#COVID19 Nimepata Chanjo ya Corona nchini Marekani, puuzeni uzushi

Kwani lazima kila mtu achanjwe?! Hata chanjo ikiletwa si lazima kila mtu achanjwe. Ukijisikia kuchanjwa sawa,asietaka sawa.
Dawa au chanjo isio ya lazima siitaki mwilini mwangu.
Sawa, sio lazima lakini ni ujinga kwa viongozi kusambaza propaganda inayolenga kuwafanya wananchi wawe wajinga!
 
Kwani lazima kila mtu achanjwe?! Hata chanjo ikiletwa si lazima kila mtu achanjwe. Ukijisikia kuchanjwa sawa,asietaka sawa.
Dawa au chanjo isio ya lazima siitaki mwilini mwangu.
You think, act and behave the way society shaped you.
You have been wrongly indoctrinated!
 
Haya Kiranga na wengine mlio huko majuu mtatusaidiaje na sisi tupate anagalau hiyo mnasema unachomwa sindano moja tu[ j&J]? Huku hali tete, Jiwe anasema yeye anaamini BUBIJI itatuponya na wapambe wake wakina Msukuma ndio hao wanajenga NYUNGU vijijini kwao!!!
Mkuu nasikia watu wanaenda Nairobi kupata chanjo.
 
Kwa nini Kenya
kawadharau mpaka madaktari wetu
Halafu anakwambia ujifukize na uombe mamamamayeeeee
Akafe mbele useless Kenge
 
Nimefanikiwa kupata chanjo ya Corona hapa napoishi na kufanya kazi Dallas, Texas. Nimepata dose mbili za sindano kwenye bega ya kwanza tarehe 5 mwezi wa pili na ya pili tarehe 4 mwezi wa tatu. Nimepata chanjo kutoka kampuni ya Moderna. Nilivimba kidogo kwenye bega kwa mara zote lakini sijapata homa kama watu wengine wanapata homa kwenye sindano ya pili.

Chanjo ni muhimu na zinaokoa maisha hasa kwa wale wenye au ambao waliwahi kuwa na pumu, kisukari, wazee, wenye magojwa ya moyo na wamegundua pia wenye type A ya damu nao wanaumwa sana wakipata corona. Asilimia 90% ya watu wakipata hawazidiwi hivyo inawezekana hata wewe umeshapata Corona bila kujua. Lakini baada ya siku 90 unaweza kupata tena na inaweza kuwa mbaya zaidi maana mwili unakuwa hauna nguvu sana. Kwasababu kirusi cha corona kimekaa zaidi ya mwaka kinabadilika ili kiweze kuingia kirahisi kwenye miili yetu hii kitaalamu wanaita variant. Hivyo mpaka sasa kuna variant ya South Africa, England, Brazil na ili ya China. Ya South Africa ndiyo kali kuliko zote na ndiyo imeingia Tanzania kwa sasa na kusababisha watu kufa na kuumwa sana kulinganisha na ile ya mwanzo.

Kwenye kinga kuna kinga nyingi sana cha maana ni upatikanaji, usalama na chanjo kufanya kazi. Kuna vipimo vikubwa viwili vya kuzingatia cha kwanza ni kinga ya chanjo yaani ambayo inazuia mtu kupata Corona lakini cha pili je mtu akipata corona ambaye ana chanjo ataumwa kiasi cha kulazwa au kuzidiwa?. Hii ya south Africa inaonyesha kinga haifanyi kazi vizuri hasa kwa hii chanjo ambayo nchi za Africa inauziwa za Oxford Astrazenica au AZD1222. Hawajatoa data kuonyesha je mtu akiumwa inakuwaje au kinga inakuwaje. Lakini chanjo ya Johnson and Johnson imeonyesha inakinga ya corona ya south Africa kwa asilimia 57% lakini hata ukipata corona ni karibu 100% hautazidiwa. Lakini mpaka sasa HAKUNA MTU ALIYEPATA CHANJO YEYOTE POPOTE NA KUUMWA NA KUZIDIWA KIASI CHA KULAZWA. Hii ina maana gani ni kwamba inawezekana kinga ikawa ndogo lakini watu nhawatapoteza maisha ambao wana chanjo

Tanzania wanaogopa chanjo kama hii niliyopewa kwasababu inatumia technologia ya mRNA ambayo ni ya DNA na wanaogopa eti DNA zetu wazungu watabadilisha. Wakati nimeenda kupata chanjo kulikuwa na wazungu wengi wamepewa chanjo kama yangu sasa sijui hizi habari ni za wapi?!!!. Lakini kuna chanjo ambazo zina technologia kama chanjo za zamani mfano Sputnik V ambayo ni ya Urusi inatumia technologia ya zamani ya chanjo na sasa wamefanya utafiti unaonyesha inakinga aslimia 90%. Lakini hii ina order nyingi hasa huko South America itachukua muda kuipata.

Hivyo ushauri wangu ni kwa serikali kutumia chanjo yeyote kasoro ile ya China ambayo haina data ambazo watu wamezionana kusema zipo sawa. Lakini hii wenzetu wa Kenya, Nigeria, Ghana wamepata chanjo yenyewe inawezekana kinga ni ndogo kwa hii ya south Africa lakini ukipata chanjo corona itakuwa kama mafua ya kawaida haitakuuwa kama sasa hivi. Hivyo nashauri bado ni bora sana kuliko kukaa na kutokufanya maamuzi yeyote. Tukiweza kuweka order hii ya J&J ni zuri kwasababu ni sindano mmoja na inahitaji jokofu la kawaidia kuifadhi.

Tatizo serikali inaweza kusema wataalamu wanachukungaza lakini mpaka sasa hakuna habari yeyote uchunguzi umefika wapi, nani yupo kwenye hiyo team inawezekana ni maneno tu.
Tupe nauli na sis tuende
 
Kila siku watu wanakufa ,unaona ni wimbi la watu weng kufa sababu ni maarufu ,hiv kila anaekufa kila mkoa tukipost kama hao watu mashuhur mnaodai wamekufa na corona kutakalika ,si itaonekana ni vifo vya kutisha nchini ??

Hata hivyo kuna vifo vya kutisha sasa hivi hapa Nchini.
 
Mkishamalizana na chanjo...

Kesho mtaambiwa kuna corona mpya imeingia...
Covid 19+...

Utadhani series za simu...
 
Kwa Nini chanjo ya Corona imekuja haraka Sana hivyo kuliko chanjo za magonjwa Kama ukimwi ambayo Yana athari kubwa huku kwetu afrika?
Na kwa Nini mnapiga promo ya hiZi chanjo Nini kipo nyuma ya pazia?
 
Kama mtakumbuka kipindi Corona iliporipuka mara ya kwanza bwana billgate aliionya afrika kwamba kutatokea vifo zaidi ya milioni 30 vinavyotokana na korona akaja na mpango wa chanjo na ifanyiwe majaribio africa....Africa iliposhtuka kupitia mkuu wa who ndio wakaona waifanyie majaribio huko kwao,Sina imani na hiZi chanjo zenu Zina walakini Sana,wewe kwa kuwa uko USA basi ukila sumu unataka na watu wote wale.
 
Back
Top Bottom