mtk eng
Member
- Oct 18, 2021
- 92
- 219
Iko hivi.. kuna kiwanja nimenunua muuzaji kanionesha ramani ambayo imechorwa na surveyor wake ..madai yake kasema alienda ofisi za ardhi kujua eneo analotaka Kuuza ni kwaajil ya makazi au limetengwa kwaajili ya shughuli za serikal na akapata majibu kua eneo ni kwaajil ya makazi.. alichokifanya muuzaji ni kumuita surveyor wake na akamcholea mchoro na ukaonesha unatoa viwanja 8 na vyenye ukubwa wa square meters 500 each one.. na mimi nikafanikiwa kuchukua kimoja.. na tukaandikishana kwa ofisi za kata.. swali langu jee naweza nikaanza ujenzi? Pili je kiwanja kiko salama? Nifanyeje naombeni ushauri wa kitaalamu nisije niingiazwa mkenge..