kichwa kufikiri kabla hujaandika upupu.
 
Dogo nenda kapige kazi upate experience wewe maslahi baadaye, ndyo kwanza fresh graduate wenzio tulikaa benchi for 3 years tukaja kupata kazi mshahara 150,000/=

Fanya Kwa malengo either for a year ,then tafuta sehemu unayoona inakufaa zaidi

Kila rakheri,wanasema safari moja huanzisha nyingine, wakimaanisha ukiwa kazini ni rahisi kupata kazi Nyingine tofauti na ukikaa home ukisubiri ije. Kakomaee !
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom