Nimenunua line ya Halotel, spidi ya internet yao ni kama ya kinyonga

Huko nakotaka kwenda TTCL haijafika bado. Lakini pia review za watu wengi bado hawarecommend ttcl nje ya mji maana hata hapa mjini tu nasikia inaleta shida. Kuna mshikaji wangu yuko Kigamboni anasema akilala chumbani kwake, akilalia ubavu wa kushoto anapata mtandao wa ttcl, akigeuza ubavu wa kulia hakuna mtandao😂
😂😂😂😂😂😂
 
Juzi nimesajili laini ya halotel kwa sababu nina shughuli ya kwenda kufanya vijijini huko nikaambiwa halotel ndio inapatikana huko, sasa ili nisikose mawasiliano ikanibidi kusajili laini ya Halotel.

Baada ya lusajili nikanunua na kifurushi kikubwa cha internet ili nifurahie huduma yao, aisee ni majanga makubwa. Niko hapa Daslam kasi ya internet yao ni ya kinyonga aisee. Sijui ni 2G au 3G ila iko chini sana. Sasa kama hapa Daslam napata kasi ndogo hivi huko bush itakuaje?

Mbadala wa vidacom kwa kasi ya mtandao hapa nchini bado sijaona aisee. Nikitoka bushi hii laini naieeka kabatini.
Jaribu kuitumia ukiwa kwenye chombo cha moto kama piki piki ama baiskeli kwenye mteremko mkali ili kuongeza kasi ya mtandao!
 
User N wengi Now dayz speed ni chini ya kiwango ile 5mb per second downloading speed imebak storY
 
Halotel wanajitahidi sana upande wa internet, speed yao ni nzuri labda kama tu haikua poa kwa wakati huo wewe unatumia. Najiunga Royal bando kwa 10,000/= naperuzi mwezi mzima bila kikomo.
Mkuu mimi pia niko Halotel hivi hii Royal Bando ukiitaka unajiungaje? Tafadhali msaada wako.
 
Halotel unatakiwa uinunulie mkoa husika ukinunulia mkoa mwingine utumie mkoa mwingine majaanga. Mimi nilinunua halotel Morogoro nikija DSM ni majaanga. Inakuwa ipo chini sana, na kwy Internet
 
Back
Top Bottom