Nimepata habari usiku huu saa 3 ya kwamba Salum Kabunda "Ninja" hatinaye tena...........

Kwani ni nani huyu? Na ana maslahi gani kwa taifa hadi iwe mhimu kujua habari za kifo chake? Kama ni rafiki yako, sema tu kwamba umefiwa ili tukupe pole

tulimkubali. inaonesha wewe ni kizazi hiki cha copa coca cola, ungekaa kimya kungoja wanaomjua
 
DAAAA KATUTOKA KABUNDA NAKUMBUKA MBALI SANA KWENYE MPIRA WA TZ
ALIIITWA SALUMU KABUNDA NINJA AU MSUDANI!
R.I.P BROTHER! a
 
R.I.P Ninja we will always remember you...,nakumbuka wakati huo "Salum kabunda ninja anapiga kulia kuleee kumtafuta Sanif Lazaro Tingisha,Mohamed Hussein Chinga one,Edibily jonas Lunyamila,Said mwamba kizota nk

kwake tigana kupiga palee ah anamtafuta ken mkapa anarudi nyuma anapiga kwake hamis gagalino anampata Kabunda golini pale anapigwa chenga Mwameja anapigaa gooo dah Yanga 1 Simba 0
May god give u a wonderful rest Kabunda.
 
RIP Ninja...
Nimekumbuka 'incidence' ya aliyomkwatua Kassongo Athumani....hadi Issa (RIP) akasusa kucheza na kuungana na waliomkimbiza Kassongo hospitali....
 
Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,poleni watanzania,poleni wanayanga,poleni ndugu jamaa na marafiki,let him rest in peace
 
Zamoyoni mogela"GOLDEN BOY"alikuwa hakatizi."Que ton ame reste en paix"AMEN
 
Kwani ni nani huyu? Na ana maslahi gani kwa taifa hadi iwe mhimu kujua habari za kifo chake? Kama ni rafiki yako, sema tu kwamba umefiwa ili tukupe pole

Hata tukikwambia haitokusaidia.
Cha msingi nenda kachukue kopo ukachambe.

Wewe ni mmoja kati ya ushuzi ambao mmekuja kipindi hiki cha kuamshwa na power breakfast.

Wakati tunaomjuwa Kabunda tulikuwa tunaamshwa na Kombora.
 
nakumbuka wao walikuwa na Kasanga Bwalya na sisi tukawa na Kabunda Ninja ''Msudan''.

Dah enzi hizo Mungu bado hajaondoka Tanzania.
watangazaji wa mpira walikuwa Chaaz Hilary, Omari Jongo, Bujaga Izengo na wengine weengi.
Fundi mitambo alikuwa Obi Mwambungu wakati msimamizi wa matangazo pale RTD alikuwa Nazir Mayoka.

Marehemu afande Mkama Sharp akiwa juu ya Farasi wake huku akiangalia hali ya amani kwa washabiki na vyombo vyao vya usafiri.

''Kifo hutaki watu wakipendana, umezoea kututenganisha, kifo eeh kifo, kifo hakina huruma''...

Kwa heri ya kuonana Kabunda...
 
Nakumbuka wakati yupo yanga ya Abasi Gulamali mwaka 91/92, kocha alikuwa Mziray akisaidiwa Charles Boniface Mkwasa, Huyo beki alikua noma, bora mpira uende mchezaji abaki, alicheza na kina Steven Nemesi,Sanifu Lazaro, Sahau Kambi,Keneth Mkapa,Said Zimbwe,Issa Athumani,Abubakari Salum,Justin Mtekele,Said Swedi,Ramadhani Kilambo,Athuman china,Peter Tino,John Mngazija,Thomasi Kipese,Willy Mtendawema,. PUMZIKA KWA AMANI Ninja.
Umemsahau mzee wa koma kumwanya, Godwin Aswile. RIP Salum Kabunda Ninja. Your pace, power and determination will remain in our memories forever
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom