Nimenasa kwenye ulimbo wa ndoa natamani kutoka nashindwa

Noel wa ruben

JF-Expert Member
Oct 11, 2020
364
509
Mimi ni kijana ambaye tayari nina miaka 30, nilifunga ndoa yangu mwaka 2019. Ndoa yangu imekuwa ya furaha kwa miezi 6 pekee baaada ya hapo mambo yaliharibika na sijui ni kwanini.

Nakumbuka siku moja natoka zangu kazini namkuta wife kajamu, nilipouliza kulikoni sikupata jibu, kuanzia hapo hatuna mawasiliano zaidi ya kuwasiliana kama kuna kitu kimepungua nyumbani nitapewa taaarifa.

Uchumi wangu umeyumba sababu ya hizi vurungu, nimefunga nakuomba hakuna ndoa haitulii kuna wakati nikiona mtu na mke wake wakitembea njiani huku wakipiga stori na kucheka naona nijambo la ajabu nijiuliza inawezekanaje hii?

Nimejaribu kushirikisha ndugu zake bado hatoi majibu nini ambacho nilimkosea. Kiukweli nimestuka baada ya watu wawili kuniuliza kwanini nakonda, kwanini sina amani kama zamani?

Mimi ndugu zangu ni bingwa wa kuvumilia matatizo lakini kwa hili nimenyoosha mikono nimeamua niondoke nikaaanze maisha mapya ili nipate amani ya moyo wangu, Mungu ataibarika kazi ya mikono yangu nitainuka tena.
 
Duh pole mkuu! Ila hajawahi kukwambia sababu kabisa? Ama alishawahi kukwambia before ukamuignore sababu ni vitu vidogo vidogo? Je ukimuuliza anakaa kimya au anajibu?

Ila Huyo mwanamke naye aache gubu ,suluhisho ni kuongea, kuombana msahama na kusonga mbele. Kununiana siyo vizuri kwa ustawi wa familia.
 
Mimi ni bingwa wa kutoa ushauri shagharabagara ila kwa hili sitathubutu kutoa ushauri shagharabagara, maana maumivu yako ni makubwa.

U mnyenyekevu sana, vijana wa leo kufunga kwa ajili ya changamoto zao ni ngumu.

Je, mke wako mnasali kanisa moja?

Huenda alipata habari yako ya background ndio iliyomuumiza.

Ila yawezekana kuwa ana pepo mchafu ambaye amemwingia kiasi cha kukuona unanuka na takataka.

Hebu muulize mwambie akuambie tatizo nini.

Funga mlango Jumapili moja mwambie leo humu sitoki mpaka akuambie tatizo
 
Duuuh pole sana mkuu ila ninapata mashaka kuwa kabla hiyo ndoa haijafungwa kuna mambo hayakuwa tayari... sijui its just my intuition ila kwa maelezo yako naona kuna mambo hayakuwa yamekaa sawa upande wa bond baina yako na huyo mwanamke. Me sikuwepo ila I have strong doubt... pole mkuu cha msingi mrudishe kwao kwanza halafu jipange taratibu.
 
Hakuwa na shida ya ndoa, yeye shida yake ilikuwa ni harusi tu ili awaringishie rafiki zake na aweze kupost picha Facebook.

Umri wako bado mdogo sana kuanza kutafutiwa maradhi ya stroke na kisukali.

Tatizo ukitaka show za nje hakuna cha bure inabidi visenti viwili vitatu uwe navyo, piga show za nje tu babu kama ni kweli huyo ni mke atajurudi ila kama shida yake ilikuwa harusi ataondoka mwenyewe.
 
Duh pole mkuu! Ila hajawahi kukwambia sababu kabisa? Ama alishawahi kukwambia before ukamuignore sababu ni vitu vidogo vidogo? Je ukimuuliza anakaa kimya au anajibu?. ila Huyo mwanamke naye aache gubu ,suluhisho ni kuongea, kuombana msahama na kusonga mbele. Kununiana siyo vizuri kwa ustawi wa familia.
Sijui tatizo sasa mwaka na kitu,huwezi amini nakonda mbaya kuishi na mtu ndani lakini kama hatufahamiani vile.na huwezi fanya suluhu na mtu ambae hakuambii umekisea wap.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom