Nimenunua Nondo za kujengea, fundi anasema ni fake

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Nimenunua nondo lakini fundi chuma ambae ndio anazitumia anadai hizo nondo ni fake kwani akizikunja zinavunjika wakati nondo inatakiwa kupinda.

Wapi natakiwa kupeleka sample ya hizi nondo kuzihakiki na nini natakiwa kufanya kudai hasara niliyoingia?
 
Nadhani TBS, Chuo kikuu au Mwenge kwa taasisi ya utafiti wa Majengo usawa wa round about ta kwanza kama unatoka Mwenge kwenda Ubungo nyuma ya maduka mengi ya hardware upande wa kulia.
 
Hili ni tatizo moja kubwa sana ambalo linaweza kupelekea kuanguka kwa nyumba (esp Ghorofa). Tatizo lenyewe ni kutozingatiwa kwa viwango kwenye hivi viwanda vya Nondo. Nondo kabla haijaingia sokoni inatakiwa ihakikiwe ubora wake ambapo hupimwa (Tensile strength - uwezo wa kubeba uzito, pamoja na bending strength - uwezo wa kujikunja). Lakini hivi vyote vinategemea chemical composition especially Carbon Content. Kwa kawaida nondo ili iweze kubalance hizo properties (bending &tensile) carbon content inatakiwa isizidi 0.3 %wt. Ikizidi inafanya chuma kuwa kiguma na kikikunjwa kinakatika (hakipindi).
Kinachotekea ni kwamba, hivi viwanda vyetu vinatengeneza nondo kwa kutumia vyuma chakavu kama spare za magari ambavyo vingi vinakuwa na carbon content kubwa (zaidi ya 4 %wt). Kwahiyo wakianza kuyeyusha carbon inakuwa juu sana, kwahiyo huwalazimu kuishusha mpaka ifike mpaka 0.3 %wt au chini zaidi. Lakini walio wengi inawachukua muda sana na pengine kushindwa kuishusha (zaidi ya 0.5 %wt) na kuamua kutengeneza tu nondo hivyo hivyo na matokeo yake ndo kukatika.Nondo hizi mara nyingi huchanganywa na ambazo zina ubora.
Kwahiyo, unataka kulishugulikia hilo tatizo, inabidi kwanza upime hivyo vitu hapo juu, TBS, then uende kwa huyo aliyekuuzia , yeye anafahamu hizo nondo alikozitoa (kiwanda).
 
Nimenunua nondo lakini fundi chuma ambae ndio anazitumia anadai hizo nondo ni fake kwani akizikunja zinavunjika wakati nondo inatakiwa kupinda.

Wapi natakiwa kupeleka sample ya hizi nondo kuzihakiki na nini natakiwa kufanya kudai hasara niliyoingia?

Mkuu kama uko DAR vifaa vya ujenzi zikiwemo nondo nenda kanunue kwa wale Warusi wanaitwa KAMAKA wapo pale relini Buruguni (Mandela Road). Vitu vyao vina ubora wa kuridhisha binafsi nimenunua vitu vingi sana kwao na bei zao pia ni nafuu mno kuliko sehemu yoyote TZ.
 
nenda ofisi za tume ya ushindani wale watakupa msaada unaostahili pamoja na kuwachukulia hatua kazi yao kubwa ni kulinda maslahi ya walaji hawana longolongo hata ukiuziwa simu feki wanadeal nayo
 
ubungo Asante,

@rmashauri nimenunua tayari, nimemwambia fundi asimamishe kazi ili nitafute namna ya kufanya, nataka nikazipime TBS na kama haziko sawa basi niwadai, maana tutauliwa na hizi substandards!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom