Nimenyang'anywa Watoto wangu na moyo unaniuma maana nawataka sanaa

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
672
1,000
Sijui niseme kunyang'anywa au vipi...

Ila iko hivi...

Ni ndefu kidogo ila naomba jitahidi uimalize ili uweze kunishauri jinsi ya kuwapata watoto wangu (wakike) wa 4....

1. MTOTO WA KWANZA.

2012 nilimaliza Diploma nikapata Kazi mapema sanaa (nilimaliza chuo June na July nikapata ajira). Nikabahatika kupata binti mzuri sanaa, tukawa kwenye mahusiano mazito na mazuri sanaa.

2013 akapata mimba, nikaona ndio wakati wa kumuoa. Alinishauri nisubiri ajifungue ndio tutaoana. Kwelii bana 2013 hiyo hiyo akajifungua binti copy yangu na mimi nikarudisha ile hoja ya ndoa mezani. Akanijibu "bila wewe KUBADILISHA DINI Basi mi sitaki ndoa..!!""

Mimi ni mkristo na yeye ni muislamu. Wazazi wake wakakomaa kweli mimi nibadili dini ili nimuoe binti yao. Nikagoma kabisa, nikawaomba nifunge ndoa na binti yao ya serikali hiyo ilikua January 2014 mara May 2014 naona anapost picha FB kaolewa na muislamu mwenzake.

Duh ghafla sanaa. Kiukweli iliniuma balaa. Ila nikavumilia kiume. Nilimuomba Basi anipe mtoto wangu nimlee ye aendelee na ndoa yake "alijibu mtoto gani.

Mpaka leo 2021 sijui mwanangu yuko wapi na yule dada (X) kwasasa hatumii social media yoyotee hivyo hata sijui wapi anaishi na huyo mumewe.

Familia yake imegoma kabisaa kunipa ushirikiano. Baba ake binti kupitia simu ya mdogo ake binti alishawahi kunipiga mkwara atanisomea albadili hivyo niachane na familia yao. 2014 hiyohiyo Nikafuta mawasiliano yao yotee ili kuleta amani.

NAMUNHITAJI MWANANGU ILA AMEIBWA NA UKOO WA KIISLAMU WALIONIITA MIMI KAFIRI...!!!

2. MTOTO WA PILI

October 2014 nikapata Kazi mkoani (baada ya interview kali sanaa, tulikua waombaji 1000 na kitu huko na nafasi 88 bila connection wala kujuana nikatoka kwenye list wa 42).

Nikahamia mkoani kazini. Kazini kwa pembeni kuna private firm nikatokea kumpenda dada mmoja. Kilichonivutia kwake ni upole wake na ukarimu. Baada ya mahusiano kukolea akashika mimba. Maisha yakaenda akajifungua. Tukawa tunaishi wotee, wazo la kumuoa likaja.

Sasa bana.. kuna siku ile nasachi pochi yake kutafuta 1000 nikanunue vocha nikakutana na VIDONGE VYA HIV@ARV. Nilishtuka balaa.

Nikapiga picha na kunyamaza. Jioni nikamuhoji akaanza kulalamika kwanini nasachi vitu vyake (kasahau yupo kwangu..!!!) Mi nilichojibu ni kuchukua begi la mgongoni na baadhi ya nguo na kusepa. Nikaenda kukaa kwa mshkaji, nilimuachia kila kitu.

Baada ya muda nikaona anaanza kukondaa (kumbuka tupo jirani ofisini) kuumwa umwa. Niliona bora nimshirikishe dada ake (ni nesi wa hospital kubwa tu) asije akafa mwanangu akapoteza mama.

Dada ake hakuamini, alisema "asante kwa kuniambia, ila wewe shida yako umuokoe mwanao, Basi mi naomba unisaidie pia kumuokoa mdogo angu".

Basi tukafanya kikao nae, alikiri kweli aliupata zamani kutoka kwa mchungaji. Ila baadaye alitaka kuolewa alivyoona mchungaji ni mume wa mtu akaona bora anyamaze asiniambia kwa maana alinipenda. Na aliaanza kutumia ARV ili anilinde. Na mtoto ni mzima.

Basi kwa kuthibitisha hili nilienda kupima mara kumi (kila baada ya wiki nilipima hospital mbili tofauti) na majibu yoote yaliyotoka mimi na mtoto ni wazima.

Nikapanga kwengine na kuwaachia gheto, nikawa nawasiliana nae sababu ya mtoto. Mara ghafla nikawa simuoni kazini kwao.
Kumbe aliuza kila kitu anakimbilia sauzi (alipata kazi huko). Ila mpaka leo sijui sauzi kaenda lini, yupo pande gani huko, ofisi yake mpya inaitwaje. Kifupi SIJUI CHOCHOTEE kuhusu alipo na mwanangu...!!!

3. MTOTO WA 3

November 2015 nikarudi Shule kusoma bachelor mkoa mwengine (ofisi ilinipa ruhusa).

Nikiwa mwaka wa pili wakaja first yr. Nikajipatia chombo kikaliii (mtoto white). Tukaanza mapenzi alinikuta nakaa hostel. Akapanga chumba na kuniomba tuishi wote. Nikakubali, maana wote tulitoka kazini (in service).

Mapenzi yakawa motomoto. Marafiki zake wakawa marafiki zangu. Mi nilimaliza bachelor nikaunga masters chuo cha jirani. Mwaka wa 3 wake chuoni (2019) ukafika, ila mwezi mmoja kabla hajamaliza alisema Nina mimba YAKO..!!!

Nilifurahi balaaa, nikasema Basi sawa ""maliza Shule, jifungue tuoane" Kwahiyo nikawa namlea yeye na mimba yake. Mi niko masters mwaka wa 1 ye yupo bachelor mwaka wa 3. Mara akamaliza, akasema anaenda kwao kulea mimba yake hivyo mimi nijiandae kwenda kujitambulishe. Nikaona poa.

Mi nikamaliza fisrt yr (course work) ila second yr (research) nikaona nikafanyie kazini huku nikisuka mipango ya kwenda kuchukua mke.
Kufika kwao akawa hapokei simu, na ujinga niliyofanya sikua namjua hata ndugu yake mmoja. Mara namba yake ikawa imefungwa.

Ikabidi nishirikishe rafiki zake, siku moja rafiki yake mmoja aliniambia "Tukutane nikupe ukweli" Nikafunga safari hadi mkoa wake (nae baada ya kumaliza chuo akawa anaishi mkoa jirani na wangu). Rafiki alinieleza kila kitu.

Kumbe yule demu ni mke wa mjeda. Na mumewe alienda Sudan, na huko Sudan mawasiliano wakapangana lini wapigiane simu, hivyo siku ambazo zilikua za kupigiana simu alikua anatafuta chochotee na hata ugomvi tu ili nimpe nafasi ya kupiga simu..!!! (wanawake sumuu).

Sometimes alikua ananidanganya ana discussion kumbe alikua kwa rafiki yakee anategea mjeda apige simu. Kwahiyo mimi nilitumika kama "nyeg* remover".

Na akiwa third yr semister ya pili mjeda alirudi, kwahiyo ili a balance mambo aliniaga anakwenda home kuna msiba kumbe alienda kwa mjeda akalala nae wiki halafu kurudi Shule maisha yakaendelea.

Alitaka mjeda aamini mimba ni yake. Maongezi yakaisha, kesho yake nikarudi kazini kuugulia uchungu. 2020 Mtoto akazaliwa na akapewa jina nilililo wahi kulipendekeza mimi.

Rafiki yake akanipigia simu ""xxx kasema hongera kwa kugraduate masters ila yeye kajifungua mtoto wa kike na jina ni hili *** na kaomba ukae nae mbali usije kuharibu ndoa yake maana mtoto SIO WAKO.""

Ikabidi nimuombee rafiki yake anifanyie uspy wa pua na michoro ya viganja ampige picha hizo location halafu anitumie. Alivyoenda kumsalimia mara ya pili akanitumia picha japo kwa wizi, aisee pua kama yanguu na viganja vya mikono vina michoro yangu kabisaaaaa..!!!

2020 hiyohiyo rafiki yake aliolewa ikawa mwisho wa mimi kuwasiliana nae na kwasasa hata sijui yuko wapi. Nikipiga simu naambiwa namba imefungiwa. Kwahiyo sina tena taarifa yoyotee juu ya mwanangu.

Napajua anapofanya kazi huyo demu kwahiyo naweza kwenda hata leo ila SIWEZI KUDAI MTOTO SABABU NAOGOPA KUVUNJA NDOA YA WATU...

Mjeda anajua mtoto wake na alisex nae wiki moja au mbili baada ya kupata mimba yangu. kwahiyo huyu dada akipiga hesabu na mipango yoote ilifanikiwa..!!! (wanawake Nyok*)

NIKAWA MIMEPOTEZA MKE NA MTOTO...!!!

4. MTOTO WA 4.

Mwaka 2019 huyo demu wa 3 alipomaliza chuo (July 2019) akiwa hapatikani, kuna siku niliingia BADOO nikajiokotea manzi. Baada ya chatting tukagundua tupo jirani sanaa (nauli 400 tu).

Tukabadilishana namba.
Nikaomba mchezo, alijibu "mimi siwezi na condom na huku mi nimekuja kwa dada kukaa baada ya kupunguzwa kazini, hivyo kuniona BADOO usidhani mi malaya. Kama kweli umenipenda tukapime then dada akujue halafu tutatomban* mpaka ukinai""

kweli bana tukaenda tukapima wote tupo safi. Akawa Bado ananizingua kunipa mchezo. Nikawa naanza kumpotezea (mi kwake nilitaka game tu).

Baada ya wiki ya kupotezeana ikaingia sms "Tukapime na leo halafu twende kaniagie kwa dada nitoe outing then tukalale kwako" Kweli bana tukapima then tukapitia dukani kwa dada ake tukaaga mi nikaenda kujilia mzigo.

Nilikaa na mzigo naucheketa wikiendi yoote bila condom (ilikua safe days zake). Urafiki ukaendelea mara akapata Bwana mpya mjini (bosi/meneja wa mtandao mmoja hivi).

Kwahiyo tukawa tunamla watu wawili. Na mimi nilijua sanaa kinachoendelea ila sikuwahi kumuuliza alinifanya mjinga nikamuona Malaya. Nikitaka game napewa.

Demu akapata mimba, akaja kuniambia "nakupenda ila najua huna mpango wa kunioa, na nina mimba. Naomba unioe hivyo hivyo hata kama hunipendi""

Nikawa nawaza, cha kujibu. Kuna siku alikuja kulala kwangu akasahau kuweka simu password. Niliichokonyoa simu yake kila kona. FB messenger, Whatsapp, sms za kawaida na kwengine.

Nikaja kugundua kumbe huyu demu anauza kweli, na wanaume wotee kalala nao kwa pesa tena ya one night stand, na inaonyesha ni Malaya mzoefu ila kwangu sijui aliona nini (ye anasema alinipenda).

Nika screen shot sms zotee za kuuza nyuchi yake, halafu nikampotezea. Baada ya kumpotezea wiki hivi, alituma bonge la sms kunilalamikia "kwasababu nina mimba ndio hunitaki tena"

Nikamjibu kwa kumtumia zile screen shots. Aliomba tuonane, nikakubali. Akaanza kunihadithia maisha yake. Anasema umalaya aliuanza tokea yupo sekondari (form 2) na kashatoa mimba kama 5 hivii (secondari tu Katoa 2) na hata form 4 hakufika.

Akahama kwao na kwenda kuanza maisha mkoa mwengine. Anasema club zotee zinamjua na yeye maisha yake yalikua ni pesa ilale "mpe pesa akupe nyuchi" Ila anasema mimi aliniona wa tofauti na ile tukapime ilikua tu kunitega na ndio maana hakuwahi kuniomba hata 100 kwasababu ni kweli ananipenda.

Na anasema japo bado akiwa na mimi katomban* sanaa kwa pesa ila bila shaka hii mimba ni yangu hata nisisite. Hawezi kunisingizia na kwanini anisingizie, na wala haitaji pesa ya matunzo anachotaka yeye mtoto amjue baba Basi. Nilisikitika sanaa na sikujibu nilisepa tu.

Kumbe ile mimba alipelekewa meneja, Meneja akakubali kuoa kabisa. Ile alivyojifungua dada ake aliomba nimsindikize kumpa zawadi mzazi. Tulienda mchana (meneja akiwa job).

Nilienda kumcheki mtoto aisee ni Mimi kabisaa copy na michoro ya mikononi imeongea. Mara October 2020 nikapata transfer kuja mkoa mwengine na yule binti tukapotezana (kila mtu alimdelete mwenzake). Kwahiyo tena SIWEZI KWENDA KUDAI MTOTO KWASABABU MTOTO KAUZWA KWA MENEJA.

NA MIMI NILIOGOPA KUBAMBIKIWA MIMBA NA DEMU ALIKUA MUUZAJI. Na siku zote Malaya ni Malaya tu MI SIAMINI KAMA DEMU ATABADILIKA, THEN NILISITA KUMUOA.

Niliamua kufuta mawasiliano na familia yake yotee ile namba waliyoikua wanaijua chip ilipotea kazini hivyo hatuwasiliani tenaa mpaka leo.

NIMEMUACHIA MENEJA AI ENJOY MAISHA YAKE. Kwasasa nina miaka 31 ila sijui nitaoa lini na kifupi mpango sina (labda 5 yrs to come ndio nitawaza Mambo ya ndoa).

MI NACHOTAKA NI MABINTI ZANGU WA 4 NILEE. ILA SIJUI NITAWAPATAJE. Na hii ndio story yangu ya mapenzi na wanawake wa mjini...
 

Gobole

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
656
1,000
Damu ni Nzito kuliko Maji, km kweli ni wako watakutafuta tu someday..inaweza kua sio leo wala kesho ila watakutafuta tu. Otherwise km una guts nenda kadai watoto wako..wapigie hesabu wakifika 7yrs nenda kawadai.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom