Nimenunua bidhaa Zanzibar, bandarini Dar wametaka kodi. Hii imekaaje Jamhuri ya Muungano?

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
Kwani inakuwaje Zanzibar na Tanganyika zimeungana na kuwa nchi moja halafu mimi nimenunua screen kutoka visiwa vya karafuu badae naambiwa nilipie kodi ya tra wakati bidhaa imenunuliwa Tanzania
 
Kwani inakuwaje Zanzibar na Tanganyika zimeungana na kuwa nchi moja halafu mimi nimenunua screen kutoka visiwa vya karafuu badae naambiwa nilipie kodi ya tra wakati bidhaa imenunuliwa Tanzania
watu wanakatwa mpaka kodi kwa ubuyu wa babu issa itakuwa screen, ukitoka zanzibar nao wanakata, ukifika dar nao wanakata, tatizo hata hawa wanaokata ushuru bandarini inabidi wapewe semina, inaonekana kabisa ndani ya nchi kitu unakilipia ushuru mara 3 na hapo kama unaenda tabora napo watakata, mnyonge ananyongwa sana
 
Kwani inakuwaje Zanzibar na Tanganyika zimeungana na kuwa nchi moja halafu mimi nimenunua screen kutoka visiwa vya karafuu badae naambiwa nilipie kodi ya tra wakati bidhaa imenunuliwa Tanzania

Ule kuna ZRB huku kuna TRA sasa hapo ng'amua mwenyewe
 
Ule kuna ZRA huku kuna TRA sasa hapo ng'amua mwenyewe
hapana, kuna tra, zrb yani zanzibar revenue board, makampuni yanalipa kodi mara 2, wanalipa tra na wanalipa zrb, walishalalamika sana lakini sijui kama walipata suluhisho
 
Ndo utaratibu mkuu!!! Waligundua watu wanahamia kuingizia vitu Zenji... It was cheaper kiivyo
 
Hiyo hiyo si ndo alipotoka
12e5ef653e31f19b3057c21028ebc3fb.jpg
 
hapana, kuna tra, zrb yani zanzibar revenue board, makampuni yanalipa kodi mara 2, wanalipa tra na wanalipa zrb, walishalalamika sana lakini sijui kama walipata suluhisho

Asanteh kwa kunisahihisha basi kwenye A weka B hapo ndo nilitaka ujue zinakwendaje
 
kuingiza mzigo zanzibar rates zake zipo chini ukilinganisha na Tanzania Bara. hivyo kwa uelewa wangu kinachofanyika ni mzigo ukitoka zanzibar TRA wanaangalia tofauti kati ya kodi inayostahili kulipwa na ile ambayo tayari ishalipwa zanzibar.TRA wasipofanya hivyo inaweza kuharibu uchumi wa bara kwa sababu mizigo yote itakuwa inapitia zanzibar halafu inaletwa bara. hii itakuwa changamoto
kwa swala la muungano nadhani ni changamoto kwa sasa lakn nadhani ni makubaliano baina ya nchi hizi mbili hasa ili kupunguza kero za muungano.

nimejaribu kushare uelewa wangu
 
Back
Top Bottom