Nimepanga kuacha kazi kisha kwenda kujiendeleza kimasomo

Soma open university au ongea na bosi wako vizuri..
Wapo waliofanya kazi mwaka mmoja tu wakapewa ruhusa ya masomo.

Kuna MTU aliajiriwa May/2014 na Oct/2015 akaenda masomoni. Na alisoma bachelor + masters.. Hivyo alipata likizo ya miaka 5..!!!

#YNWA
Ahsante kwa ushauri mkuu
 
Usithubutu kufanya hivyo, narudia tena USITHUBUTU. shule ipo tu, unakimbilia wapi? Yaani kuna wenzako wanakomaa waajiriwe serikali tena kwenye entry level position na wako above 35 yrs, wewe 32 inakuchanganya?
Utapoteka kazi na mke!
 
kama unafanya kazi ya medical moja ya sababu inayokufanya kuwaza kurudi shule ni kutambiana eneo la kazi, ma Md wanajiona sasa
wewe una familia, piga kazi baba achana na habari zakusoma hakuna maana yakuacha kazi uende kusoma alafu urudi kutafuta kazi tena, watu wapo kitaa wanasaka kazi na usomi wao
piga kazi, ongeza kipato kwa kufikiria ata biashara baba lakin sio kwa njia yakuongeza elimu..
Ahsante kwa ushauri
 
Usithubutu kufanya hivyo, narudia tena USITHUBUTU. shule ipo tu, unakimbilia wapi? Yaani kuna wenzako wanakomaa waajiriwe serikali tena kwenye entry level position na wako above 35 yrs, wewe 32 inakuchanganya?
Utapoteka kazi na mke!
Ahsante kwa ushari
 
Soma open university au ongea na bosi wako vizuri..
Wapo waliofanya kazi mwaka mmoja tu wakapewa ruhusa ya masomo.

Kuna MTU aliajiriwa May/2014 na Oct/2015 akaenda masomoni. Na alisoma bachelor + masters.. Hivyo alipata likizo ya miaka 5..!!!

#YNWA
Huwez kusoma any medical course open university
 
Okay,kama una familia tayari haijalishi mkeo ana kipato au hana(kipato cha mke hakihesabiki),komaa hiyo miaka 3/4 ya utumishi serikalini ndo ukapige shule kwa faida 2:


1-job security

2-kuna uwezekano raisi atakayekuja ataongeza mshahara,so kipindi utakachoingia shule mostly mshahara utakua umepanda hata kama si mkubwa ila afadhali


Lengo lako unataka ukapige kazi private sector

Private sector ili ufaidi ingia na elimu kubwa,so baada ya kumaliza pigs hata mph ukiwa kazini then omba likizo bila malipo then ukafaidi mahela huko private huku una uhakika wa ajira yako ya serikali pakinoga unapiga chini serikalini pakibuma uko na secured job with MD salary ambapo kwa kipindi hicho itakua inakidhi mahitaji
 
Sasa ndo miaka 6 hiyo?!?! MD Miaka mitano. Mwaka wa sita unakuwa unafanya kazi kwa vitendo Hospital fulani, unakuwa pia unalipwa. Ndo utauhesabia kama Mwaka wa 6?

Sema Miaka mitano.

Kuhusu kuacha kazi, sikushauri. Jaribu kuwaomba ruhusa, wakikataa basi unakuwa mpole.
Intern ni mwaka wa mafunzo , ni part ya shule pia ukiomba ruhusa huombi 5yrs unaomba 6 yrs ,
 
Hello mimi ni kijana mtanzania nina mwaka kwenye ajira ya serikalini but miaka 3 before nilifanya kazi private sector natamani nijiendeleze ila kutokana na mkwamo wa ajira za serikali itanibidi nisubiri mpaka 2024 ,, ndo nipate nafasi

Mwaka 2024 nitakuwa na miaka 32 , kozi nnayopenda kusoma ni 6yrs kumaliza itakuwa ni 2031

Kipi bora niache kazi nikasome mapema ila nikirudi ,na ganga private ,au nikomae
Kusoma sana ni woga wa maisha
 
Omba likizo ya bila malipo.Aga unaenda kusoma, hakuna ataekuzuia.Jamaa angu alipewa ruhusa kama hip 5 year.
 
Kuna taaluma ni lazima ukae darasani kwa ufanisi zaidi, mojawapo ni hiyo ya utabibu. Na kuna taaluma nyingine zinahitaji ujue zile basics halafu kulingana na consistency ya kazi kwa muda mrefu basi unakuwa mbobevu hasa kwenye sehemu hiyo.

Wenzetu huwa wanaangalia muda uliofanya kazi kwenye eneo fulani la taaluma kisha wakipima, wanakupa mwaka mmoja wa kupata theory na kukutunuku degree ambayo popote inatambulika.

Sio mfumo mbaya, na kuna baadhi ya maeneo hawajali sana makaratasi ila nini ulichonacho kichwani na output yako kwa eneo lako la kazi.

Kwetu, ni lazima uwe na karatasi za vyuo na utaaminiwa tu hata kama ulipata makaratasi kwa kudesa au kuhonga ngono.

Hivyo basi, ni muhimu kuwa na makaratasi makubwa na mengi tu ili uweze kuaminika kwenye ajira. Ila, kama ni kusoma kwa umri huo, soma kwa jinsi mfumo unavyotaka yaani uende shule kwa ruhusa yao, ukachukue karatasi(maarifa si muhimu sana huku kwetu) waliyokutuma kwaajili ya kukupandisha cheo.

Mwisho, si kila mtu asome kihivyo, kuna Mabwana na Watwana ili ulimwengu uwe na uwiano sawia. Wote hatuwezi kuwa Bakhresa au Dangote.
 
Hahaha eti Md wanajiona
kama unafanya kazi ya medical moja ya sababu inayokufanya kuwaza kurudi shule ni kutambiana eneo la kazi, ma Md wanajiona sasa 😂😂😂
wewe una familia, piga kazi baba achana na habari zakusoma hakuna maana yakuacha kazi uende kusoma alafu urudi kutafuta kazi tena, watu wapo kitaa wanasaka kazi na usomi wao
piga kazi, ongeza kipato kwa kufikiria ata biashara baba lakin sio kwa njia yakuongeza elimu..
 
Usiache kazi Mkuu , miaka inasogea mno hiyo 2024 sio mbali itafika hivi karibuni utaomba ruhusa kwenda kusoma .
Watu wanasoma wakiwa 40's sembuse wewe utakuwa 32 bado kabisa .
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom