Nimeoa kumkomoa mwanamke nileyempenda kwa dhati. Najuta

Shy land

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
6,024
1,958
Nimeoa mwanamke ili kumukomoa mwanamke ambaye nilimpenda kwa dhati ambaye nilikuwa naye mahusiano kipindi cha mwaka mmoja.
Tuliahindiana kumuoa ila doto hizo zilizimika pale nilpomununulia simu ya Huawei y330.
Ikiwa siku moja nilipochukua simu yake nakwenda kwenye call history ili kuangalia namba anayowasliana nayo mara kwa mara.
Nikakuta namba ya mtu mwingine.
Ambayo namba ile ilikuwa imepingiwa na kupinga mara nyingi zaidi yangu mimi.
ambaye history ilionesha nimepigiwa mara tano na jamaa kapigiwa mara 89.
Siku ile nilichukua ile namba nakuipingia nakungudua ile namba kumbe ilikuwa na mimi ninayo kwenye simu yangu
Jamaa nikawa nimemujua.

Baada ya hapo nilimtafuta jamaa tukaongea kiume tukayamaliza na ili kumkomoa yule dada.

Tulielewana na jamaa tumuache wote na tukawa marafiki sote tukashauriana tukaoe kwingine kweli lengo letu lilifakiwa tukaoa na yule damu akabaki hana boyfriend tena.

Tangu nioe leo ni mwezi mmoja na mahali nimetoa ngombe 12
Baada tu yakuoa yule dada alikuja kwangu nakuniomba msamaha kwa yale yote yaliyotokea
Kusema ukweli nampenda sana huyu dada
Na huyu niliyemuoa sifurahii kabsa katika tendo hadi inafikia wakat ili kuijoy zaidi nihamishe akili kwamba ni yule wa zamani ninayefanya naye tendo

Vituko na dharau kwa huyu niliyemuoa zinanifanya nimkumbuke zaidi x wangu.

Jamani wana JF naomba msaada wenu wa mawazo nifanyaje kwenye njia panda hii ya mapenzi.
 
Pole sana ila hukujua kama unakosea lakini ni mapema sana kumkosoa pengine umpe muda zaidi na jaribu kumwelewa Mungu awasaidie ndoa yenu idumu milele . Amen
 
Nimepata tabu kuelewa jitahidi basi kuandika vizuri ndgu, ulifanya maamuzi yakiume sana kwanza jipongeze kwa hilo, siku zote songa mbele kaka,sikushauri uachane na mke wako wa sasa bali jifunze namna yakumfurahia kuachana sio suluhisho,na kama utaachana naye oa mwingine mpya achana na matapishi
 
Jifunze kutokulipiza visasi... ona ww umekurupuka... haya ndio yalio kukuta. Sasa ona ulipodumbukia.

Embu jaribu kuongea na mkeo....
Ikiwezekana shirikisha wazazi.. akizingua moe red card
 
wasukuma mambo yenu bwana..!!

ukajiona mjaanja....mwenyewe!

samehe ngo'ombe hizo mrudishe kwao huyo mdada
 
Huna jinsi. Maji ulishayavulia nguo inabidi kuyaoge, jitahidi kumrekebisha anapokosea nina imani atabadilika kwan mwezi bado ni muda mfupi usije ukachukua naamuzi ukaja kujuta baadae.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom