Nimeona ujumbe unaodhaniwa ni wa Balozi wa Uturuki dhidi ya shule za Feza; Naomba Serikali iwe makini na mgogoro huu, wafuate taratibu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Serikali ya Uturuki ipo vitani kuwasaka wanaodhaniwa kufadhili mapinduzi miaka kadhaa iliyopita. Upo mgogoro mkubwa huko Uturuki na inatamani kuua nguvu za kiuchumi za maasimu wao ambao baadhi ni wamiliki wa Shule ya Feza iliyopo hapa nchini.

Serikali yetu inalo tatizo la kiukombozi, wakati wote Viongozi wetu wamekuwa wanawaza kukomboa watu fulani. Zamani Enzi za Mwalimu tulikuwa wakombozi wa waafrika wenzetu kutoka kwa wakoloni Lakini Sasa tumekuwa wakombozi wa viongozi wa mataifa mengi duniani waweze kuendelea kutawala.

Nimwombe Rais na Waziri wa Mambo ya Nje asiangaike na chokochoko za Waturuki. Kama wanaamini wamiliki wa feza ni wauaji basi wawasilishe hati ya mashtaka kwa mujibu wa Sheria.

Siyo Afya Balozi kukosa adabu na kutumia mitandao kushinikiza interest zao za kisiasa, wafuate sheria

Pia soma:
 
Yule balozi amenishangaza sana, maneno yake yalikuwa very undiplomatic. Pengine wameongea chini chini wanaona hakuna kinachofanyika. Naamini itakuwa ngumu kufunga hizo shule, unaanzaje kufunga best performing school, tena wanazosoma watoto wa viongozi hao hao 😳😳😳?
 
Mbona hujasema kuhusu yule wa Ujerumani aliyemtorosha Lissu na aliyemwambia Mbowe DO NOT GIVE UP
 
Serikali itakayojiingiza kwenye siasa za Erdogan na wapinzani wake itakuwa serikali ya ajabu sana.
 
Yule balozi amenishangaza sana, maneno yake yalikuwa very undiplomatic. Pengine wameongea chini chini wanaona hakuna kinachofanyika. Naamini itakuwa ngumu kufunga hizo shule, unaanzaje kufunga best performing school, tena wanazosoma watoto wa viongozi hao hao ?
Kibaya zaidi, viongozi wa Kituruki walioko madarakani ni waovu zaidi
 
Kwani ndio mnajua leo? Kwa mujibu wa Uturuki na Erdogan ,hizo shule zinamilikiwa na kiongozi wa Upinzani aliteratibu mapinduzi yaliyoshindwa, huyo bwana anaishi Marekani.

Ni miaka mingi tu wanatoa malalamiko.
 
Back
Top Bottom