Nimeoa Nina wiki 4 girlfriend wa zamani (chuoni) nae Ana panga safari aje

Wakuu nipo njia panda hapa sijui nifanye nini chuoni nilikua na mahusiano na binti wa kinyaturu Miaka mi3 lakni mwaka Jana nimemaliza namwambia twende kwao nikalipe mahari nilijikunjua mwanaume pesa za korosho nikalipe akagoma,, niliondoka chuoni nikamwambia nakupa miez mi4 tafakari nipo sirias..

Wakati huo nilijandaa kisaikolojia mapema nikarusha jiwe bukoba kwa muhaya.. Akaingia king.. Wiki 3 zilizopita nimemvuta kusini huku.. Maisha yameanza Safi..

Sasa yule wa chuoni ndo anasema na yeye anakuja Maana nilimpa ramani ya kwetu tukiwa wapenzi kipindi kile.. Sasa hapa nashindwa nifanye nini,,

Wakuu wenye nidhamu na hekima ushauri wenu.. Mimi mkristo Siwezi oa mitaala.. Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
Umelima miwa karibu na shule mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hapo wasi wasi uko wapi?
Unamwambia ukweli kuwa katika kipindi kile yeye anatafakari yeye wewe ulioa kabisa kwahiyo aendelee na maisha yake. Muwe marafiki tu. Full stop.
 
Ungemaliza utoto ndio uoe kwanza usingekuja na thread ya kipuuzi kama hii.
 
Back
Top Bottom