Nimenunua kiwanja hakijapimwa naomba ushauri wa kisheria

mtk eng

Member
Oct 18, 2021
92
219
Iko hivi.. kuna kiwanja nimenunua muuzaji kanionesha ramani ambayo imechorwa na surveyor wake ..madai yake kasema alienda ofisi za ardhi kujua eneo analotaka Kuuza ni kwaajil ya makazi au limetengwa kwaajili ya shughuli za serikal na akapata majibu kua eneo ni kwaajil ya makazi.. alichokifanya muuzaji ni kumuita surveyor wake na akamcholea mchoro na ukaonesha unatoa viwanja 8 na vyenye ukubwa wa square meters 500 each one.. na mimi nikafanikiwa kuchukua kimoja.. na tukaandikishana kwa ofisi za kata.. swali langu jee naweza nikaanza ujenzi? Pili je kiwanja kiko salama? Nifanyeje naombeni ushauri wa kitaalamu nisije niingiazwa mkenge..
 
Peleka laki moja kwa afisa mtendaji/serikal za mitaa, waambie wakanywe soda. Tafuta fund anza ujenzi.
 
Unapatikana wapi..?
Mchoro wa mipango miji ndio unao onesha kiwanja chako kimekaaje, na matumizi yake. Savea kazi yake ni kupima ardhi, kuandaa na kuidhinisha ramani ya upimaji.
Kwa kesi yako, kisheria umiliki halali wa ardhi ni kuwa na hati sio maandikishiano ya serikali ya mtaa. Ili upate hati eneo lako lazima liwe limepangwa na kupimwa.
Kwenye kufanya ujenzi inategemea na mahali ulipo na ufuatiliaji wake, kuna sehemu hauwezi kujenga bila kuwa na kibali cha ujenzi, ukitaka kupata kibali cha ujenzi lazima wataanza kufuatilia vitu nilivyokuelezea apo juu.
Karibu inbox kwa ushauri, kazi na maelekezo zaidi.
 
Iko hivi.. kuna kiwanja nimenunua muuzaji kanionesha ramani ambayo imechorwa na surveyor wake ..madai yake kasema alienda ofisi za ardhi kujua eneo analotaka Kuuza ni kwaajil ya makazi au limetengwa kwaajili ya shughuli za serikal na akapata majibu kua eneo ni kwaajil ya makazi.. alichokifanya muuzaji ni kumuita surveyor wake na akamcholea mchoro na ukaonesha unatoa viwanja 8 na vyenye ukubwa wa square meters 500 each one.. na mimi nikafanikiwa kuchukua kimoja.. na tukaandikishana kwa ofisi za kata.. swali langu jee naweza nikaanza ujenzi? Pili je kiwanja kiko salama? Nifanyeje naombeni ushauri wa kitaalamu nisije niingiazwa mkenge..
UTAPIGWAA KUWA MAKINI
 
Mwaga mchanga,ita fundi anza ujenzi, acha uoga wewe!
Mambo ya viwanja inatakiwa huwe kauzu mkuu,

Kuna kiwanja nilikinunua kitambo, siku nataka kujenga majirani Mara sijui umezidi,Mara sijui ilikuaje,
Mi Wala sikuwa na muda wakuwajibu, nilikuwa muda wote nimekula ganzi sicheki na mbwa yoyote,

Viwanja inatakiwa huwe mtata kuliko maelezo,yaan ikibidi huwe mwehu haswaa,kingine nilipakana na mchaga, huyo alitia akili na tamaa zake za ardhi ,

Na hii haswa kwa viwanja ambavyo Ni skwata , kwa ambavyo vimepimwa vina afadhal kiasi
 
Back
Top Bottom