Nimepata habari usiku huu saa 3 ya kwamba Salum Kabunda "Ninja" hatinaye tena...........

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Habari hizi nimepigiwa simu na mtu wa karibu naye.......Amefariki akiwa tegeta jijini Dar es Salaam taarifa zaidi tutawaletea.
 
Kwani ni nani huyu? Na ana maslahi gani kwa taifa hadi iwe mhimu kujua habari za kifo chake? Kama ni rafiki yako, sema tu kwamba umefiwa ili tukupe pole
 
Kwani ni nani huyu? Na ana maslahi gani kwa taifa hadi iwe mhimu kujua habari za kifo chake? Kama ni rafiki yako, sema tu kwamba umefiwa ili tukupe pole
Ni mchezaji aliyewahi kuichezea Yanga na kuliwakilisha taifa lake huko siku za nyuma, R.I.P Kabunda
 
Kwani ni nani huyu? Na ana maslahi gani kwa taifa hadi iwe mhimu kujua habari za kifo chake? Kama ni rafiki yako, sema tu kwamba umefiwa ili tukupe pole
Acha kukurupuka wewe kwani wote wanaotangazwa kuwa wamekufa hapa jukwaani wana umuhimu kwa taifa ,kwa taarufa yako Marehemu Salumu Kabunda umuhimu wake ni mkubwa kwa taifa hasa katika nyanja za kabumbu la nchi hii,RIP Ninja ulikuwa beki shupavu tofauti na mabeki wetu wa sasa ambao kwao ukakamavu ni msamiati
 
we wish him well in his new missions wherever he is...........and may the Almighty God have mercy on his poor soul.............
 
Sisi wapenzi wa Tukuyu Stars, Yanga na Taifa Stars tutakukumbuka daima.
Mungu akupumzishe kwa amani.
 
Kwani ni nani huyu? Na ana maslahi gani kwa taifa hadi iwe mhimu kujua habari za kifo chake? Kama ni rafiki yako, sema tu kwamba umefiwa ili tukupe pole

Kama haujui nini kinachozungumzwa ni Bora Kunyamaza, Buriani Salum Kabunda, Utakumbukwa Na Wapenda Soka Wote Hapa Tz.
 
R.I.P Ninja we will always remember you...,nakumbuka wakati huo "Salum kabunda ninja anapiga kulia kuleee kumtafuta Sanif Lazaro Tingisha,Mohamed Hussein Chinga one,Edibily jonas Lunyamila,Said mwamba kizota nk
 
ninja miaka ya 90 aliongoza kakakuona kwenye kombe la chalenji ikafika fainali.wasiomjua kabunda ni under 20. R.i.p ribelo wa kimataifa.
 
ninja miaka ya 90 aliongoza kakakuona kwenye kombe la chalenji ikafika fainali.wasiomjua kabunda ni under 20. R.i.p ribelo wa kimataifa.

maneno mujarab haya....pumzika lijendari wangu kabunda
 
Nakumbuka wakati yupo yanga ya Abasi Gulamali mwaka 91/92, kocha alikuwa Mziray akisaidiwa Charles Boniface Mkwasa, Huyo beki alikua noma, bora mpira uende mchezaji abaki, alicheza na kina Steven Nemesi,Sanifu Lazaro, Sahau Kambi,Keneth Mkapa,Said Zimbwe,Issa Athumani,Abubakari Salum,Justin Mtekele,Said Swedi,Ramadhani Kilambo,Athuman china,Peter Tino,John Mngazija,Thomasi Kipese,Willy Mtendawema,. PUMZIKA KWA AMANI Ninja.
 
Acha kukurupuka wewe kwani wote wanaotangazwa kuwa wamekufa hapa jukwaani wana umuhimu kwa taifa ,kwa taarufa yako Marehemu Salumu Kabunda umuhimu wake ni mkubwa kwa taifa hasa katika nyanja za kabumbu la nchi hii,RIP Ninja ulikuwa beki shupavu tofauti na mabeki wetu wa sasa ambao kwao ukakamavu ni msamiati
Salumu Kabunda aka Ninja atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika medani ya soka. Poleni familia yake na wanamichezo wote hususani wanachama na wapenzi wa Dar Young African.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom