Nimeona daraja la waya (cable stayed bridge) la SGR Kamata likivunjwa, shida nini?

Vipi kuhusu delays za mradi?
Mkandarasi mbobezi huwa anafanya calculations plus muda utakaotumika kufanya marekebisho, huwa hatuhesabu siku na muda wa kufanya kazi pekee bali pamoja na kuweka tahadhari ya kushughulikia yasiyoonekana yatakayojitokeza.
Ukifuatilia hata ujenzi wa barabara baada ya ukaguzi ujenzi ukiendelea...wakaguzi wasiporidhika huwa zinabomolewa na kujengwa upya kwa gharama za mkandarasi.
Mkataba lazaima uwe na kipengele cha tahadhari (Contingency)

Katika utendaji hili ni jambo la kawaida kabisa na hili lina BAJETI yake kabisa.
Najua wengi mtaliangalia kwa jicho la kisiasa.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hata muda (Time factor) usipouzingatia hasa kwenye masuala ya uhandisi ni HASARA.

So hasara zipo pande zote,kwa serikali na kwa mkandarasi.
Ni kweli lakini inategemea na kasi ya mkandarasi.
Huenda hadi sasa yupo mbele ya muda.
Labda kama hili limejirudia mara nyingi ni tatizo, vinginevyo kubomoa katika ujenzi ni sehemu ya ujenzi na inakubalika lakini isiwe zaidi ya 10% hilo litakuwa ni tatizo kubwa

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa (Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika.

Ila cha kushangaza, jana nilipopita pale nimekuta mnara mmoja ukiendelea kuvunjwa, kwa mnaofahamu, nini kinaendelea?

Ukikosea msingi ina bidi ufanyeje kama unajenga gorofa.engineer over
 
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa (Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika.

Ila cha kushangaza, jana nilipopita pale nimekuta mnara mmoja ukiendelea kuvunjwa, kwa mnaofahamu, nini kinaendelea?
Ukijua kujenga jua na kubomoa

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa ( Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika.

Ila cha kushangaza, jana nilipopita pale nimekuta mnara mmoja ukiendelea kuvunjwa, kwa mnaofahamu, nini kinaendelea?
Lissu akipiga picha hapo tukaona nuksi hiyo tumebadili michoro
 
This project will NEVER work because of the blood and theft money and mistreatment of Tanzanians.
Roho mbaya tu, the project will work na roho zenu mbaya mtalipanda tu, ptu. Watu kama mashetani, hiyo ni msaada kwa mamia ya raia, ila sababu amefanya magu mna wish hao watu waendelee kutaabika
 
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa (Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika.

Ila cha kushangaza, jana nilipopita pale nimekuta mnara mmoja ukiendelea kuvunjwa, kwa mnaofahamu, nini kinaendelea?
Nakumbuka siku moja kwenye mwezi wa saba hivi, nilipita kwenye daraja lile la kuning'inia pale Goldstar, Nilibaini kuwa zege iliyotumika kwenye kipande kile upande ule wa Goldstar ilikuwa ya chini ya viwango, ukilinganisha na maeneo mengine yaliyoisha kujengwa!, Naamini hata mafundi wajenzi waliokuwa juu siku hiyo walinishangaa mimi kwa kulishangaa daraja lile kwa muda. Sikuwa na mahali pa kuhoji ila nilimezea tu.... Kama ulichokiona ni kweli kimetokea, basi niwapongeze kwa kuliona tatizo mapema.
 
Kwenye mradi mkubwa kama huu kubomoa na kurekebisha baadhi ya maeneo ni jambo la kawaida sana. Hongera kwa kufuatilia maendeleo ya mradi huu unaojengwa kwa kutumia kodi za Watanzania wote.
Umejibu kihandisi mkuu. Kwenye ujenzi kubomoa ni kawaida kwa baadhi ya hatua au vipande fulani katika mradi. Ndio maana kunaundwa vifaa vya kubomolea na pia wahandisi hufundishwa kujenga kitu na kukibomoa pia.
 
Nakumbuka siku moja kwenye mwezi wa saba hivi, nilipita kwenye daraja lile la kuning'inia pale Goldstar, Nilibaini kuwa zege iliyotumika kwenye kipande kile upande ule wa Goldstar ilikuwa ya chini ya viwango, ukilinganisha na maeneo mengine yaliyoisha kujengwa!, Naamini hata mafundi wajenzi waliokuwa juu siku hiyo walinishangaa mimi kwa kulishangaa daraja lile kwa muda. Sikuwa na mahali pa kuhoji ila nilimezea tu.... Kama ulichokiona ni kweli kimetokea, basi niwapongeze kwa kuliona tatizo mapema.
Mkuu una uhakika na ukisemacho?! Baada ya kusoma hii thread nimepita pale leo hii. Lile daraja halikuwa limeisha. Ile section ambayo chini ndio magari yanapita kulikuwa na beams sio zege. Na nimepita leo walichoondoa ni zile beams tu. Sijui kwanini ila kilichoondolewa sio zege.
Cc FRANCIS DA DON
 
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa ( Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika
Ni bridges, siyo cable stayed
 
Mkuu una uhakika na ukisemacho?! Baada ya kusoma hii thread nimepita pale leo hii. Lile daraja halikuwa limeisha. Ile section ambayo chini ndio magari yanapita kulikuwa na beams sio zege. Na nimepita leo walichoondoa ni zile beams tu. Sijui kwanini ila kilichoondolewa sio zege.
Cc FRANCIS DA DON
Ok, Kesho nenda tena eneo lile lile, pale kwenye beam ya kwanza kati ya mbili zinazobeba daraja, ukitokea station kwa juu,simama upande wa Goldstar na uangalie kwa makini tofauti iliyopo ukilinganisha na sehemu nyingine zilizokwisha jengwa.
 
Vertical concrete beam moja nimeona kama imekwanguliwa/kumegwa nafikiri ni katika kuondoa hizo horizontal beams ambazo zilishaungwa au?
 
Holizontal beam moja ikiwa imeishaungwa wakati huo ndio iliyonifanya nishitukie "consistence" yake na "smoothness" yake, sina maneno mbadala ya kiswahili kwa maneno hayo.."...." Ila nikuhakikishie kwa asilimia mia niliona kuwa kuna kitu hakikuwa sawa pale.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom