Nimeota ndoto iliyonifikirisha sana

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
251
636
Habari wana jamvi, ngoja niende moja kwa moja kwenye mada

Leo usiku nimeota kitu cha tofauti kidogo sio cha kushangaza lakini kilinifikirisha. Sijui ni ndoto fupi au niseme ninakumbuka kwa uchache sana kuhusu hii ndoto.

Nimeota nipo mahali na baadhi ya watu sio wengi sana, watu kama watu wanne hivi. Tulikuwa tunajadili kuhusu biblia, tunafundishana na kuwekana sawa.

Nilipoamka mstari pekee nilioukumbuka ni "YEREMIA 4:22" na nilopoamka tu nikaandika huo mstari kwenye note book ya simu yangu.

Sasa muda huu wakati napitia pitia note book yangu ndo nikauona na nikaona na maeleozo yake. Nikakumbuka

IKUMBUKWE: Mara ya mwisho kukaa na mtu kujadiliana nae kuhusu biblia ni wakati nipo sunday school (mwaka 2000), maana hata mafundisho sijafanya na kanisani kiukweli ni mtu wa kwenda kwa event; pasaka, christmass.

Hiyo YEREMIA 4:22 inasema "Watu wangu ni wapumbavu, hawanijui mimi. Wao ni watoto wajinga; hawaelewi kitu chochote. Ni mabingwa sana wa kutenda maovu, wala hawajui kutenda mema.”

Nawasilisha:
 
Aisee kuongelea biblia mwisho mwaka 2000 na umekumbuka mstari wa ndotoni😂😂😂. Mm hata saiv uniambie huo mstari nikisoge mbele sikuumbuki. Sijisifii ila nakupa hongera.

Hiyo ndoto imekukumbusha acha ujinga mfate Mungu wako.
 
Aisee kuongelea biblia mwisho mwaka 2000 na umekumbuka mstari wa ndotoni. Mm hata saiv uniambie huo mstari nikisoge mbele sikuumbuki. Sijisifii ila nakupa hongera.
Hiyo ndoto imekukumbusha acha ujinga mfate Mungu wako.
Amen kiongozi nitafanya hivyo
 
Back
Top Bottom