Nimepata kazi lakini mshahara ni mdogo mno

Kiwango utaje mwenyewe kisha uanze kunung'unika baadae. Tatizo umeweka matarajio makubwa sana kuliko uhalisia wa maisha yalipo. Zile chai za chuoni za; "After a year, I will be a billionare as an employee into any sector." hizo zipuuze toka sasa, "Life is made up of ups and downs, never overrate it."
 
Ni ngum sana mtu (mbongo) aliyesugua benchi mtaani kwa muda mrefu afu akate mshahara wa laki tisa themanini elfu.

Jamaani sio laki 9 80 ningepata hiyo nisingekua hapa. Tatizo hamsomi kuelewa mnakimbilia kutukana tu.
 
Habarini humu ndani

Kama nimekosea jukwaa mtanisamehe. Mimi ni fresh graduate. Nimemaliza chuo mwaka jana. Katika mishe za kutafuta kazi nimehangaika sana. Nime apply sehemu kama 10+ hakuna hata moja nilioitwa interview.

Basi hivi karibuni kuna dada alinielekeza mahali akaniambia hiyo sehemu kazi zipo ila wanalipa hela kidogo sana nenda pale muulizie flani huyo ndo anaajiri hapo.. Nikaenda kupeleka documents zangu hata hakufungua yule jamaa. Baada ya kuuliza chuo nlichosoma basi akaniuliza unataka mshahara wa shillingi ngapi. I asked how much do you offer akasema kiwango ambacho ni kidogo zaidi ya salary scale ya serikali (tsh 980,000) Kwa kua sijui ni uoga au ni desperation basi nikakubali. Akaniambia baada ya kuweka mambo yangu sawa nirudi.

Baada ya kutoka pale nilikua nimefurahi sana finally nimepata kazi lakini kila nikifikiria sina amani. I feel stupid. Nimeongea na rafiki yangu ameniambia yeye kapata kazi analipwa 1.5M hapo ndo nimechangamyikiwa kabisa. Nafikiria sijui nipotezee nisirudi pale. Sielewi cha kufanya. Kazi nataka lakini pesa ndogo. Sijui nifanye nini.
We mbuzi kweli watu huu mwaka wa nne hatuna ajira wewe unakataa kisa mshahara mdogo? Fanya hapo huku unaongeza experience mbuzi kabisa.
 
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
Unalipwa kiwango kidogo ukilinganisha na nani?
Na kwanini ulinganishe na watu?

Na tangu ulisikia watu lazima walingane mshahara kwakua wamesoma pamoja wanaishi pamoja?
 
Kwa hiyo 980 ni hela ndogo? Unaijua salary scale za serikalini?
Mhh
Hamjanielewa shida sio kufanana na mtu, hapana. Shida ni kua nalipwa kiwango kidogo.
Niendelee kutafuta sehemu nyingine au nifanye hapo baada ya miezi kadhaa ni re negotiate na boss.
Naomba ushauri sio matusi
 
Habarini humu ndani

Kama nimekosea jukwaa mtanisamehe. Mimi ni fresh graduate. Nimemaliza chuo mwaka jana. Katika mishe za kutafuta kazi nimehangaika sana. Nime apply sehemu kama 10+ hakuna hata moja nilioitwa interview.

Basi hivi karibuni kuna dada alinielekeza mahali akaniambia hiyo sehemu kazi zipo ila wanalipa hela kidogo sana nenda pale muulizie flani huyo ndo anaajiri hapo.. Nikaenda kupeleka documents zangu hata hakufungua yule jamaa. Baada ya kuuliza chuo nlichosoma basi akaniuliza unataka mshahara wa shillingi ngapi. I asked how much do you offer akasema kiwango ambacho ni kidogo zaidi ya salary scale ya serikali (tsh 980,000) Kwa kua sijui ni uoga au ni desperation basi nikakubali. Akaniambia baada ya kuweka mambo yangu sawa nirudi.

Baada ya kutoka pale nilikua nimefurahi sana finally nimepata kazi lakini kila nikifikiria sina amani. I feel stupid. Nimeongea na rafiki yangu ameniambia yeye kapata kazi analipwa 1.5M hapo ndo nimechangamyikiwa kabisa. Nafikiria sijui nipotezee nisirudi pale. Sielewi cha kufanya. Kazi nataka lakini pesa ndogo. Sijui nifanye nini.
Ukute una GPA ya above 3.5..!!!

What a sad MILLENIAL

Braza nilianzaga kazi kwa wazungu Mshahara USD 150..!!!
 
“ACHA KAZI UONE KAZI KUPATA KAZI”

Read me between the lines nilichoandika hapo juu usichukulie maisha poa poa pitia nyuzi za wenzako humu wanatafuta hata kazi za kujitolea ili kwamba angalao baadae waonewe huruma wapewe kibarua na wanakosa.

Kwa akili hizi siamini kama umefika chuo labda umeishia chekechea wewe kwa upeo wako ukaona ni chuo umemaliza.
 
Alafu wewe dada nakuelewa sana naomba uni pm please kuna ishu naomba unishauri
Dogo nenda kapige kazi upate experience wewe maslahi baadaye, ndyo kwanza fresh graduate wenzio tulikaa benchi for 3 years tukaja kupata kazi mshahara 150,000/=

Fanya Kwa malengo either for a year ,then tafuta sehemu unayoona inakufaa zaidi

Kila rakheri,wanasema safari moja huanzisha nyingine, wakimaanisha ukiwa kazini ni rahisi kupata kazi Nyingine tofauti na ukikaa home ukisubiri ije. Kakomaee !
 
Kwa fresh graduate ambaye bado hujawa na majukumu makubwa sio mbaya kwa kuanzia..milango mingine itafunguka as you go. Kuna muimbaji aliimba "maisha ni foleni kila siku inasogea pole pole"

Kwahiyo usijali mdogo wangu utatoboa ila sio rahisi kuanza na mshahara mkubwa wakati ndio kwanza fresh graduate. Mshukuru sana Mungu kwa hicho alichokupa, kuna rafiki yangu alipata kazi akawa analipwa elfu tatu per day na degree yake.

Hiyo pesa ni kubwa tu kikubwa itumie kwa akili do not overspend, live within your means. Mungu akutangulie katika kazi yako mpya
Basic. Maana yake wakikata naweza kuondoka na 400k.
 
Back
Top Bottom