Nimeona hizi picha kwenye Yahoo, nimesikitishwa eti ndizo picha bora za Afrika

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,861
1,302
Nimeona hizi picha kwenye yahoo, nimesikitishwa eti ndizo picha bora za Africa, Zione hapa baadhi

1622183950499.png

Hivi kweli hakuna kitu more positive katika Aftrica? Habari yote iko hapa.. Africa's week in pictures: 21-27 May 2021

1622184041060.png
 
Usawa haupo hii Dunia, kuna watu watapata Raha zote duniani Kwa sababu ya kuhodhi Mali na fedha ambazo kiuhalisia sio zao zote, lakini nao wasipate Raha huko tuendako baada ya maisha ya hapa.

Vinyo hivyo Kwa wengine hawatapata Raha ya duniani Hadi wanaondoka, Ila wakawa na Raha ya milele huko tuendako.
 
Usawa haupo hii Dunia, kuna watu watapata Raha zote duniani Kwa sababu ya kuhodhi Mali na fedha ambazo kiuhalisia sio zao zote, lakini nao wasipate Raha huko tuendako baada ya maisha ya hapa

Vinyo hivyo Kwa wengine hawatapata Raha ya duniani Hadi wanaondoka, Ila wakawa na Raha ya milele huko tuendako
Mkuu tafuta rahaa hapa ulipo maana hujui hizo story za huko uendako shauri yako.
 
cha ajabu ni kipi mbona nimewaona wazungu tena ulaya wanalala chini ya madaraja wanajifunika mabanketi yaliyochakaa
 
Mkuu tafuta rahaa hapa ulipo maana hujui hizo story za huko uendako shauri yako
Sio Kwa kupora na kuuwa ama kudhurumu haki za wengine, kisa Raha ya kitambo tu mkuu, itanisaidia nini Ikiwa nitaiba, kuuwa, kudhurumu nakuwa na kila kitu then niviache siku moja

Mkuu, Ila umenishauri vyema, lkin lile la mhimu zaidi staliacha
 
Kabla ya Kuwalaumu hao wanaotudhalilisha Waafrika hebu tujiulize kidogo je, na Sisi Waafrika wenyewe tunapendana, hatudhalilishani na wala hatuchukiani wazi wazi mpaka Kurogana na hata Kuuana? Waafrika hebu sometimes tuacheni Unafiki.
 
View attachment 1800061
Ndo usahihi wa maisha yetu, wapo sawa
Hapo kuna mabeberu wanapiga pesa ndefu kwa kutumia hizo picha. Kigezo cha kupata pesa ni kwamba wanakwenda Afrika kusaidia kaya masikini, ukiletwa mlungula wadau wanafaidi na kidogo mnakuja kujengewa vyoo mchezo unakuwa umeisha kiivyo.

Hivyo usitegemee mtu wa hivyo akuweke picha yako nzuri lazima atafute ile unayotia huruma umekaa kiboya boya akutangaze.

Hitimisho ni kwamba, anayetakiwa kuonyesha mandhari nzuri ya mazingira yetu ya kiafrika ni sisi wenyewe. Tukitegemea vinginevyo lazima tufanyiwe husuda. Tena hapo naona wametuonea huruma kidogo, miaka ya 2004 kurudi nyuma zilikuwa zinawekwa picha mtoto anataabika na njaa plus utapiamlo na kudhoofika halafu pembeni yupo tai anasubiri dogo akate moto tai amalize mchezo.
 
Nimeona hizi picha kwenye yahoo, nimesikitishwa eti ndizo picha bora za Africa, Zione hapa baadhi

View attachment 1800029

Hivi kweli hakuna kitu more positive katika Aftrica? Habari yote iko hapa.. Africa's week in pictures: 21-27 May 2021

View attachment 1800031
πš„πšœπš‘πšŠπš πšŠπš‘πš’ πš“πš’πšžπš•πš’πš£πšŠ πš”πš πšŽπš—πš’πšŽ πš™πš’πšŒπš‘πšŠ πš‘πšžπš“πšŠπš πšŠπš‘ πš”πšžπš–πšžπš˜πš—πšŠ πšœπš‘πšŽπšπšŠπš—πš’ πšŠπš”πš’πš πšŠ πš–πš πšŽπšžπš™πšŽ πš•πšŠπš”πš’πš—πš’ πš™πš’πšŒπš‘πšŠ πš£πšŠπš”πšŽ πš£πš’πš—πšŠπš–πšžπš—πšŽπšœπš‘πšŠ πš”πšžπš πšŠ πš–πš πšŽπšžπšœπš’ (π™½πšπš˜πš£πš’ πš—πš’πšŽπšžπšœπš’) πš•πšŠπš”πš’πš—πš’ π™ΌπšŠπš•πšŠπš”πšŠ πš”πš’πš•πšŠ πš™πš’πšŒπš‘πšŠ πš–πš πšŽπšžπš™πšŽ πš’πš•πšŠ πšžπš πšŽπšžπš™πšŽ 𝚠𝚊 πš”πš’πš£πšžπš—πšπšž πš”πšŠπš‹πš’πšœπšŠ? πš•πšŠπš”πš’πš—πš’ πš πšŠπš—πšŠπšœπšŽπš–πšŠ πšœπš‘πšŽπšπšŠπš—πš’ πšŠπš•πš’πšπš˜πš”πšŠπš—πšŠ πš—πšŠ π™ΌπšŠπš•πšŠπš’πš”πšŠ πšŽπšπš’ πšŠπš•πš’πš”πšžπš πšŠ πš–πšžπšŠπšœπš’.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kuna mabeberu wanapiga pesa ndefu kwa kutumia hizo picha. Kigezo cha kupata pesa ni kwamba wanakwenda Afrika kusaidia kaya masikini, ukiletwa mlungula wadau wanafaidi na kidogo mnakuja kujengewa vyoo mchezo unakuwa umeisha kiivyo.

Hivyo usitegemee mtu wa hivyo akuweke picha yako nzuri lazima atafute ile unayotia huruma umekaa kiboya boya akutangaze.

Hitimisho ni kwamba, anayetakiwa kuonyesha mandhari nzuri ya mazingira yetu ya kiafrika ni sisi wenyewe. Tukitegemea vinginevyo lazima tufanyiwe husuda. Tena hapo naona wametuonea huruma kidogo, miaka ya 2004 kurudi nyuma zilikuwa zinawekwa picha mtoto anataabika na njaa plus utapiamlo na kudhoofika halafu pembeni yupo tai anasubiri dogo akate moto tai amalize mchezo.

Nilijitolea kufanya kazi Mashirika ya msaada kama mawili makubwa kabisa duniani, nilichoka. CEO analipwa mshahara hadi Β£250,000K. 80% ya budget inaenda kwenye gharama za matumizi.

Wafanyakazi karibu 80% wanajitolea, kodi za maduka wapunguziwa, vitu wanapewa bure. Unajiuliza hizo 80% zinaenda wapi?

Ngapi zinamfikia mtu wa mwisho wa chini kabisa? Wajanja na Mashirika mengi ya dini yanafanya hivyo. Wameustukia mchezo.
 
Back
Top Bottom