Nimeongea nae, anawasalimu na yuko pamoja nasi

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,416
85,842
Nilikua nae mchana wa leo, maongezi yetu yalianza kwa kulaumiana kwa nini niwe UKAWA! Nikamweleza nae akanieleza yafuatayo.

Moja, wameongezewa posh mara 100% na hivyo haoni sababu ya kutokujihusisha na mipango haramu ya kuiba kura.

Pili, wametawanywa kila mkoa na kwa Dar wako kila mahali, wamepangiwa vyumba kila kona ya jiji na kwamba wana vitambulisho vya "kiraia ". Kwa haraka huwezi kuwatambua ila wapo tuko nao na si ajabu hata ulipo uko nao!

Tatu, jana waliiitwa na Jamaa mahali na amewaahidi vyeo tena vyeo na magari ili wafanye hio kazi iliyowaleta huku mikoani.

Nimemuuliza swali, je uko tayari nchi yako iingie kwenye machafuko ili kulinda maslahi yako ya ahadi na ya watu wachache? Amesema Ndio yuko tayari. Nimeshtuka na nimeogopa.

Baada ya maongezi yetu amekubali kwa shingo upande kuwa atakua pamoja nasi, huyu ni mmoja tu kati ya wengi!

Nimeongea nae, anawasalimia. Tuiombee nchi yetu. Wametumwa kazi moja tu kufanya juu chini mkubwa wao ashinde!
 
umezungumza na kijana/mtu wa makumbusho.mwili wake hautaki mabadiiko ila nafsi yake inataka.wapo wengi wa namna hiyo.Mimi ni mmoja wao....raia wa kawaida ninaye taka mabadiliko.
 
Hahahahaaa, niliandika kuwa wakitaka wanaweza kuutafuta ukweli wa habari hii.

Unakumbuka kuna watu walikuwa wakipita katika nyumba za watu wakijifanya wanasajili namba za kupigia kura? Unaweza kuniambia walikuwa wakifanya kwa niaba ya nani?
 
mkuu Elli hebu tupe ufafanuzi kidogo juu ya ishara ya kazi wanazozifanya ambazo tukiwaona itakua rahisi kuwajua hawa jamaa
 
Last edited by a moderator:
mkuu Elli hebu tupe ufafanuzi kidogo juu ya ishara ya kazi wanazozifanya ambazo tukiwaona itakua rahisi kuwajua hawa jamaa
Mpwa utawajua tu wako wengi sana hapa Dar, wana kazi mbili kubwa tu kama nilivyosema hapo juu, wanajitahidi kuvaa kiraia na kuongea lugha za kistaarabu sana. ila ukiwaangalia vizuri utajua kuwa si wenzetu
 
Unakumbuka kuna watu walikuwa wakipita katika nyumba za watu wakijifanya wanasajili namba za kupigia kura? Unaweza kuniambia walikuwa wakifanya kwa niaba ya nani?
Mpwa sijui, siwezi kusema nisilolijua, mimi nalijua hili, wewe kama unajua hilo sema
 
Back
Top Bottom