Nimeota nimekatwa miguu nikawekewa ya bandia, naombeni ufafanuzi

Katika ulimwengu wa roho kukatwa mguu ni jambo zito sana - tayari mafanikio yako yanakwenda kukatwa na kuzikwa, ni suala la muda tu !!

Kwa kawaida miguu ndiyo inayokufanya ufanye shughuli zako zote ili kujiletea maendeleo , sasa ukishakatika unakuwa grounded...

Cha kufanya jitahidi ujinasue haraka sana, huyo ni adui ambaye anajiandaa kukumaliza ki-uchumi - Muombe Mungu wako saana kwa maombi na kufunga, ipende familia yako (wazazi, mkeo na wanao) toa zaka na kusaidia yatima, jitahidi usimtendee mtu kitu ambacho wewe ukitendewa hutapenda.

Unakwenda kwenye misukosuko mikubwa ya kimaisha, ila yaonekana utayashinda yote lakini utabaki na alama (miguu mbandia) you wont be the same as before baada ya dhoruba inayokujia kuishinda.
 
Ina maana kama ni mtumishi utaondolewa na kushushwa cheo.kama ni mfanyabiashara utapoteza mtaji wako wa maana na utategemea kwa mtu mwingine.
Mwisho wa tafsiri
 
Usipuuze,siku chache zijazo utajuta mana itakua kama ulivyoota,kama kweli umeota nipm nikupe namba za mchungaji umpigie akakufanyie maombi ili kubatilisha huo uharibifu kwenye ulimwengu wa roho
 
Kukatwa miguu kuwekewa ya bandia sio kitu kizuri, huwez katwa kitu chako ukawekewa ya bandia. Miguu yako imeenda wapi? Nani amepewa?

Mafanikio yako yamebarishwa, unapewa hatua fake we unahis ya kwako lakini sio ya kwako.

Kwa miguu unamiliki, Sasa ukipewa ya bandia unamilik vipi?
Jiombee, omba Toba halafu mwambie Mungu akupiganie miguu yako ilipo pelekwa irudishwe.

Nyie mnao puuzia ndoto mna hal mbaya Sana hata Kama hamsem, ndoto Iwe unaijua maana huijui maana yakupasa uombe
Mkuu, @Divine siku nyingi sana hujatokea jukwaani, nimefurahi sana kusoma bandiko lako hakika Mungu akubariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom