Nimemuadhibu mdogo wangu sasa wazazi wana hasira nami

goodhearted

JF-Expert Member
Feb 15, 2015
967
1,207
Leo sina amani kabisa, nimempiga mdogo wangu kipigo cha mbwa mwizi.

Ni hivi, mimi nipo mkoa wa mbali kikazi. Nimekuja likizo home. Niliyokutana nayo ni bora nisingekuja hata likizo.

Nimekuta mdogo wangu ambae yupo form three kawa mhuni kupindukia. anaingia nyumbani usiku kuanzia saa3, mwanafunzi anamiliki simu, hana adabu hata kwa simu ya mama yake. utakuta kakopa salio bila taarifa ya mama na mama akiweka vocha anakatwa bila kujua lolote anabaki tu kulalamika bila kuchukua maamzi yoyote kama mzazi.

Yote tisa, kumi nimempa bi mkubwa kiasi cha elf 40 kwa ajili ya manunuzi ya kitu flani bahati mbaya kaisahau pesa kitandani kurudi anakuta elf 30, kumi hainekani. Nimeconect umiliki wa simu wa dogo huku hana chanzo cha mapato na upotevu wa pesa nikakonclude kuwa ni yeye tu ndo aliechukua.

Mbaya zaidi nimeiangalia simu yake na kuona kabloc line kumuuliza anasema eti mtoto ndo kaiblock nikahisi amefanya makusudi ili kuvuruga ushahidi.

Kiukweli nimempa kipigo heavy na ukizingatia nimetoka JKT hata miaka miwili haijaisha basi kala doso la uhakika mpaka majirani waliingilia.

Sasa kinacho niumiza si baba wala mama wote wananichukia.
Nimeamua kuondoka home kwa muda bila kuaga ili nitulize hasira zangu na nimepanga baada ya hapo nikachukue begi langu nirudi kazini.

Hivi kwanini wazazi wanapenda kuwatetea watoto watukutu. Eti anaomba hela ya tuition wakati anamiliki simu hivi kweli huyo ni msomaji? Je anawezaje kukosa pesa ya tuitiona na kupata hela ya kununua simu?

Iam so frustrated, ushauri tafadhali.
 
Usiumize kichwa...chukua begi lako na ondoka hapo nyumbani....mimi pia ilishawahi kunitokea ishu kama hiyo ila dogo yeye aliku mdokozi na hataki kuwasaidia wazazi..yeye siku nzima ni kuzurura tu nakuiba vitu vya watu kesi inakuja nyumbani...Nilimtega sikumoja kaingia kweye 18 zangu nikaongea na mwenyekiti tukampa kakipigo na kumpeleka polisi bila wazazikujua..kule alipewa kipigo kila asubuhi na jioni na msosi nilikua nampelekea...sasa wazazi walivyojua...duu..walinichukia mbaya ila yule dogo alivyotoka amekua na adabu hata kuliko mm...anachapa kazi mbaya hadi wazazi waliniita na kunishukuru...
Wewe ondoka home kuna siku watakukumbuka.
 
Umefanya vizuri kuondoka ili hasira ipungue, ila sikushauri ukatize likizo for such a minor thing. Kha umepita jeshi kweli wewe kitu kidogo tu hicho you want to pack and leave? Ukioa/ ukiolewa je?

Ukishakuja kuwa mzazi utaelewa kwanini wazazi wako wako vile towards huyu mdogo wako. Halafu pia inaelekea huyu ni mjukuu wao yaani yule mtoto wa uzeeni so wana-take it slow na yeye, ni tofauti ulipokua unakua wewe wazazi walikua bado vijana na wana nguvu wana weza kuhimili mikiki ya kukimbizana na teenagers. Pia huyu dogo (she or he?) ndio yuko katika umri matata anachohitaji ni kuelekezwa zaidi kuliko kipondo cha kijeshi, na siku nyingine na yeye mkatieko kidogo walau kawekundu kamoja kha kaka/ dada gani mbahili hivyo tena siku nyingine atakuchomolea mwenyewe (joke)
 
Saf sana mkuu umefanya jambo la muhimu sana atlist umeonyesha tofaut ya kuwa mkubwa kwenye familia....
 
Ukute mpo nae humu,,,, huwez jua unapoleta hela hom nae pia huleta kupitia hyo sim na kitendo chakuibloc usipende kuhsi sana,,, kama na yey ana mtu anaemtoa out ulitaka uyadabe mawasiliano yao?? madogo wa ck iz atakam ni ME wanao masuga mamy halikadhalka na kw KE..... usijion we ndo mtoaji hela sana hom huwez jua na dogo nae labda anatoaga,,,,,,, kitendo cha wazaz kukacrk n haki iLI wakuOnye maana nyie wa JKT mnaweza mtundka mtini mtu hvhv na akafa mbele y wazaz--- mi naona n haki YAO.
 
Hizi ishu ni shida sana,nakaa na mtoto Wa Shemeji yangu kaja mjini kurudia mtihani Wa form four.Baada ya kuuzoea mji na kupata wababa wa mjini kaanza kunipanda kichwani,bahati mbaya mama yake huko nyumbani hatoi ushirikiano ye ni mwendo wa Lawama na kejeli.Nimeamua moja mtoto arudi akakae na mama yake.

Staki kukaa na ndugu wajinga wajinga
 
Dah!!! Nakumbuka nilitoa dozi moja ya hatari sana kwa mdogo wangu wa kike.Alikuwa anataka kutoka huku akiwa amevaa kama changudoa fulani hivi. Nikamuuliza uanenda wapi eti na yeye akaniambia mbona wewe ukitoka hapa huwa hauulizwi nikapatwa na hasira za ajabu sana kitoto cha mwaka 1992 kiniulize mimi shit kam hiyo.
Baada ya ile adhabu wazazi walinichukia sana ndio ikawa sababu ya mimi kuhama kwenye nyumba ya wazazi wangu kwa sababu nikaona itafika siku hata huyu dogo ataleta dharau nitashindwa kutoa adhabu.
 
Hizi ishu ni shida sana,nakaa na mtoto Wa Shemeji yangu kaja mjini kurudia mtihani Wa form four.Baada ya kuuzoea mji na kupata wababa wa mjini kaanza kunipanda kichwani,bahati mbaya mama yake huko nyumbani hatoi ushirikiano ye ni mwendo wa Lawama na kejeli.Nimeamua moja mtoto arudi akakae na mama yake.

Staki kukaa na ndugu wajinga wajinga

kweli kabisa mkuu, hawa watoto wa ndugu ndo shida kabisa. mi bora lawama kama ni kumsaidia ni akiwa kwao.
 
kweli kabisa mkuu, hawa watoto wa ndugu ndo shida kabisa. mi bora lawama kama ni kumsaidia ni akiwa kwao.
Aiseeee we acha tu binti kasaidiwa kwa kiwango kikubwa kwa kadiri ya uwezo wangu ila mwisho nimeishia kupata lawama.Nimeamua moja tu arudi kwao bora lawama kuliko hizi karaha ninazopata
 
tatizo mkuu shee-eagle,huyu dg nilisha kaa nae sana kumshauri. mwanzo alionekana kama kunielewa lakini nilivyorudi tem hii nimemkuta amebadilika tena sana.
Ndo maana nikaona angalau nitumie nguvu za kijeshi kidogo!!
 
Dah! yaani matatizo ya familia yanalingana sana. wazazi wakianza kuzeeka wanakuwa ni wagumu sana kusimamia maadili ya watoto,Wao hupenda kutetea hata uovu na ujinga. mm baba yangu anapenda sana kumdekeza mjukuu wake yaani mtoto wa marehemu dada yangu hata mkimtuma anakataa akijua babu yake atamtetea. sasa mtoto yule kakua anaingia kidato cha sita. ni hashikiki jamn. akitumwa akanunue kitafunwa cha kula yeye mwenyewe mpaka apewe hela ya vocha ndo aende. uwiii lol.
Yaani mimi mwanangu siwezi kukubali aende kwa babu yake kukaa zaid ya wiki. maana izo siku 2 tu anazoenda akirudi anakuwa kama alienda kozi ya madeko.
 
...pole, kikubwa rudi waombe msamaha wazazi na dogo baada ya hapo ondoka na achana na kumsaidia dogo, wasaidie wazazi kwa kiasi. Ila dogo akipinda mpaka kufikia hatua ya kuwapiga wazazi au kuwaibia au hata kuwaua wewe wakumbushe.
 
...pole, kikubwa rudi waombe msamaha wazazi na dogo baada ya hapo ondoka na achana na kumsaidia dogo, wasaidie wazazi kwa kiasi. Ila dogo akipinda mpaka kufikia hatua ya kuwapiga wazazi au kuwaibia au hata kuwaua wewe wakumbushe.

kuomba msamaha tena kwa mkosefu!!? sdhani, ila stahangaika nae tena hata kama wakinisakama sitajibu lolote nitakuwa kimya kabisa kama bwege flani hivi. Malengo na mikakati niliyoipanga kwa wazazi yote nitaitimiza japo sitaitimiza kwa haraka kama nilivyokuwa nimeplan

Ila dg labda abadilike na aje aniombe msamaha vinginevyo atakapomaliza form four na kufail huo ndo utakuwa mwisho wa mawasiliano na yeye
 
Pole kwa misukosuko,ndio mambo ya dunia kumbuka kua kuna wazazi wengine hua wanampenda mtoto mmoja mpaka mwisho wanamuharibu,sawa ni mdogo wako lakini wao nikidonda chao usiguse,sikunyengine usimpige mtu hata kama umekasirika vipi jaribu kujizuwia au kama unakereka uondoka,manake kipigo hicho ungemuua mbona unagesahaulika kama ulikua duniani sababu hakuna wakukutetea,bila kusahau hao ni wazazi pindi utakapo rejea kuchukua bag lako ongea nao
waombe msamaha sababu umewakera najua its not fair lakini fanya sababu wewe ni mtoto,wambie samahani nimewakera
kwakumpiga mdogo wangu ila sio kwa nia mbaya nikwakumkanya ili ajue alichofanya sio sawa na akumbuke sisi ni binadamu
leo tuko hai kesho tumekufa,atakua anaishi na watu wengine ambao hawatomelewa mapungufu yake. baada ya hapo unaweza
kuondoka trust me wakikaa peke yao watatafakari...

Mtoto wa Mamangu mdogo alianza kula unga lakini mama yake alivyokua anampenda akawa anasema watu wanamchukia
akaanza kuiba mara cm mpaka alipoibiwa yeye cm mpyaaa na mwizi huyo alifungua chandarua akachukua cm tuu hapo ndio akasema huyu mtoto mwizi,tukamwambia ampeleke police alituchamba mpaka basi leo hii mtoto kawa teja lakupepe
anakwenda msikitini anasema mamangu kafa nisaidieni nauli anapewa akitoka hapo ni unga kwakwenda mbele,
mama mtu bado anasema mwanangu karogwa na kutoa laana kuwatupia wanawe wengine.. sasa wazazi hua na tabia flani
na huwezi kusema chochote na hasa mtoto anaependwa akajua ndio anazidi kuharibika,chamsingi waombe mungu wazazi wako na wewe Inshallah mwenyezi mungu akupe moyo wa Subra ...
 
Back
Top Bottom