Nimemvunja moyo sana mke wangu, kama una chochote cha kuniambia au kunishauri wewe nishauri tu

Rodriquz

Member
Aug 13, 2020
37
139
Kawaida ya wanaume tumeumbiwa tamaa, hakuna mwanaume asiyemsaliti mke wake iwe sirini au wazi wazi, mimi na mke wangu tumepitia changamoto nyingi sana kwenye maisha, amenivumilia kwa mengi toka ajifungue amekuwa wa hospital tu anatoka leo anarudi kesho.

Mimi naishi mbali nae kwa sababu ya kazi ninazofanya, kwahiyo anasema watoto wanamsumbua sana, shida imeanzia pale nilipomtongoza rafiki yake mara ya kwanza alikuja kugundua baada ya huyo rafk ake kuweka mambo hadharani, niliaibika tukasameheana yakaisha, juzi nikatest tena kwa huyo huyo rafk ake dah!

Kisicho riziki hakiliki, sijui kama atanisamehe, tulipanga tuonane leo na huyo rafiki yake bahati mbaya tena mipango yetu imejulikana maana rafiki yake alienda akasahau simu kwa mke wangu na msg tulizochati zimeonekana, mke wangu amenilaumu sana kwanini namfanyia hivi tena kwa rafiki yake kabisa, ila kiukweli sijawahi kutembea nae huyo rafiki yake wala kufanya nae chochote, sasa nimeshkwa na ngozi, nijitetee vipi nipeni mbinu basi?
 
Tamaa mzee shida ni tamaa, hivi kwanini huwa mnapenda kusema wanaume sisi hatuwezi kuishi na mwanamke mmoja hiyo mentality aliekuambia nani, ulisikia wapi, jisemee nafsi yako mkuu, sema wewe huwezi kukaa na mwanamke mmoja, ni kujiendekeza tu
 
Nashindwa kuwaelewa, hivi unaanzaje kukamatwa? Mie hapa nilipo nakula mdogo wa wife, na mchepuko wangu wa siku nyingi kabla hatujafunga ndoa! Ni family friend kabisa mpaka wanasaidiana kwa shida na raha, wife hajawahi hata kuhisi tu! Njoo inbox nikupe mbinu, hutakamatwa tena!
 
Ndoa ni kwa ajili ya wanaume wenye akili tu!
Kama unajijua wewe ni ndunga embe ukijichanganya kuoa matokeo yake lazima yawe kama yaliyokukuta wewe
Wengi snaaaaa wapo tu mitaani wamejaa kibao wanaume bila mchepuko, nashangaa kauli za kusema sisi wanaume sijui nini, sisi wanaume tuko hivi hao sio wanaume ni aina ya mashetani tu, mwanaume unaanzaje kumsaliti mkeo tena na rafiki yake madharau ya kipuuzi hata shetani anashangaa.
Safi sana bora umesema haya wewe mwanaume.

Hao wanataka kuhalalisha ubaradhuri wao eti ni"nature" kumbe kujiendekeza tu.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom