Nimeona daraja la waya (cable stayed bridge) la SGR Kamata likivunjwa, shida nini?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,012
40,681
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa (Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika.

Ila cha kushangaza, jana nilipopita pale nimekuta mnara mmoja ukiendelea kuvunjwa, kwa mnaofahamu, nini kinaendelea?

==================================
Update: 12/10/2020

Nikweli linavunjwa, lilijengwa walipo limaliza tu likapata nyufa sehemu nya kitako baada ya sehemunitakayo pita reli, walikosana sana na msimamizi wa mradi hata injinia aliyesimamia ujenzi hapo alishafukuzwa.
Wakakubaliana waendelee na kazi nyingine hapo wata parudia.
 
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa ( Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika.

Ila cha kushangaza, jana nilipopita pale nimekuta mnara mmoja ukiendelea kuvunjwa, kwa mnaofahamu, nini kinaendelea?
Toka lini umekuwa mhandisi? Kwani shida iko wapi? Mlisema mkiingia ikulu mnabomoa reli madaraja na flyover! Sasa tumeanza kubomoa hilo la kamata mbona tena unachukia? Tar 28 kura zote kwa magu
 
Toka lini umekuwa mhandisi? Kwani shida iko wapi? Mlisema mkiingia ikulu mnabomoa reli madaraja na flyover! Sasa tumeanza kubomoa hilo la kamata mbona tena unachukia? Tar 28 kura zote kwa magu
Walisema akina na nani hadi unijumuishe? Unataka kujua kama mimi ni mhandisi?
 
Kwenye mradi mkubwa kama huu kubomoa na kurekebisha baadhi ya maeneo ni jambo la kawaida sana. Hongera kwa kufuatilia maendeleo ya mradi huu unaojengwa kwa kutumia kodi za Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom