Nimemuona Hassan Mwakinyo akipigana, maoni yangu ni haya

choupa moting

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,508
2,553
Niwe tu muwazi kwamba mimi si mtaalamu wa mambo ya boxing ila ni mfuatiliaji na mshabiki wa mchezo huu toka enzi za akina Tyson za kuamka alfajiri kusubiri pambano na Lewis. So ni shabiki wa mchezo ila si mwenye taalum nalo.

Jana majira ya saa nne usiku kulikuwa na pambano la masumbwi lililowakutanisha mtanzania mwenzetu Hassan Mwakinyo mwenye umri wa miaka 24 na muajentina Sergio Gonzales mwenye miaka 40.

Binafsi nililisubiri sana kwa hamu pambano hilo kutokana na ukweli kwamba nilikuwa sijawahi kushuhudia pambano la mtanzania mwenzangu Mwakinyo akipigana live zaidi ya kuona vipande tu vya youtube.

Jana nikatoka zangu mihangaikoni mapema kurudi nyumban kuona ndondi.

Ndondi zilikuwa za round 8 katika pambano ambalo halina mkanda. Lilianza round ya kwanza kwa kusomana mchezo baina ya wapinzani hawa wawili.

Kwa muda mfupi niliona kitu kwamba yule mzungu japo alikuwa umri umeenda lakini yupo makini sana ukimlinganisha na ndugu yetu ambaye mara zote alikuwa anarusha ngumi upepo bila kufika target.

Kwa mtu aliyeona pambano atakubaliana na mimi kwamba Mwakinyo alikuwa anapigwa sana ngumi za uso mpaka akaanza kupanic.

Hii ilimpelelea kuanza kurusha ngumi hovyo kabsa ndio zile zikawa znampiga jamaa mabegani na tumboni.

Mpaka round ya tano ambayo mzungu amekaa chini ni zile jamaa kampiga begani mkono ukashindwa kufanya kaz mwamuzi akaamua kuahirisha pambano kwa mahesabu ya TKO.

Maoni yangu ni kwamba the guy ni mzuri sana endapo atapata kocha mzuri atafika mbali maana umri bado unaruhusu ndio kwanza ana miaka 24. Lakini pia mwili wake umefanana na huu mchezo ambapo ndio credit kubwa pia.

Hassani bado hajaiva kuwa bingwa wa dunia wa kuweza kuhimili mikiki ya walimwengu kwenye uwanja wa boxing.

Kwa upiganaji wa jana kama angekutana na mtu mwenye ngumi nzito basi pambano lingeisha round ya tatu kwa yeye kupigwa.

Ongeza sana bidii ya mazoezi hasa upande wa kucheza na sura ya mpinzani wako.

Uzuri ni kwamba umekuja kipindi ambao nchi ina mwamko kwenye michezo na mambo mengine hivyo support unaipata, wenzio wakina Matumla walipigana kipindi hata google hakuna achana na whatsapp, facebooka au instagram.

Kila la kheri katika maisha yako ya michezo.
 
mmmh.! kumbe ana miaka 24.? kweli maisha tunatofautiana, me nina 20 lakini naonekana mzee zaidi yake.
Dk0G6kvW4AAQZzC.jpg
 
Umeandika vizuri , sema Gonzalez alikuwa mjanja Sana Kwa kuwa alikuwa ana pinda hivyo kuikwepesha Sura yake ,sehemu yake rahisi kuifikia ilikuwa ni mabega, kingine kwenye ngumi ni lazima kuna kipindi upumzike hili kumsoma mpinzani wako
 
nimeuona ulempambano jamaa alikuwa anatumia ufupi kumsogelea hasan na kurusha upper cut lakini hasan alisha mstukia akaona amalize pambano mapema big up hasan kwa kuipeperusha bendera ya tz vema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania yetu hii ngumi nzuri ipo Dar tu, wachezaji wote wa mikoani wananguvu (punch zenye nguvu) wavumilivu sana tatizo hawana technic za ngumi, Dar wachezaji wazuri sana wa ngumi skill, technic inaleta radha hata kwa mashabiki ila sio wavumilivu na pia ngumi zao hazina madhara kushinda kwao ni point tu au wapoteze, kiufupi bado tunachangamoto sana kwenye hi tasnia ya masumbwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marehemu Thomas Mashali, Mbwana Matumla hawa ndio walikuwa maboxer, Marehemu Mashali alikosa discipline ya maisha akapotea.. Kwa sasa namuona Dullah Mbabe anakuja vizuri huyu Mwakinyo amepata promota au management nzuri inambeba lakini ni wa kawaida sana..

Watanzania wenzangu michezo ni fursa hebu wale wenye vipato mjaribu kuchukua management ya hawa watu kuanzia boxing, football na basketball.. Uwekezaji kwenye tasnia ya sports unalipa..na Tanzania vipaji viko vingi tatizo havifikiwi na hakuna watu serious wakuendesha hii biashara.. Nawaona maboxer wengi sana uswahilini huko ambao kama wanapata bahati ya kuingia kwenye ring za USA na EUROPE ni biashara kubwa sana..
 
Ni kweli kabisa mkuu
Niwe tu muwazi kwamba mimi si mtaalamu wa mambo ya boxing ila ni mfuatiliaji na mshabiki wa mchezo huu toka enzi za akina Tyson za kuamka alfajiri kusubiri pambano na Lewis. So ni shabiki wa mchezo ila si mwenye taalum nalo.

Jana majira ya saa nne usiku kulikuwa na pambano la masumbwi lililowakutanisha mtanzania mwenzetu Hassan Mwakinyo mwenye umri wa miaka 24 na muajentina Sergio Gonzales mwenye miaka 40.

Binafsi nililisubiri sana kwa hamu pambano hilo kutokana na ukweli kwamba nilikuwa sijawahi kushuhudia pambano la mtanzania mwenzangu Mwakinyo akipigana live zaidi ya kuona vipande tu vya youtube.

Jana nikatoka zangu mihangaikoni mapema kurudi nyumban kuona ndondi.

Ndondi zilikuwa za round 8 katika pambano ambalo halina mkanda. Lilianza round ya kwanza kwa kusomana mchezo baina ya wapinzani hawa wawili.

Kwa muda mfupi niliona kitu kwamba yule mzungu japo alikuwa umri umeenda lakini yupo makini sana ukimlinganisha na ndugu yetu ambaye mara zote alikuwa anarusha ngumi upepo bila kufika target.

Kwa mtu aliyeona pambano atakubaliana na mimi kwamba Mwakinyo alikuwa anapigwa sana ngumi za uso mpaka akaanza kupanic.

Hii ilimpelelea kuanza kurusha ngumi hovyo kabsa ndio zile zikawa znampiga jamaa mabegani na tumboni.

Mpaka round ya tano ambayo mzungu amekaa chini ni zile jamaa kampiga begani mkono ukashindwa kufanya kaz mwamuzi akaamua kuahirisha pambano kwa mahesabu ya TKO.

Maoni yangu ni kwamba the guy ni mzuri sana endapo atapata kocha mzuri atafika mbali maana umri bado unaruhusu ndio kwanza ana miaka 24. Lakini pia mwili wake umefanana na huu mchezo ambapo ndio credit kubwa pia.

Hassani bado hajaiva kuwa bingwa wa dunia wa kuweza kuhimili mikiki ya walimwengu kwenye uwanja wa boxing.

Kwa upiganaji wa jana kama angekutana na mtu mwenye ngumi nzito basi pambano lingeisha round ya tatu kwa yeye kupigwa.

Ongeza sana bidii ya mazoezi hasa upande wa kucheza na sura ya mpinzani wako.

Uzuri ni kwamba umekuja kipindi ambao nchi ina mwamko kwenye michezo na mambo mengine hivyo support unaipata, wenzio wakina Matumla walipigana kipindi hata google hakuna achana na whatsapp, facebooka au instagram.

Kila la kheri katika maisha yako ya michezo.
I.Nami nilibahatika kuliona lile pambano huyu Bro Mwakinyo ana kazi ya ziada
 
Marehemu Thomas Mashali, Mbwana Matumla hawa ndio walikuwa maboxer, Marehemu Mashali alikosa discipline ya maisha akapotea.. Kwa sasa namuona Dullah Mbabe anakuja vizuri huyu Mwakinyo amepata promota au management nzuri inambeba lakini ni wa kawaida sana..

Watanzania wenzangu michezo ni fursa hebu wale wenye vipato mjaribu kuchukua management ya hawa watu kuanzia boxing, football na basketball.. Uwekezaji kwenye tasnia ya sports unalipa..na Tanzania vipaji viko vingi tatizo havifikiwi na hakuna watu serious wakuendesha hii biashara.. Nawaona maboxer wengi sana uswahilini huko ambao kama wanapata bahati ya kuingia kwenye ring za USA na EUROPE ni biashara kubwa sana..
Sio kweli mkuu, mwakinyo Yuko vizuri , kama hasingekuwa vizuri hasingempiga Sam egginton, mbwana yes alikuwa vizuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom