Nimepata kazi lakini mshahara ni mdogo mno

Kwa fresh graduate ambaye bado hujawa na majukumu makubwa sio mbaya kwa kuanzia..milango mingine itafunguka as you go. Kuna muimbaji aliimba "maisha ni foleni kila siku inasogea pole pole"

Kwahiyo usijali mdogo wangu utatoboa ila sio rahisi kuanza na mshahara mkubwa wakati ndio kwanza fresh graduate. Mshukuru sana Mungu kwa hicho alichokupa, kuna rafiki yangu alipata kazi akawa analipwa elfu tatu per day na degree yake.

Hiyo pesa ni kubwa tu kikubwa itumie kwa akili do not overspend, live within your means. Mungu akutangulie katika kazi yako mpya

Ahsante kwa kunipa moyo. Ahsante sana. Niliweka haya mawazo yangu humu ndani ili nipate mchango wa watu walionizidi experience lakini nimeambulia matusi tu.
Ahsante ntalifanyia kazi.
 
Usiache....yaani hapo hapo komaa fanya kazi hadi wafanyakazi wenzako wakushangae, piga kazi hadi wao waseme poo. Kuna msemo wa biblia unasema "aliye mwaminifu katika mambo madogo atakua mwaminifu katika mambo makubwa".

Hata ukienda sehemu wanayokulipa 1.5 M per month baada ya muda fulani utaona pesa haitoshi utataka kuongezewa tena. Pesa haitoshagi hata siku moja, we always want more. Kwahiyo fanya kazi mdogo wangu, kutokana na juhudi zako hata boss wako anaweza akaku recommend mahali pengine maana ameona una nidhamu uliyonayo kazini.
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
 
Jamaani sio laki 9 80 ningepata hiyo nisingekua hapa. Tatizo hamsomi kuelewa mnakimbilia kutukana tu.
Sisi tuliokuelewa tunakuambia kafanyekazi kwa hiyo 600K,au unapokaa bure unapata zaidi ya hiyo?Kumbuka hapo una manufaa ya kutengeneza Cv si unajua sehemu nyingi wanataka watu wenye uzoefu kazini? Fungua ubongo.
 
Dogo nenda kapige kazi upate experience wewe maslahi baadaye, ndyo kwanza fresh graduate wenzio tulikaa benchi for 3 years tukaja kupata kazi mshahara 150,000/=
Fanya Kwa malengo either for a year ,then tafuta sehemu unayoona inakufaa zaidi
Kila rakheri,wanasema safari moja huanzisha nyingine, wakimaanisha ukiwa kazini ni rahisi kupata kazi Nyingine tofauti na ukikaa home ukisubiri ije. Kakomaee !
Hiyo, tsh.150,000/= ulikutana nayo, mwaka gani? Nikupongeze tena na tena.
 
Sisi tuliokuelewa tunakuambia kafanyekazi kwa hiyo 600K,au unapokaa bure unapata zaidi ya hiyo?Kumbuka hapo una manufaa ya kutengeneza Cv si unajua sehemu nyingi wanataka watu wenye uzoefu kazi? Fungua ubongo.

Nimekuelewa. Ahsante
 
Usiache....yaani hapo hapo komaa fanya kazi hadi wafanyakazi wenzako wakushangae, piga kazi hadi wao waseme poo. Kuna msemo wa biblia unasema "aliye mwaminifu katika mambo madogo atakua mwaminifu katika mambo makubwa".
Hata ukienda sehemu wanayokulipa 1.5 M per month baada ya muda fulani utaona pesa haitoshi utataka kuongezewa tena. Pesa haitoshagi hata siku moja, we always want more. Kwahiyo fanya kazi mdogo wangu, kutokana na juhudi zako hata boss wako anaweza akaku recommend mahali pengine maana ameona una nidhamu uliyonayo kazini.
Unafaa sana kuwa mshauri na mpatanishi wa migogoro ya ndoa maana, umebadilisha uelekeo wa upepo ghafla, hakika kila atakaye pitia maandishi yako lazima atoke na upako wa mtazamo tofauti kabisa; kwamba mtoto mdogo uonyeshwa njia iliyo salama apate uzima daima.
 
Gradute wa idara gani analipwa 980 kwa serikalini? Nani kakudanganya?
Habarini humu ndani

Kama nimekosea jukwaa mtanisamehe. Mimi ni fresh graduate. Nimemaliza chuo mwaka jana. Katika mishe za kutafuta kazi nimehangaika sana. Nime apply sehemu kama 10+ hakuna hata moja nilioitwa interview.

Basi hivi karibuni kuna dada alinielekeza mahali akaniambia hiyo sehemu kazi zipo ila wanalipa hela kidogo sana nenda pale muulizie flani huyo ndo anaajiri hapo.. Nikaenda kupeleka documents zangu hata hakufungua yule jamaa. Baada ya kuuliza chuo nlichosoma basi akaniuliza unataka mshahara wa shillingi ngapi. I asked how much do you offer akasema Tsh 600,000 kiwango ambacho ni kidogo zaidi ya salary scale ya serikali (tsh 980,000) Kwa kua sijui ni uoga au ni desperation basi nikakubali. Akaniambia baada ya kuweka mambo yangu sawa nirudi.

Baada ya kutoka pale nilikua nimefurahi sana finally nimepata kazi lakini kila nikifikiria sina amani. I feel stupid. Nimeongea na rafiki yangu ameniambia yeye kapata kazi analipwa 1.5M hapo ndo nimechangamyikiwa kabisa. Nafikiria sijui nipotezee nisirudi pale. Sielewi cha kufanya. Kazi nataka lakini pesa ndogo. Sijui nifanye nini.
 
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi

Ulikosea mwenyewe unaulizwa tukulipe ngapi nawe ukauliza swali

Ulitegemea mwajiri akutajie mshahara mkubwa....nyambafuuuu....hivi huwa hamsomagi maswali na majibu ya usaili?

Anyway

Usiache kazi, private sector miaka hii Ni shida mnooo.... biashara ngumu

Fanya kazi, mshahara utapanda baadae.
 
Habarini humu ndani

Kama nimekosea jukwaa mtanisamehe. Mimi ni fresh graduate. Nimemaliza chuo mwaka jana. Katika mishe za kutafuta kazi nimehangaika sana. Nime apply sehemu kama 10+ hakuna hata moja nilioitwa interview.

Basi hivi karibuni kuna dada alinielekeza mahali akaniambia hiyo sehemu kazi zipo ila wanalipa hela kidogo sana nenda pale muulizie flani huyo ndo anaajiri hapo.. Nikaenda kupeleka documents zangu hata hakufungua yule jamaa. Baada ya kuuliza chuo nlichosoma basi akaniuliza unataka mshahara wa shillingi ngapi. I asked how much do you offer akasema Tsh 600,000 kiwango ambacho ni kidogo zaidi ya salary scale ya serikali (tsh 980,000) Kwa kua sijui ni uoga au ni desperation basi nikakubali. Akaniambia baada ya kuweka mambo yangu sawa nirudi.

Baada ya kutoka pale nilikua nimefurahi sana finally nimepata kazi lakini kila nikifikiria sina amani. I feel stupid. Nimeongea na rafiki yangu ameniambia yeye kapata kazi analipwa 1.5M hapo ndo nimechangamyikiwa kabisa. Nafikiria sijui nipotezee nisirudi pale. Sielewi cha kufanya. Kazi nataka lakini pesa ndogo. Sijui nifanye nini.
Ngazi ya degree government unaanza na TGSD ambayo ni sawa na 710,000/= kwa non science course. Kwa course za science unaanza na TGSE ambayo ni sawa na 950,000/=. Jitathimini kijana
 
Back
Top Bottom