#COVID19 Nimepata chanjo ya Covid-19 aina ya Johnson & Johnson, je wewe?

SHEDEDE

JF-Expert Member
Feb 6, 2021
339
551
Wakuu,

Leo asunuhi nimepata chanjo ya COVID 19 aina ya Johnson & Johnson; single dozi.

Kwakweli najiskia kujiamini sana kwenye vita dhidi ya Covid-19. Najiona ni mzima zaidi na kama vile hii vita nimeishinda.

Nimepata vi-contraindications kidogo kama vile kichefuchefu, mdomo kuwa mchungu na maumivu ya joints...nilirudi home nikalala 3 hrs.

Hali inaisha na ninaona nakua imara.

Dokta alinielimisha kabla kunichanja akasema hii chanjo ni ya kweli na serikali kupitia wataalam wake imezifanyia "GENOME ANALYSIS" na kubaini ni kweli wanachosema 'wazungu' ndicho kilichomo, na kweli kinatibu. Sikuelewa vizuri masuala ya kitaalam zaidi hayo.

Nilijisemea moyoni: uvumi unasema chanjo itaniua...lakini pia nafajamu corona inaweza kuniua. Nika conclude bora nife kwa chanjo kuliko kwa corona pasipo kupata chanjo.

Error type 1 vs. error type 2
 
Mzungu hawezi kuangamiza dunia au africa maana wao wanategemea africa/dunia vile vile..

Chanjo ni ya kweli, WHO hawawezi kupitisha vitu visivyo na uhakika.

Ikifika zamu yetu tutaenda.

Wewe umechanja kwenye category ipi? Mzee(55+) , Kada wa afya/mwanahabari/mwanasiasa au magonjwa sugu?
 
Nilijisemea moyoni: uvumi unasema chanjo itaniua...lakini pia nafajamu corona inaweza kuniua. Nika conclude bora nife kwa chanjo kuliko kwa corona pasipo kupata chanjo.
📌📌📌
 
Mzungu hawezi kuangamiza dunia au africa maana wao wanategemea africa/dunia vile vile....
Ni kweli hawawezi kuangamiza Afirca maana wanaihitaji. Kama walivyohitaji Marekani ya kaskazni, austraria n.k.

Unaweza kuniambia wenyeji wa America ya kaskazini na Australia wako wapi?
 
CCM wako wanafanya fix wakachanjwe kimya kimya, hawa watu dah
 
Back
Top Bottom