Nimenunua moja ya visimbuzi lakini mpaka sasa sijaona hizo local channels

Gwajima

JF-Expert Member
Sep 6, 2018
253
406
Niliona Tangazo toka TCRA kupitia moja ya vituo vya habari vya Television hapa nchini. Tangazo lilitaka/kusisitiza Watanzania kununua visimbuzi vya Ting, Continental, Digitek na Startimes ili kupata channels za ndani bila malipo.
Nimenunua moja ya visimbuzi hivyo na mpaka sasa sijaona hizo local channels. Nilimsikia pia waziri akizungumza kuwa visimbuzi tajwa hapo juu vingetoa huduma hiyo bure, tena alienda mbali zaidi na kusema tutapokea zaidi ya channels 40 za ndani bila malipo.
Nina maswali mawili tu
1. Waziri na TCRA ni waongo?
2. Ting wameniuzia kisimbuzi kibovu?
 
startimes zipo bure wik mbili,tatizo hata kuunganisha ukute huwez ,mpo kuisema serikali tu
 
startimes zipo bure wik mbili,tatizo hata kuunganisha ukute huwez ,mpo kuisema serikali tu
Mkuu hakuna cha bure.
Ukiona wewe unaona bure basi ujue kuna sababu ya kibiashara ya wao kukuvutia kwa muda tu, lakini kuna mfumo wa kutakiwa kulipia.

Ving'amuzi ni biashara ya kitapeli hapa Tanzania, tena utapeli unaohalalishwa kwa kulipia kodi.
 
acha ubishi ,startimes ni bure kwasasa local channels

japo mm nimekihack naangalia nilizohack na hizo local ni bure wiki ya 2 sasa
 
Naipongeza serikali kwa kurufisha channel za bure Leo. Kwa hili naipongeza saba serikali japo mmetuongezea gharama za Umeme kwa kuwa na visimbuzi vinavyotumia Umeme pia vikiharibika kuvitengeneza kwa hili mmefail mngerudisha analogia ikaenda na digital pamoja tukachagua. Ila Asanten.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom