Nimeota ninakunywa bia, ila mimi sinywi bia. Nini maana yake?

no nm

JF-Expert Member
Apr 1, 2014
212
32
Wadau, mimi sio mlevi na wala situmii kilevi cha aina yeyote ile, Sitamani kuwa mlevi na wala sijawahi kuwaza kutumia kilevi, hata haya ma-energy drinks sijawahi kutumia.

Cha kushangaza jana usiku nimeota nakunya bia, nilipata pafu moja ila ikawa na ladha mbaya then nikaitema. Hii ni mara ya pili naota ndoto hii, mara ya kwanza ilikua kama miezi miwili hivi iliyopita, sijajua maana yake ni nini, na siajawahi kumwambia mtu yeyote.

Watumishi wa Mungu na Wajuvi wa kutafsiri ndoto, hii maana yake ni nini?

Nawatakia usiku mwema.
 
Ndoto hiyo umeota kwa sababu kichwani mwako na mawazoni mwako unaichukia sana pombe kiasi cha kwamba hupati picha itawezekanaje itokee unywe pombe haswa ukizingatia ladha yake mbaya labda na athari zake.

Kwa hiyo mawazo hayo ya namna unavyochukia ndo yamekuja usiku kama ndoto ya mtindo huo, ila haina maana yoyote ile ama kuashiria jambo baya maishani mwako.

Zaidi sana we kumbuka tu kuwa ndoto ni matokeo ya mawazo yetu ya mchana.
 
Si uanze kunywa bia mzee kwani ni sumu. Inaonekana unaitamani ila unaogopa wanaokuzunguka!

Anza kuonja onja utazoea. Anza anza na wine au desperado. Sio unatamani kitu mpaka unakiota haipendezi
 
Back
Top Bottom