Nimepata kazi Dar es Salaam, je nitapata nyumba ya kuishi mjini?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Jana nimepeta barua ya kuanza kazi Dar es Salaam kwenye kampuni kubwa ya kimataifa yenye ofisi yake hapo mjini kwenye hayo maghorofa Samora avenue.

Natakiwa nihamie haraka iwezekanavyo, je nitapata nyumba ya kuishi hapo mjini kati maana sitaki kuishi sehemu ya kupambana na mabasi kila alfajiri, nataka nitembee tu kwenda ofisini.

Budget ya nyumba ya chumba na sebule self na jiko sh. 650,000 isizidi hapo au iwe chini ya hapo kwa mwezi pamoja na umeme na maji inclusive.

Isiwe na wahindi wengi wachache sawa, iwe na standby generator, iwe na parking ambayo ni safe ambaye itaweza kuenea gari aina ya subaru wagon ni ndefu kidogo sio fupi kama starlet.

PM kwa anayejua.
 
kwa chumba na sebule master duh hapana kampuni inanipa zaidi ya hapo ili nichague nyumba ya standard nnayo taka sasa si lazima nibaki na hela yangu kwa matumizi ya machine
Mbona hiyo 650,000 ni hela ndogo ,ongeza walau 970,000 tutakufikiria
 
Apartment labda Upanga,mtu akitokea lets say maeneo ya Regency kwenda Samora kwa mguu na mwingine akitoka labda Rombo akapanda mwendokasi express kwenda town,inawezekana wa express akawahi kufika,Kupanga ni kuchagua
 
kodi ntalipa ya mwaka mmoja kwanza sio zaidi ya hapo ntalipa kuanzia j3 ikiwezekana
 
Sehemu nzuri kukaa apo ni upanga ,unakatiza dakika mbili tatu upo samora .upanga ushuani ,kama utaitaji upanga njoo pm
 
kodi ntalipa ya mwaka mmoja kwanza sio zaidi ya hapo ntalipa kuanzia j3 ikiwezekana
Haacha huo ushamba, ulipe pesa ya mwaka mzima unaijua Dar es salaam wamiliki wengi wa Nyumba wana desturi za kusumbua na isitoshe Nyumba nyingi zinakuwa na matatizo nakushauri lipia Pesa ya miezi 3.
Matatizo ya Nyumba za kupanga apa Dar es salaam ni:-
Matatizo ya maji
Matatizo ya umeme
Matatizo ya majungu kati ya mwenye Nyumba na wapangaji
Matatizo ya mwenye Nyumba kuwa na kupenda kuomba kukopa Pesa kwa wapangaji wake
Matatizo ya watoto wa mwenye Nyumba kukuonea wivu kama wakikuona unafanya kazi
Matatizo ya ushirikina kwy Nyumba za kupanga na ufanywa na mwenye Nyumba au wapangaji

Kwa iyo apa Dar es salaam sio salama kutoa Kodi ya mwaka Maana ukikaa mwezi mmoja unaweza ukaikinai Nyumba
 
HUYO MWAJIRI ANAKULIPA MSHAHARA WA KULIPA PANGO 650K NA BADO AMESHNDWA KUKUTAFUTIA NYUMBA.

NENDA JENGO PACHA LA PSPF LILE... LA RANG YA NJANO PALE SOKOINE DRIVE, KWA MWEZ NADHANI M. 5
 
Jana nimepeta barua ya kuanza kazi Dar es Salaam kwenye kampuni kubwa ya kimataifa yenye ofisi yake hapo mjini kwenye hayo maghorofa Samora avenue.

Natakiwa nihamie haraka iwezekanavyo, je nitapata nyumba ya kuishi hapo mjini kati maana sitaki kuishi sehemu ya kupambana na mabasi kila alfajiri, nataka nitembee tu kwenda ofisini.

Budget ya nyumba ya chumba na sebule self na jiko sh. 650,000 isizidi hapo au iwe chini ya hapo kwa mwezi pamoja na umeme na maji inclusive.

Isiwe na wahindi wengi wachache sawa, iwe na standby generator, iwe na parking ambayo ni safe ambaye itaweza kuenea gari aina ya subaru wagon ni ndefu kidogo sio fupi kama starlet.

PM kwa anayejua.

Kama huna Mke na utakuwa unapenda ' Kubaioloji ' sana Mademu nakushauri tafuta Makazi maeneo ya Tegeta au Bunju Mkuu. Nilitaka nikushauri utafute Makazi maeneo ya Tabata ila tatizo Kubwa la huko ni upatikanaji wa Maji hivyo unaweza ukawa na wakati mgumu mno pale unapokuwa ' Unabaiolojika ' na Mademu wa huko Kiharufu ( japo si wote )
 
Dah mkuu kazi kwanza hayo mengine badae, wanawake wapo tu hawaishi, huko mbali sana sipendi sana joto kukaa mbali halafu kusafiri kwa umbali hivyo ndo nakwepa kabisa nataka mjini kati tuishi na wahindi
 
natumai nyumba hiyo sitaishi na mwenye yumba hapo hapo, nashukuru kwa ushauri wako maana nlitaka nsiwe na mzigo wa kumfikiria mwenye nyumba nashukuru ntalifanyia kazi
Haacha huo ushamba, ulipe pesa ya mwaka mzima unaijua Dar es salaam wamiliki wengi wa Nyumba wana desturi za kusumbua na isitoshe Nyumba nyingi zinakuwa na matatizo nakushauri lipia Pesa ya miezi 3.
Matatizo ya Nyumba za kupanga apa Dar es salaam ni:-
Matatizo ya maji
Matatizo ya umeme
Matatizo ya majungu kati ya mwenye Nyumba na wapangaji
Matatizo ya mwenye Nyumba kuwa na kupenda kuomba kukopa Pesa kwa wapangaji wake
Matatizo ya watoto wa mwenye Nyumba kukuonea wivu kama wakikuona unafanya kazi
Matatizo ya ushirikina kwy Nyumba za kupanga na ufanywa na mwenye Nyumba au wapangaji

Kwa iyo apa Dar es salaam sio salama kutoa Kodi ya mwaka Maana ukikaa mwezi mmoja unaweza ukaikinai Nyumba
 
Dah mkuu kazi kwanza hayo mengine badae, wanawake wapo tu hawaishi, huko mbali sana sipendi sana joto kukaa mbali halafu kusafiri kwa umbali hivyo ndo nakwepa kabisa nataka mjini kati tuishi na wahindi
Kwahiyo unataka wahindi wakati Watanzania wenzio tupo?
Kuhusu umbali usijali....bajaji,uber, boda ziko bwerere....
Afu kawaida ya mapopo hatuna umbali katika kufata kidate.

Nimewamiss sana watu wa mkoani.
 
Back
Top Bottom