Nimemuambia huyu secretary nikirudi nisiikute

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Leo nimeanza kibarua kwenye hii kampuni, ofisi nitakayokuwa naitumia nimekuta kuna picha tatu ukutani, ya Mwalimu, Ben na ya Mr. Pilot. Nimemuambia huyu Secretary nikitoka lunch nikute amekwishaondoa picha ya Ben, zibaki hizo mbili, Kwa heshima ya ofisi yake kwa Taifa letu hii ya Mr.Pilot nitaendelea kutafuta busara namna ya kudeal nayo.
 
Bakiza moja tu ya mwalimu, mm dukani kwangu nimeweka ya mwalimu, akija mteja kabla sijamtajia bei ya bidhaa kwanza naiangalia picha ya mwalimu inanikumbushia kipindi kile cha foleni kununua kipande cha sabuni. hii picha inanipa ujasiri wakukutajia bei kubwa.
 
Hiyo ofisi ni museum?...Uko Makumbusho ya Taifa nini jomba?
Kwanini kuwe na picha ya MkaaHapa, halafu kusiwe na ya Mwinyi?
Kama wameamua kutunza picha za marais wastahafu basi watundike za marais wote!
 
Ebwana eeh MR Pilot..ila kweli kwa jinsi Vasco da Gama anavyosafiri sana hatofautiani na Pilot wa Precision Air-ways..utafikiri yeye ndio mrusha ndege!!
 
Leo nimeanza kibarua kwenye hii kampuni, ofisi nitakayokuwa naitumia nimekuta kuna picha tatu ukutani, ya Mwalimu, Ben na ya Mr. Pilot. Nimemuambia huyu Secretary nikitoka lunch nikute amekwishaondoa picha ya Ben, zibaki hizo mbili, Kwa heshima ya ofisi yake kwa Taifa letu hii ya Mr.Pilot nitaendelea kutafuta busara namna ya kudeal nayo.

Pamoja na kuwa wewe ni senior expert Member, hii mada umeiweka hapa kuongeza post na si hadhi yako.
 
Mkwara mbuzi huo...acha utoto
Hizo picha hazihusiani na kazi...piga mzigo n make a difference...

Aise watu naona hamjui sharia, nakumbuka wakati ben amechaguliwa kuwa Rais, baada ya siku moja tu PALE MAHAKAMA YA KISUTU kuna kesi ilishindwa kuendela mpaka picha ya Rais Mtukufu Mwinyi ilipoondolewa! sasa sielewi huu usemi wako labda watu wa sharia watujuze !
 
Bakiza moja tu ya mwalimu, mm dukani kwangu nimeweka ya mwalimu, akija mteja kabla sijamtajia bei ya bidhaa kwanza naiangalia picha ya mwalimu inanikumbushia kipindi kile cha foleni kununua kipande cha sabuni. hii picha inanipa ujasiri wakukutajia bei kubwa.

Nimecheka mpaka machozi yamenitoka ! dah! ukiudhika tu ingia JF utatoka unacheka mpaka ! teh teh teh aaah! kile kibabu nacho kilikuwa nuksi kweli kweli !
 
Mkwara mbuzi huo...acha utoto
Hizo picha hazihusiani na kazi...piga mzigo n make a difference...
Zinauhusiano mkubwa sana, ninategemea kuwa natumia si chini ya masaa nane ndani ya ofisi hii, kwa hiyo ni lazima nihakikishe inamazingira yote ya kunifanya nifurahie kuwa humu ndani, kwa hiyo ni sahihi kabisa kuondoa vitu vyote ambavyo vinaweza kuniondolea furaha yangu.

Kumbuka kazi sio utumwa.
 
Uko huru kuelezea hisia zako..wasikutishe!
 
Hiyo ofisi ni museum?...Uko Makumbusho ya Taifa nini jomba?
Kwanini kuwe na picha ya MkaaHapa, halafu kusiwe na ya Mwinyi?
Kama wameamua kutunza picha za marais wastahafu basi watundike za marais wote!
Walioziweka wanajua kwamba mwinyi ndio kiongozi mbovu aliewahi kutokea africa!,

Nchi yangu aliirudisha utumwani
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom