Nimeombwa Ushauri na rafiki yangu kuhusu wasichana wake wawili

Huwa sipendi wanawake wasiri,yaan nikishagunduaga kwamba mwanamke alinificha kitu au anaficha kitu huwa napiga chini fasta...mwanamke msiri anaweza kukuumiza siku yoyote iwe kimapenzi au vyovyote!
 
Kama ni lazima aoe hao B ndio Ana faa

Kwanza ndio ambae yupo kwenye mahusiano

Pili Ana sifa nyingi njema kuliko kasoro zake

Ana onekana ni wife material kuzidi A

ila A anaonekana ni mchunaji yupo kwa mwamba kwa maslah kifup Ana act love Ata kule kujituma kitandani ni trick tuu ya kumkoreza jamaa

Mimi hapo ninge chukua B Ata kama Ana sura ya Baba
Mwamba kamata kinywaji baridiii
 
Nawasalimu kwa Jina la Jamuri ya Muungano wa Tanzania (Kiitikio - wote)

Ama baada ya salamu, dhumuni la andiko hili ni kuleta hoja niliyoletewa na rafiki yangu wa kiume akiomba ushauri kwangu. Mimi kwakweli nilishindwa kumshauri vema isipokuwa kwakuwa nafahamu kuwa kuna jukwaa hapa nikaonelea nililete hapa kwa mashosti zangu na kaka zangu waweze kutoa ushauri na mimi nitaufikisha kwa niaba yenu ndugu zangu.

Jambo lenyewe ni kuwa, best yangu huyu ana wasichana wawili lets tuwaite A na B ambao wote anadate nao. Kabla ya maelezo nilimuuliza kwa nini unadate na wasichana wawili, akajibu kuwa hakupenda iwe hivyo ila, ilitokea kama coincidence baada ya kuachana na huyu A na kuanza mahusiano na B, badae A alirudi kuomba mhasamaha na hakukubali moja kwa moja warudiane lakini A ni kama ameamua kukaa kwabest yangu hata kama hapati ushirikiano wa kutosha.

Sasa best yangu huyu anaomba ushauri kwasababu inaonekana sifa za hawa mashost wawili (A na B) zina mchanganya kiasi kwamba anataka afanye maamuzi sahihi ya kubaki na mmoja ili ikiwezekana mwakani aoe kabisa. Pamoja kuwa alikuwa ameshaamua kuachana na A bado tabia za huyu B zinamtia mashaka pia. Nitazieleza kwa kufanya comparison kama nilivyoelezewa pia.

1. A- Anajua majukumu ya ndani kama mke yaani anajituma kuanzia usafi hadi kupika bila kinyongo kabisa.
B - Anayajua majukumu ya ndani kama mke lakini ni mvivu Anafanya akijisikia na anapika siku akijisikia.
( Sifa hii ameipima kwa siku ambazo walimtembelea gheto)

2. A - Mara nyingi hana ushauri wa maendeleo kwa best yangu yaani bora siku ziende tu. (Anapenda kucritisize mawazo)
B - Ana mawazo mazuri na anamushauri mara nyingi best yangu jinsi ya kujiletea maendeleo (Anapenda kutia moyo)

3. A - Anajituma chumbani (wakubwa mtakuwa mmenielewa)
B - Chumbani bora siku ziende, yaani kawaida.

4. A - Anatoka familia ya kawaida yaani best yangu kutatua shida za nyumbani kwa huyu A ni kawaida.
B - Anatoka familia yenye uwezo wa kati, yaani best yangu wakati mwingine anapata support kutoka kwa huyu B

5. A- Anafanya biashara (duka) ila mara nyingi humwambia best yangu hela ya mwanamke ni ya mwanamke hivyo lazima apatiwe matumizi hata kama anabiashara zake.
B- Anafanya kazi ila pesa kutoka kwa mwanaume si kipaumbele sana isipokuwa vizawadi vidogo vidogo tu au pale inapobidi.

6. A - Ni msiri sana, mfano kuna wakati aliagiza gari kimya kimya, jamaa yangu alikuja kuambiwa tu rafiki wa huyo A kuwa hongereni maana gari yenu karibia inafika huku best yangu akiwa hajui kitu. Huo ni mfano mmoja ila kuna mengi.
B - Anapenda kumshirikisha best ynagu kila hatua ya maendeleo anayopanga kufanya na ikiwezekana anataka wafanye pamoja

7. A - Ni muongo muongo (anaweza sema nipo dukani leo kumbe amesafiri hata nje ya Dar es salaamu kabisa)
B - Ni suspect wa uongo ila hajakamatwa ( ni ile anaweza pigiwa simu bila kupokelewa hadi baada ya saa moja ndio anakuja na excuse kibao)

Wapendwa nisiwachoshe, ila samahani sana kwa wale watakao fanikiwa kusoma uzi huu naomba tushirikiane kumshauri huyu best yangu ili aweze kufanya maamuzi sahihi. Kuna siku nilijaribu kuuandika uzi huu kwa kutumia simu ukapanganyika hivyo ikabidi niuondoe, ila dhamira iko palepale ya kuomba ushauri ili tumsaidie kimawazo huyu best yangu. Tchao!

Piga chini wote aanze na upya, sifa hiyo ya mwisho inaweza ikamuua kabisa
 
Bi ndio mwanamke wa kuoa sex ni sehemu ndogo Sana ya mapenzi hua A ni mwanamke wa kustarehe nae tuu
 
B is a better option kwa jamaa, sema nini...mpe mwanaume wadada 100 then chukua mmoja kati yao ili abaki na 99, bado atatamani kuwa na huyo mmoja.
 
B ila amchane ukweli excuse za uongo as suspected. A ni jambazi la Urusi
 
Back
Top Bottom