Nimeota serikali imemfikisha Idris Sultan mahakamani na kumsomea mashitaka

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Nimeota kuwa upande wa serikali umefanikiwa kumfikisha Idris Sultan mahakamani na kumsomea mashitaka matatu.
1. Kukalia kiti cha Rais!
2. Kumvalisha Rais nguo za ki-BITOZI au ki-CHEKIBOB!
3. Kumkata kichwa Rais
Mashtaka yaliposomwa, Hakimu alitaka kuchanganyikiwa, akapekuapekua nyaraka huku anatingisha kichwa. “Si mlisema ni “CYBERCRIME, kumbe ni MURDER?”, akauliza.
Mwendesha mashitaka akajibu, “Ndiyo mheshimiwa, yote hayo matatu ameyafanya mtandaoni”
Mheshimiwa hakimu akazidi kushangaa akitingisha kichwa, mawakili 36 wa serikali nao wakaanza kunong’onezana.
“Jamani naombeni muwe serious!”, hakimu akaomba.
Mawakili wakainama kunong’onezana tena halafu mwendesha mashtaka akasimama na kutangaza, “Mheshimiwa, ni cybercrime ila nimeambiwa upelelezi haujakamilika. Kutokana na unyeti wa kesi hii, tunaomba mtuhumiwa asipewe dhamana mpaka upelelezi utakapokamilika!”


Credit: james GAYO
 
Hivi kumbe bado hajaachiwa??

Mungu ibariki Tanzania 😔​

#SerikaliYaWanyongeMyAss!!!
 
Hahahha!!!
16865103_836153086523660_6258834125230694905_n.jpeg
13939431_729424677196502_2744442513363133887_n.jpeg
13924938_727563510715952_2353552032890642902_n.jpeg
trump.jpeg
 
Back
Top Bottom