Leo nimekutana na maajabu ambayo sikuyategemea mchana huu hapa jijini Mwanza.
Nimekwenda kupata mahitaji kwenye supermarket ambayo huwa ninapenda kufanya manunuzi yangu hapo.
Katika hali nisiyoitegemea, ile naingia tu akanifuata mhudumu wa kiume akaniamkia baada ya salamu akaniambia kuwa nakuomba ukatafute huduma yako sehemu nyingine, nikahamaki kwanini??
Akaniambia kwa sauti ya chini kuwa, umerokodiwa kwenye kamera yetu hapa dukani ni msumbufu kila ukinunua kitu UNAOMBA RISITI, kuna siku ulinunua mkate ukaomba risiti, siku nyingine maziwa ya mtindi ukaomba risiti na jana ulinunua dawa ya mbu excel ukaomba risiti.
Kama kuna mdau wa TRA Mwanza kwenye hapa JF tuwasiliane inbox nimuelekeze hiyo supermarket ilipo!