Mbigu,mngeta,mpaka Mlimba ni kutamu sana kumetulia.Mbele ya ifakara...sijui ndo kilosa? Kuzuri ajabu kama jina lenyewe..imagine nilienda august kiangazi nikakuta greenish
😀😁😂🤣Hizo ni stress za kukutana na uliopiga nao kitabu mjini wapo levo nyingine. Sasa hiyo kitaalamu inaitwa kujicoumoflage kwa kukaa na nyani ambao hawatakuuliza “Sasa hivi upo wapi” kila ukipishana nao
Yaah kule kuko safi, lkn bigwa kule juu au Bong'ola mbona green mwaka mzima.Mbingu
Kila la kheri mkuu ..Kila mtu katika maisha kuna kitu anapenda, kila mtu ana tafsiri yake ya maisha na jinsi ya kuyafurahia maisha. Toka nimerudi kutoka South Afrika Kama kuna kitu natamani kufanya kwenye maisha yangu hapa Bongo na kitanipa furaha ya kweli, basi ni kwenda kujenga na kuishi Msituni,nilijikuta napenda kuishi kwenye misitu ya Iringa, Njombe au Mbeya.
Miaka 3 toka nimerudi nilianza maandalizi ya kulifikia hili, nilishanunua Shamba Kijiji Kimoja huko Njombe la Ekari 20, Nilichofurahi katikati ya hili shamba kuna bwawa kubwa la Maji. Niliona pia Africa Kusini wazungu wengi wamejenga mbali kabisa nje ya Miji. Mm nakwenda Msituni kabisa.
Halafu Msituni kuna utulivu wa aina yake. Napenda kile Kijaniii. Nimeshapanda mazao mbalimbali ya kudumu. Mwaka huu nimeanza kufuga pia. Nilinunua Water Pump na nilishajenga vyumba vyangu viwili. Shamba zima nimezungushia Miti ya Milingoti kama uzio wa shamba langu. Katikati nimepanda Parachichi na Apples nyinyi. Ukweli mazingira yanavutia sana. Kwenye Bwawa nimeanza kufuga Samaki. Pia nina Mizinga ya Nyuki 20 tayari.
Ukweli mjini nimeona mambo ni mengi sana, hakuna utulivu kabisa, presha ya maisha ni kubwa mno. Kila kona ni siasa tu, nimechoka siasa za nchi hii, Kila Kijana Mjini mwanasiasa. kwenye mitandao utakutana na maisha tu ya Mastaa na vituko vyao.
Maisha yangu ya Porini nimepanga kufanya Kilimo na Ufugaji tu, Siku moja moja nitatafuta Kanya au Tshepiso wangu wa Kijijini nakujitafunia. Sitaki Siasa wala negativity ya aina yoyote. Ndoto zangu za Baadae ni kujenga nyumba kubwa Shambani, Kununua Trekta na Mashine nyengine. Siku za Baadae kama nitamiss kuona Mkusanyiko wa watu wengi na Maghorofa basi nitarudi Mjini, nitakwenda moja kwa moja mpaka Airport.
Nitapanda ndege mpaka Ulaya, Marekani, au Asia Nitapumziko huko miezi na miezi halafu nikitosheka narudi porini kwangu Njombe. Mwakani naanza kuvuna Parachichi zangu na Apples. Karibuni sana. Nitajitahidi kuwa narudi hapa Jukwaani kuwapa Mrejesho wa maisha ya porini, faida na changamoto zake.
At story ya uongo jmn hahahhaha hahahhaha mpaka hapo hamu ushamtoaWewe Keagan Paul mbona una_reply na kuruka comments nyingine hapa?
Mfano kwa nini umekimbia uzi wako wa story yako ya uongo kuhusu kwenda south bila uwenyeji?
Kule ni mjini ujue....! Tunasema interior hukoYaah kule kuko safi, lkn bigwa kule juu au Bong'ola mbona green mwaka mzima.
Asisahau na solar power hata ya 200W inatosha sana.Haya maisha ninayatamani sana. Nunua wheel barrow hili litakusaidia kusafirishia vitu kati ya nyumbani na shambani. Hasa wakati wa mavuno.
Shoka unaihitaji kwa shughuli za kila siku. Kama utaweza kupata chainsaw kwa kukata miti ukipanua shamba hata miti ya ujenzi wa mabanda.
Kama una bwawa fuga na bata, kwenye bwawa mradi uwawekee sehemu za chakula na kutagia haya yanakua mabanda kwani mvua ikinyesha pumba zisinyeshewe.
Kama ukipata na grinder ndogo ya mahindi huhitaji vitu vingi.
Gari ni muhimu kwaajili ya kufuata mahitaji mjini mara moja kwa mwezi na kupelekea mazao sokoni.
Mwenzio huyo hapo alishawahi huko msituni....Kila mtu katika maisha kuna kitu anapenda, kila mtu ana tafsiri yake ya maisha na jinsi ya kuyafurahia maisha. Toka nimerudi kutoka South Afrika Kama kuna kitu natamani kufanya kwenye maisha yangu hapa Bongo na kitanipa furaha ya kweli, basi ni kwenda kujenga na kuishi Msituni,nilijikuta napenda kuishi kwenye misitu ya Iringa, Njombe au Mbeya.
Miaka 3 toka nimerudi nilianza maandalizi ya kulifikia hili, nilishanunua Shamba Kijiji Kimoja huko Njombe la Ekari 20, Nilichofurahi katikati ya hili shamba kuna bwawa kubwa la Maji. Niliona pia Africa Kusini wazungu wengi wamejenga mbali kabisa nje ya Miji. Mm nakwenda Msituni kabisa.
Halafu Msituni kuna utulivu wa aina yake. Napenda kile Kijaniii. Nimeshapanda mazao mbalimbali ya kudumu. Mwaka huu nimeanza kufuga pia. Nilinunua Water Pump na nilishajenga vyumba vyangu viwili. Shamba zima nimezungushia Miti ya Milingoti kama uzio wa shamba langu. Katikati nimepanda Parachichi na Apples nyinyi. Ukweli mazingira yanavutia sana. Kwenye Bwawa nimeanza kufuga Samaki. Pia nina Mizinga ya Nyuki 20 tayari.
Ukweli mjini nimeona mambo ni mengi sana, hakuna utulivu kabisa, presha ya maisha ni kubwa mno. Kila kona ni siasa tu, nimechoka siasa za nchi hii, Kila Kijana Mjini mwanasiasa. kwenye mitandao utakutana na maisha tu ya Mastaa na vituko vyao.
Maisha yangu ya Porini nimepanga kufanya Kilimo na Ufugaji tu, Siku moja moja nitatafuta Kanya au Tshepiso wangu wa Kijijini nakujitafunia. Sitaki Siasa wala negativity ya aina yoyote. Ndoto zangu za Baadae ni kujenga nyumba kubwa Shambani, Kununua Trekta na Mashine nyengine. Siku za Baadae kama nitamiss kuona Mkusanyiko wa watu wengi na Maghorofa basi nitarudi Mjini, nitakwenda moja kwa moja mpaka Airport.
Nitapanda ndege mpaka Ulaya, Marekani, au Asia Nitapumziko huko miezi na miezi halafu nikitosheka narudi porini kwangu Njombe. Mwakani naanza kuvuna Parachichi zangu na Apples. Karibuni sana. Nitajitahidi kuwa narudi hapa Jukwaani kuwapa Mrejesho wa maisha ya porini, faida na changamoto zake.
DuhHahahhaha ! Alimalizana na berries...zilivamiwa sana