Nimeoa kumkomoa mwanamke nileyempenda kwa dhati. Najuta

Maamuzi yako yanaonyesha unampenda lakini ukachukua uamuzi wa hasira pole sana vunja hiyo ndoa tu maana humtendei haki huyo mkeo na mwisho wake utamuumiza mtu asie na hatia hapo.
 
Mhh ndo hapo naposhindwa kuelewa unakubalije kuoa mwanamke usiyempenda. Bora ya mwanamke akiolewa na mwanaume asiyempenda anaweza kujifunza kumpenda ila kwa mwanaume huwa ni ngumu. Pole sana mtoa mada ila ulikosea.

Naenda nje kidogo ya uzi, kuna hili suala la kusema mwanamke anaweza kujifunza kupenda anapokuwa kwenye relation na mtu mpya. Je lina ukweli au ni porojo tu ??
 
Ikitokea ukamuacha uliefunga nae ndoa na kurudia maumivu utakuwa umecheza "fyongo" heshimu hisia za mwenzio kwa sababu ushaamua kuingia kwnye maisha ya ubaba.vinginevyo utakaribisha mazingira ya majuto katka nafsi yko
 
Mkuu umetisha. Dah! Ng'ombe 12 au ni kuku 12? Halaf unafikisha mzigo home unakuta kumbe ndivyo sivyo. Dah! Haya, ukiurudisha mzigo kwa wenyewe itakuwaje kwani hata nusu au sijui robo mwaka bado. Huo utaweza kuitwa used kweli??
Sijui, nasema sijui. Halaf mkuu, huoni kinyaa kwani hata huyo unayemuwazia ili ufike kilele ni cha wote?? Haya mkuu, rudia matapishi kwani weye ndo mjanja kuliko yule wa calls 89 tena kwa sim ulonunua weye.
 
Ukitaka furaha ya maisha owa mtu unaempenda kwa dhati, lkn Kiowa kwa kufurahisha ndugu na marafiki ni sawa na kukalia moto unaofukuta chini.

Hiyo ni adhabu yako na uitumikie kwa dhati kbs, ndoa siyo kitu cha mchezo mchezo tuu. Furaha na utulivu unaupata kwa umpendae wewe umemkomoa ex wako.Malipo hapa hapa kesho hesabu.
 
Nimeoa mwanamke ili kumukomoa mwanamke ambaye nilimpenda kwa dhati ambaye nilikuwa naye mahusiano kipindi cha mwaka mmoja.
Tuliahindiana kumuoa ila doto hizo zilizimika pale nilpomununulia simu ya Huawei y330.
Ikiwa siku moja nilipochukua simu yake nakwenda kwenye call history ili kuangalia namba anayowasliana nayo mara kwa mara.
Nikakuta namba ya mtu mwingine.
Ambayo namba ile ilikuwa imepingiwa na kupinga mara nyingi zaidi yangu mimi.
ambaye history ilionesha nimepigiwa mara tano na jamaa kapigiwa mara 89.
Siku ile nilichukua ile namba nakuipingia nakungudua ile namba kumbe ilikuwa na mimi ninayo kwenye simu yangu
Jamaa nikawa nimemujua.

Baada ya hapo nilimtafuta jamaa tukaongea kiume tukayamaliza na ili kumkomoa yule dada.

Tulielewana na jamaa tumuache wote na tukawa marafiki sote tukashauriana tukaoe kwingine kweli lengo letu lilifakiwa tukaoa na yule damu akabaki hana boyfriend tena.

Tangu nioe leo ni mwezi mmoja na mahali nimetoa ngombe 12
Baada tu yakuoa yule dada alikuja kwangu nakuniomba msamaha kwa yale yote yaliyotokea
Kusema ukweli nampenda sana huyu dada
Na huyu niliyemuoa sifurahii kabsa katika tendo hadi inafikia wakat ili kuijoy zaidi nihamishe akili kwamba ni yule wa zamani ninayefanya naye tendo

Vituko na dharau kwa huyu niliyemuoa zinanifanya nimkumbuke zaidi x wangu.

Jamani wana JF naomba msaada wenu wa mawazo nifanyaje kwenye njia panda hii ya mapenzi.
Mkomeshe na huyo oa mwingine
 
sio uislam tu hata ukristo hakuna mahali wamezuia mtu kuoa mke zaidi ya mmoja isipokuwa tumefata ustaarabu wa wazungu badala ya kufata kweli yaani biblia
Imeandikwa mtu asipunguze neno katika kitabu hiki maana sehemu yake itaondolewa katika uzima wa milele na mtu asiongeze neno maana ataongezewa mateso katika hukumu... Unataka kusema Mungu alimuumba Adam na wanawake wangapi? Kwanini asingemuumbia wanawake wengi kama ni sahihi mahusiano ya namna hiyo; unadhani haya magonjwa yote tuliyonayo yanayoenezwa kwa ngono ni jambo jema?
Imeandikwa mtu atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe sio wakeze.
Usiongelee ukristo kwa point za kijinga, usimtukane kristo kwa tamaa zako.
Eti ustaarabu wa wazungu
 
wewe ni maamuma wa maandiko kina ibrahim yakobo daudi na wengine walikuwa na wake wangapi?ni wapi Mungu au biblia imekataza mtu kuwa na mke zaidi ya mmoja
 
biblia haijakataza wala kuzuia watu kuoa wake zaidi ya mmoja isipokuwa walioleta dini walileta na ustaarabu wao wakiwaaminisha kuwa ni dini
 
Imeandikwa mtu asipunguze neno katika kitabu hiki maana sehemu yake itaondolewa katika uzima wa milele na mtu asiongeze neno maana ataongezewa mateso katika hukumu... Unataka kusema Mungu alimuumba Adam na wanawake wangapi? Kwanini asingemuumbia wanawake wengi kama ni sahihi mahusiano ya namna hiyo; unadhani haya magonjwa yote tuliyonayo yanayoenezwa kwa ngono ni jambo jema?
Imeandikwa mtu atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe sio wakeze.
Usiongelee ukristo kwa point za kijinga, usimtukane kristo kwa tamaa zako.
Eti ustaarabu wa wazungu
kwa kukusaidia tu imani ya ukristo tuliyoletewa na wazungu ina matobo kibao likiwemo hilo zaka utatu mtakatifu na mengine mengi mara sijui shetani alikuwa malaika yote haya ni uongo hakuna ukweli hapo
 
Naenda nje kidogo ya uzi, kuna hili suala la kusema mwanamke anaweza kujifunza kupenda anapokuwa kwenye relation na mtu mpya. Je lina ukweli au ni porojo tu ??
Ndio lina ukweli. Inawezekana mwanamke akawa ameolewa au kudate na mwanaume ambaye hakumpenda ila upendo anaouonyesha yule mume kwa mkewe humvuta mwanamke. Baada ya mda mke hujikuta anampenda mmewe tofauti na mwanzo. Umewahi kuwaza inakuaje mdada amechaguliwa mchumba na wazazi halafu akawa hamkubali jamaa, then anaolewa kwa shingo upande ila baada ya muda anakuwa tofauti, anaonyesha upendo wa hali ya juu kwa mumewe.
 
wewe ni maamuma wa maandiko kina ibrahim yakobo daudi na wengine walikuwa na wake wangapi?ni wapi Mungu au biblia imekataza mtu kuwa na mke zaidi ya mmoja
Hao hawakua wake walkua vijakaz mkuu Ibrahim alikua na mkewe Sara mpk Sara alipotaman mtt na kumruhusu mmewe kutembea na kjakazi na sio kuoa mke wa pili.... Mpk Mungu alipoona maumivu ya Sara nakuwapatia Mtt ktk uzee.. Mke ni 1 tu mkuu
 
Nimeoa mwanamke ili kumukomoa mwanamke ambaye nilimpenda kwa dhati ambaye nilikuwa naye mahusiano kipindi cha mwaka mmoja.
Tuliahindiana kumuoa ila doto hizo zilizimika pale nilpomununulia simu ya Huawei y330.
Ikiwa siku moja nilipochukua simu yake nakwenda kwenye call history ili kuangalia namba anayowasliana nayo mara kwa mara.
Nikakuta namba ya mtu mwingine.
Ambayo namba ile ilikuwa imepingiwa na kupinga mara nyingi zaidi yangu mimi.
ambaye history ilionesha nimepigiwa mara tano na jamaa kapigiwa mara 89.
Siku ile nilichukua ile namba nakuipingia nakungudua ile namba kumbe ilikuwa na mimi ninayo kwenye simu yangu
Jamaa nikawa nimemujua.

Baada ya hapo nilimtafuta jamaa tukaongea kiume tukayamaliza na ili kumkomoa yule dada.

Tulielewana na jamaa tumuache wote na tukawa marafiki sote tukashauriana tukaoe kwingine kweli lengo letu lilifakiwa tukaoa na yule damu akabaki hana boyfriend tena.

Tangu nioe leo ni mwezi mmoja na mahali nimetoa ngombe 12
Baada tu yakuoa yule dada alikuja kwangu nakuniomba msamaha kwa yale yote yaliyotokea
Kusema ukweli nampenda sana huyu dada
Na huyu niliyemuoa sifurahii kabsa katika tendo hadi inafikia wakat ili kuijoy zaidi nihamishe akili kwamba ni yule wa zamani ninayefanya naye tendo

Vituko na dharau kwa huyu niliyemuoa zinanifanya nimkumbuke zaidi x wangu.

Jamani wana JF naomba msaada wenu wa mawazo nifanyaje kwenye njia panda hii ya mapenzi.
Mwezi tu ikifika miezi 3 . Hasira hasara uliniacha ukazani sifa mwenzio aliyekwambia kaniacha nk nae hapa..... Unazani kukaa na mtu usiyempenda mchezo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom