NIMENUNUA HP LAPTOP.... ProBook 4530 ina windows 7 nimesikitika kumbe imetengenezwa China

Mmetu-release pressure watu wengi mjue!Mimi mwenyewe juzi juzi nilidaka DELL INSPIRON made in China kwa 1.2 nikajua nimepiga mbizi kwenye lami!
 
Tatizo liko wapi? makampuni karibu yote ya America na Europe yanatengenezea bidhaa Asia.............


Hata yangu ninayotumia ni HP probook na imeandikwa hivyo hivyo imetengenezwa china....haina tatizo mkuu...ninayo kwa

miaka miwili sasa na haina hata dalili ya kunisumbua......
 
wanajamii mimi sion sababu ya kucomprain kuwa laptop au pc zimetengenezwa china siku zote mimi ninaamin matumizi yako ndio yataonyesha kuwa kitu hiki ni china au laa! chamsingi ni kwamba unaweza ukatumia chochote
 
Tatizo liko wapi? Waweza irudisha dukani, umpe data kwamba imetengenezewa china.. Hahahahaha, hauna warranty card??
 
Au iyo si inaitwa laptop? Si inafungua jf? Fb? Inachezesha magemu? Videos.. Basi chekelea
 
Tatizo liko wapi? makampuni karibu yote ya America na Europe yanatengenezea bidhaa Asia.............[/QUOTE
Tatizo hajui, hao Apple tu bidhaa zao zinatenenezwa Uchina ,nina Nokia ilinunuliwa New York imetengenezwa Uchina,kama ulivyosema kampuni karibu zote kubwa States hutengeneza bidhaa zao Uchina.Za Kariakoo ndio ziko kiwango cha chini kutokana na kuwa zinatengezwa na SIDO za China na TBS yetu ndio hiyo nayo imekaa kichinachina
 
Machozi yana nitoka...nimenunua hp laptop 999,999 shillingi....nikijua hp ni kampuni ya marekani only to find imetengenezwa China ...maskini sijui itadumu maana vitu vya china kila mara ni feki
Acha uoga,huwezi kumkwepa mchina,hizo kampuni zinatengeneza bidhaa zao china kwa sababu china kuna cheap labour,raw material na tchnology pia iko safi,unafikiri marekani inauzwa bei hiyo?bidhaa mpya kama hiyo ikitoka usa bei yake ungeikimbia!
 
You should worry kama huna warrant and you did not buy it from an authorized dealer otherwise hiyo kitu iko poa!
 
mleta mada fahamu kwamba CHINA RULES THE WORLD kwa kipindi hiki. Zile bidhaa feki na hafifu tunazolianazo kariakoo huwa zinatengenezwa viwanda vya uani na watoto wa VETA za kule China. Vinginevyo kitu cha mchina wa kiwanda halisi hakina matatizo.
 
Made in China but meant for European market huwa zinakuwa okey sana
Hope na iyo iko ivyo maana HP ni ya ulaya
Wengi wanaipenda China bse of cheap labour thus low production cost which implies higher profit margin if the same would have been made in European countries
 
Machozi yana nitoka...nimenunua hp laptop 999,999 shillingi....nikijua hp ni kampuni ya marekani only to find imetengenezwa China ...maskini sijui itadumu maana vitu vya china kila mara ni feki
hivi unadhani china ndo hamna vitu original? au unahisi kila kinachotoka china ni "cha kichina??"
 
naomba nikutoe woga kwa hili.
kuna kiwanda Taiwan kinaitwa FoxConn ni motherboard manufacturer pia wana pewa deals za kutengeneza electronics kutoka European,American & Japanese companies kama vile Apple na Sony kutokana na gharama za utengenezaji na usafirishaji kuwa chini.

Reference :Foxconn - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Machozi yana nitoka...nimenunua hp laptop 999,999 shillingi....nikijua hp ni kampuni ya marekani only to find imetengenezwa China ...maskini sijui itadumu maana vitu vya china kila mara ni feki

mkuu mbona kawaida ... tu ! mi niliagiza HP marekani tena kupitia website yao .. na customization nahitaji nini na nini.. lakini ilipofika baterry yake made in china .. kule wamefanya assembling tu! ...

si kweli kila kitu made in china kibovu! hii laptop mwaka wa 5 sasa ninayo hata kwa fundi sijawahi kupeleka
 
Back
Top Bottom