Nimeota napambana na paka mwitu Jeusi la kutisha kwa kupigana nalo kwa muda mrefu. Naomba tafsiri ya hii Ndoto

ndugu yangu ndoto yako ina maana hiii

hyo paka ulomuota ni adui wa kiroho linaweza kuwa kundi la wachawi au majini maana paka htumiwa sana na wachawi.

pili basi ni kipando hvyo huenda itakuwa hicho kikundi cha wachawi kilktaka kukuingiza kwwnye mfumo wao ila mungu amekulinda nao ila zaidi muombe mungu utashinda vita maana ndoto ilikuonesha kuwa huyo paka kapotea tu bila kujua kama umemuangamiza.
asante sana.Mungu Ataniwezesha kwa Hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnyama paka katika vita vya kiroho huwakilisha wakuu wa giza

Maana yake unamizimu iliyoweka mtego ktk maisha yako , kwa hiyo unafuatiliwa kwa ajiri ya maslahi Yao ktk ulimwengu wa roho

Solution

Unapaswa uwe karibu na muumba wako ili akuonyeshe hiyo mitego ukaiondoe mwenyewe maana hutegwa na ni vigumu kuifahamu . Nje ya hapo yatakusumbua mpaka kifo chako
asnte Sana Ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoto yako Haina mafumbo sana. Ila kabla ya yote kumbuka mwenye majibu sahihi ya ndoto yako Ni Mungu. Maandiko matakatifu imeandikwa "Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani."
Mwanzo 41:16

Lakini kwa ufahamu niliopewa nitakwambia machache
Ndoto ya kwanza paka anawakilisha Roho za kichawi. Hivyo ulichokuwa unaoneshwa unapambana nacho Ni roho za kichawi.

Ndoto ya pili basi ni chombo Cha usafiri Cha jumuiya. Katika basi mpo na watu mliosoma nao. Unapewa taarifa kiroho Kuna gari lilowabeba nyinyi nyote lakini Hilo gari limefikia mwisho wake hivyo unatakiwa utoke haraka maana Hilo gari linakwenda kuwadondosha muda mfupi baadaye. Umeandika kuwa gari kulikuwa linakwenda kwa Kasi likapasuka taili. Kinachoelezwa hapo Ni kuwa Jambo litatokea bila nyinyi kulitazamia mfano biashara unyoifanya imesitawi halafu ghafla inaporomoka. Angalia kwa msaada wa Roho mtakatifu kwenye elimu uliyoisomea au kazi au biashara nk.

NB: Hilo Ni onto Mungu amekupa ili akusaidie usije ukaangamia. Rejea habari za Nuhu na safina "Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani."
Waebrania 11:7


Zaidi muombe Mungu atasema nawe na kukupa maelekezo yote ya nini Cha kufanya.

Nyongeza Ni kwamba Mungu anaongea na Kila mtu Ni wewe tu kuamua kumsikiliza. Ameshaongea na mimi, mke wangu hata watoto wetu Kila Mara na tunajadiriana naye vizuri tu hivyo ondoa hofu jitakase nenda mbele zake muulize huku masikio yako ya rohoni yawe tayari kusikia
asante sana Ndugu Mungu akabariki sana nimekuelewa vema kabisa.Asante Sana kwa Kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuwa gari taili likipasuka huwa ndo mwisho wa safari
Tuanzia hapa kujuwa maendeleo yako shuleni ,maisha yako na wanafunzi wezako safari ya masomo na maisha.
Kama ni mwanafunzi inawezekana Darasa lenu mtafali,anza mchakato wa kuama shule.
Inawezekana shule umemaliza lakini wanafunzi ulioanza nao siyo ndiyo uliomalizanao pamoja.
Kwenye maisha inawezekana umefanikiwa lakin wezako wanafunzi wezako wapo kwenye shida

Kuhusu paka mweusi ulipigana naye baadaye akapotea sijajua nani alishinda lakini hilo pambano liliacha majerah. Na jerah linaweza kuwa lango la kuingiza uchafu

kuna ndoto mtu anaota anafukuzwa na Myama baadaye inapotea atutegemei kupata jerah
Asante Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoto Ni lugha ya picha ambayo Mungu huitumia kuongea na watu wake lakini pia shetani hutumia lango Hilo la ndoto kuingiza vitu vyake, lakini pia ndoto huja kwa ajili ya uchovu mwanadamu anaoupata wakati anapofanya kazi.
Soma
Matendo 2:17
Ayubu 7:14-15
Mhubiri 5:3

Lakini ndoto yako kiujumla Kuna roho ya uharibifu umeingiziwa. Angalia tabia ya konokono ni utaratibu, hawezi kwenda umbali mrefu. Angalia utaona ameingizia kwenye mkono, mkono ni kiungo unachotumia kufanya kazi, kwenye biblia imeandikwa " nitaibariki kazi ya mikono yako" . Sasa uwezo wa kufanya kazi umepunguzwa na matokeo yake uchumi wako utashuka.

Kifupi omba Toba kwaajili ya kilichosababisha ukashambuliwa
Tumia damu ya YESU kuinyunyiza kwenye mkono huo ulioshambuliwa kuing'oa hiyo roho na uharibifu wake.
Asante sana
 
Habari mkuu,
Pole kwa ndoto hizi maana kwa wengine huwapelekea kuwa na misongo ya mawazo katika maisha
1: Elewa ya kwamba paka katika ndoto huwa ni kuchezwa shere kwa muotaji na inatarajiwa aliyeota ajichunge na yale yanayomzunguka hasa katika watu aliona/anao fanya nao deal na pia kwa watumishi au wanaomfanyia kazi paka kumuota ndotoni vyovyote vile unatakiwa uwe na tahadhali kutokana na kuwindwa na adui wa kisiri siri. Kulingana na ndoto yako basi ni ishara kuwa tatizo hilo litakufika lakini utaweza kulivuka baada ya tabu na kama akikung'ata basi utahesabu kusumbuliwa na janga moja kwa mwaka mzima.

2: Kwa ndoto hii ya pili ni ishara kwamba unatakiwa uongeze elimu katika shughuli au jambo unalojishughulisha nalo na inakupa tahadhali usipofanya hivyo basi utaanguka na hii ni Sahihi zaidi mkuu chochote unachojihusisha nacho au unachotaka kujihusisha nacho ongeza elimu yake au utakwamia njiani na kushindwa kufanikia/ hata kwa jambo lolote unalofatilia muda huu

Kwa maana zingine za ndoto tembelea link hii utajua zaidi NDOTO NA MAANA ZAKE: ZIJUE NDOTO ZAKO

Rakims
asante sana Ndugu ubarikiwe Sana Nimekupata vema.Nitazidi kufanyia Kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
asante ndugu,ila sijihusishi kabisa na Mambo ya Hiza au kishirikina.Huwa Nakua Mtu wa Maombi SaNa labda ndio inapelekea kuwindwa na hawa Watu Waovu.asante kwa majibu
Tafsiri yake ni hivi paka mweusi ni nguvu za kichawi zinakufuatilia kwenye mambo yako

LA pili kuota uko na mliosoma nao zamani ni kuwa Tabia zako mbaya za zamani mbaya zimeanza kukurudia yaani MTU Wa kale kaanza kurudi.
 
Tafsiri yake ni hivi paka mweusi ni nguvu za kichawi zinakufuatilia kwenye mambo yako

LA pili kuota uko na mliosoma nao zamani ni kuwa Tabia zako mbaya za zamani mbaya zimeanza kukurudia yaani MTU Wa kale kaanza kurudi.
ASAnte Sana Ndugu Yangu.
 
usiumize kichwa na ndoto, utakuwa unaunia kichwa bils sababu, we just zipuuze tu nyingi ni matokeo ya vitu tunsvyofikiria na tunavyoons mchana, na si lazima viwe na maana kama tunayoambiwa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom